Thursday, October 6, 2011

Salt in My Porridge:- SAVE THE CHILDREN TANZANIA/ Chumvi Kwenye Uji:- Okoa Watoto Tanzania!!!


Nimeguswa sana na habari/document hii...sijui mwenzangu.

13 comments:

Rachel Siwa said...

Mmmmmmhhhhh Nchi yangu Tanzania, mimi na wewe tunaweza kusaidia hata kidogo,kama Nguo, vifaa vya shule au chochote kidogo, Nyumbani ni Nyumabani, Tatizo jee vitawafikia walengwa? najiuliza tuu.

Yasinta Ngonyani said...

Da´Rachel utafikiri ulikuwa unasoma mawazo yangu kweli vitawafikia walengwa...maana nilikuwa nawaza hii sukari ambayo mimi situmii kwenye chai yangu kama huyo anayetumia chumvi angapata si anganishukuru sana. sasa swali ndo hilo...

Rachel Siwa said...

Kabisa dada yangu!Sasa tufanyeje da'Yasinta na wewe unaesoma hapa.Ukiangalia kuna kunguo hata kama hatuna uwezo wa mpya,lakini kuna ambozo ni bado nzuri kabisa watoto wetu haziwatoshi, tuna rudi palepale.

Yasinta Ngonyani said...

Naona cha kufanya ni kujizatiti na kupeleka tu zikifika na zifike na kama hazifiki basi. Ila lazima kutakuwa na utaratibu fulani labda tufanye utafiti kwanza. wewe unaonaje?

Rachel Siwa said...

Sawa dadake hilo ni jambo jema, nipo nawe bega kwa bega dada.

mangi said...

Kutoa ni moyo na wala siyo utajiri.Mawasiliano na walengwa kupitia mamlaka husika yakifanyika bila shaka programu hii itafanikiwa.Uwajibikaji wa pamoja ndiyo msingi wa utendaji huu.

sam mbogo said...

Naomba nitofautiane nayi dada zangu kidogo. sukari siyo muhimu kiivyo,badala ya sukali mbona tuna asali ambayo tena kwa afya ni namba moja.kwa hiyo wewe Yasinta una juwa kwanini hutumii sukari,huku kwetu tz vitu kama sukari(chai),wali,nyama,kuku vina weza kusababisha mvurugano sana ama mkubwa katika familia.wakati ukiviangalia vyote nilivyo taja hpo juu vina tuadhiri kima wazo/kimtizamo tu,hivyo watu nikuelimishwa kwamba wali ni chakula cha kawaida,kuku niwakawaida tu kila mtu ana haki kumla kwa nafasi yake. chai ya weza kunyweka bila sukari na wala siyo kitu cha kusikitika ukikikosa,tumia sasli ambayo ipo ya kumwaga.ugali mbona unalika tu na wala siyo aibu kula ugali nawala siyo umasikini,hebu tuvitumie vitu vilivyo tuzunguka kwa faida ya miili yetu na afya zetu.muhimu nikubadilisha kasumba ya kudhani chai ndiyo ni uwezo/utajiri, wali ,nk ni hayo tu kwa kifupi huwa ina nikera sana baadhi ya mitazamo ya watu kuhusu hayo niliyo sema hapo juu,mnisamehe dada zangu kama nime wakwaza,ila hebu tutumie uzoefu kuwa saidia wenzentu.mimi pia situmii sukari. kaka S.

Yasinta Ngonyani said...

Ndio Mangi kwanza karibu sana katika kibaraza hiki cha maisha na mafanikio! nakubaliana nawe kutoa ni moyo.

Kaka S. Ulilonena ni kweli kabisa. Na najua hili ndilo ni sababu kubwa ya wengi kufukiri kuwa akila nyama na wali, chai ya sukari na maandazi au keki ndio ana maisha mazuri. Lakini tatizo kubwa hapa lipo kwenye kuelimishana. Na kama ulivyosema inabidi kwanza tuache kasumba...kwani katika akili yetu inaonekana kunywa uji wa chumvi ni hali ya chini/ngumu sana. Kama nisemavyo kila wakati ni kwamba bado hatujafunguka kila kitu tupo nyuma. Mimi nilitolea tu mfano wa kunywa chai bila sukari wakati wengine wanahitaji sukari, yaani ninayo ila sipendi kuitumia na wao hawana. Sikuwa na maana kuwa niwape sukari hapana...Hapo nilikuwa tu nimewaza kwa sauti kama vile ni mara ngapi unaenda dukani kununua shat/gauni wakati una moja au mawili unaweza kuyatumia na wengine hawana kabisa. katika hii habari kilichonigusa zaidi yale maji kweli wanashindwa hata kuchemsha je hata kuni nazo sijui ni shida?

sam mbogo said...

Yasinta nimekupa vizuri.sukari kwa sisi wasani (mimi) nimeitumia ka ma kitu cha kuanzia story yangu na kuona sukari hiyo ya weza kusukuma mjadala? umesha shitukia ukirudi nyumabani likiza,mfano kwa mara ya kwanza ulipo rudi chai yako ya asubuhi ilikuwaje? je na chakula cha mchana.nakumbuka chai niliokuwa nimeandaliwa we acha tu,chakula cha mchana ndo usiseme.ilinichukua muda taratibu kuelimishana juu ya chai yangu nachakula,kwa dar wali nielewa ila kijijini ambako ndo masikani yangu ili nipa shida kidogo.kijijini kwetu viazi na asali usipime,karanga na maboga vya kumwaga,lakini mwanzoni ukiviomba hivyo ,una kuta mkate mezani,sukari nk. nashukuru sasa hivi kote wamenifehemu hasa wana familia yangu.ila ngoma bado ipo ukitembelea ndugu jamaa na marafiki, utakula hovyo mpaka basi hilo halikwepeki katika mazingira ya kijijini,kuna wakati nilitembelea faimilia 4 na zote walinipkia ugali,kuku ugali nyama na mmoja aliweza kupika wali,hebu pata picha ndugu yangu,nilikuwa hoi. anyway taratibu tutafika. kaka S.

Yasinta Ngonyani said...

Haswaaaa! kaka S. hapo ndipo utakapokuja jiuliza kweli watu hawa wana njaa kweli? na kwa nini hivyo vyakula wasile wenyewe? Maana wakipata mgeni wanawapa chakula kama hicho na pengine wenyewe hawajala hata pengine mwaka mzima....hapo unajua mimi sijaelewa ni kwanini? ni mila,desturi na tamaduni zetu au?

sam mbogo said...

Ni desturi yetu watanzania,tu wakarimu sana. kakaS.

Yasinta Ngonyani said...

Ok! lakini kwa nini kujinyima mwenyewe na kumpa mgeni? Unajua huwa nakula lakini naona aibu hasa nikijua watoto hasa hawajakila kile chakula kwa muda.

Salehe Msanda said...

Habari,

Fikra/wazo la jioni na ujumbe wa salt in my porridge, vinatoa picha ya jinsi gani tunatakiwa kujipenda na kuonyesha upendo kwa wengine ili iwe faraja kwao.
Lakini sasa hivi btunaishi katika ulimwengu wa ubinafsi na umimi,kiasi kwamba tunashindwa kuwapenda wengine kwa maana ya kuwapenda.
Kila la kheri