Tuesday, October 25, 2011

KAKA SHABAN KALUSE APATWA NA AJALI YA GARI/DALADALA NA KUVUNJIKA MKONO WA KULIA!!!

Nimeamka asubihi hii na kukutana na ujumbe huu kwenye simu yangu ya kiganjani kutoka kwa kaka yetu na wanablog mwenzetu Shaban Kaluse, ujumbe unasema hivi:- Dada Yasinta nimegongwa na gari. Naomba uwajulishe wanablog kwamba nimepata ajali na niko AMANA ILALA kwa matibabu. Nimevunjika mono wa kulia. Nilikuwa navuka barabara maeneo ya Tabata Mawenzi ili kupanda daladala, nikagongwa na daladala lingine ambalo lilikuwa likiovertake kushoto ili kuwahi abiria, mimi sikuliona kabisa. Namba za hiyo daladala ni T 837 AUK.

11 comments:

ISSACK CHE JIAH said...

pole sana mwenzetu msomaji wa blog yetu ya maisha hayo ndo maisha mungu atakupa heri utapona na utaendelea na shughuli zako .
usijali na pata faraja na soma maisha na mafanilio

Anonymous said...

pole sana mpiganaji mungu akupiganie upone haraka uje uendeleze libeneke!

Mija Shija Sayi said...

Pole sana Kaka Kaluse, Mungu atakuponya..

Jamani nchi yetu ina hatari sana..yaani watu wanajali pesa tu hata usalama hawaangalii tena, Hebu angalia kama ajali hii ilivyotokea!!

Mungu yuko nawe kaka Kaluse.

Rachel Siwa said...

Pole sana kaka Kaluse,Mungu yu pamoja nawe.da'Mija wanawahi kula vichwa basi hata wakkiuumiza wewe hawajali.

Simon Kitururu said...

Pole sana Ambiere Kaluse!

Mbele said...

Pole sana. Nakuombea upone mapema.

Anonymous said...

Mungu ni mwema anaweza na ana makusudi yake,hayo ni mapito tu. Prayer,blessings and Courage!

Sara Chitunda said...

Pole sana Kaka kwa kupata ajali, nimepokea taarifa hii kwa masikitiko makubwa ila Mungu yupo yeye ni muweza wa yote atakusaidia utapona haraka.

Penina Simon said...

Mkono wa mungu usiopungukiwa, usimpungukie bali uwe ukimgusa kila siku na kumpatia uponyaji wa haraka,

o'Wambura Ng'wanambiti! said...
This comment has been removed by the author.
o'Wambura Ng'wanambiti! said...

operation yake imekuwa ikipigwa danadana...jana nilipoongea naye alidai kwa anatarajiwa kufanyiwa saa 10 jioni.

Tutaendelea kuwajuza yanayojiri!