Sunday, October 30, 2011

NINAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA, NINAPENDA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUFIKA JUMAPILI YA MWISHO YA MWEZI HUU!!!

Hapa katika picha ilikuwa mwezi wa saba wakati nikiwa Ruhuwiko. Kama kawaida Kapulya hakukosa kumdadisi BABA PADRE wakati alipofika nyumbani kwake kusoma misa ya kumkumbuka mpendwa wetu Asifiwe.

Jumapili ya leo nawaomba muungane nami na kuimba wimbo ni katika nyimbo za zamani za Bikira Maria...ambazo ni nyimbo maarufu sana ziliimbwa sana karibu na kila mwumini, naamini mtakuwa mnaufahamu ni huu hapa haya tuimbe pamoja moja, mbili, tatu :- "Sisi wana wadunia tukumbuke maneno aliyosema Bikira Maria, alipo watokea watoto wa Fatima; Lucia, Francisco na Yasinta, alisema tusali....tusali rozari na tupate amani, na tuwaombee wale wakosefu wasio na mwombezi". Ahsante kaka Baraka Chibiriti kwa kunikumbusha wimbo huu:-)

Hata hivyo naona tusikilize na nyimbo nyingize za zamani pia....

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!!!!

6 comments:

Simon Kitururu said...

Jumapili njema kwako pia Yasinta!

Asante kwa wimbo pia ingawa siye wngine hasa tutokao katika DINI na IMANI zimrukazo BIKIRA MARIA huu wimbo ni mpya ila mtamu!

R.I.P Asifiwe!

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa kunitakia jumapili njema..ila kuna kaubaridi leo hapa. Bahati mbaya nimeshindwa kujirekodi ili mngesikia jinsi unavyoimbwa:-)

ray njau said...

@Simon & Yasinta;
Asanteni sana kwa salamu za wikiendi[Jumapili] na ni furaha yangu kuwa imemalikiza kwa amani na furaha.

Baraka Chibiriti said...

ASANTE SANA DADA YASINTA....NAWE PIA NA FAMILIA YAKO, J2 NJEMA.

Anonymous said...

Hizo nyimbo ulizoweka nimechanganyikiwa sana! kwa nini sikuzisikiliza ijumapili? kumbukumbu mhimu sana.BIGUP Yasinta/Jasinta

Robsson said...

hello dada yasinta aisee kama una hii albamu tafadhali dada naomba unitumie hizo nyimbo nipo ughaibuni kwa muda sasa sijafankkiwa kuzipata hizo nyimbo na nimetafuta sana tafadhalini na wadau wengine ikiwezekana saidia mie tafadhali email yangu ni nrbanzi@yahoo.com