Thursday, October 20, 2011

KATIKA KUWAZA NIPIKE NINI JIONI HII? GHAFLA NIKAJIKUTA NATAMANI KWELI CHAKULA HIKI...

..ugali na kumbikumbi/mbulika ambacho mara ya mwisho nilikula 2009 nilipokuwa Lundo kando ya ziwa Nyasa . Mwaka huu nilipokuwa nyumbani msimu ulikuwa si mwenyewe. Pia nimetamani kweli ugali na LIKUNGU sijui wangapi mmewahi kula au tu kujua/kuona ? Likungu ni mboga, ni "wadudu/aina ya kama mbu". Huwa wanajitokeza ziwani na watu wanawakamata na kuwakanda kama vile unakanda unga wa mkateau maandazi pamoja na chumvi na pilipili na baadaye wanachoma ili kuhifadhi au unaweza kukanda na chumvi na pilipili na kuchemsha na kulamoja kwa moja. Bahati mbaya sina picha ya LIKUNGU. Ila rangi yake ni nyeusi. Kweli nyumbani kuna vyakula vingi vya asili na vitamu...Sijui sasa nipike nini? maana kupata vyakula hivi hapa itakuwa ngoma ..unga ninao ila...Ushauri jamani?

12 comments:

Rachel Siwa said...

Ugali huo wa likungu ni wa unga gani?kuhusu upike nini na hapo vitu vya Nyumbani ni adimu labda angusha kitu MAKANDE!!!!!!Wiki hii waswahili tumekumbuka Nyumbani mwehhhh,Mimi leo nimekula Ugali na Dagaa wa kigoma sasa sijui tiite hivyo,kwani dagaa wenyewe wametokea upande wa BURUNDI rafiki yangu ameniletea, jee niite wa KIGOMA AU WA BURUNDI?

Yasinta Ngonyani said...

Rachel! Likungu si unga bali ni mboga ni "wadudu/aina ya kama mbu" huwa wanajitokeza ziwani na watu wanawakamata na kuwakanda kama vile unakanda unga wa mkate na baadae wanachoma ili kuhifadhi au unaweza kukanda na chumvi na pilipili na kuchemsha na kula mara hiyohiyo. NI TAMU ndugu yangu...mmhhh wewe sasa mchokozi unazidi kunonogesha vyakula ambavyo sina dagaa ni dagaa tu bwana...

Rachel Siwa said...

Ohhh nimekupata dada yangu na Monganiwa sijui jina kama nimepatia, nao pia si wanapatikana Ziwani? jee unakula na jee unapikaje?hahahha nimekukumbusha dagaa, kuna wanayasa pia nawapenda sana.

Yasinta Ngonyani said...

Nimefurahi kama umenipata...Ndiyo Manganiwa nayafahamu na sijajua kama kuna jina jingine..haya sijawahi kula kwa kweli na ni kweli yanapatikana ziwani. Ubaya huo..LOL ila ngoja nikaangalia akiba yangu nakumbuka nilibeba dagaa mwanza na nyasa:-) nikutumia

Rachel Siwa said...

hahhaaha haya dada Hakiba ni nzuri japo waweza kupata hata harufu!!

emuthree said...

Mmmh, wengine tusio-zoea kula hawo wadudu..duuh, MLO MWEMA WAJAMENI TUPO PAMOJA

Rehema said...

Yasinta umenifurahisha sana kwa kunikumbusha kumbikumbi ambao sikumbuki mara ya mwisho nimekula lini na ukizingatia msimu ninaokwenda likizo nyumbani siyo msimu wake.Likungu nalo nilishawahi kuonja mara moja ila ilikuwa zamani sana,kwa ujumla vyakula vyote ni vitamu sana.Vipi viyenje hujavikumbuka?

ISSACK JIAH said...

HOngera kumbe ndivyo ulivyo kumbikumbi unakula pekee yako huo uchoyo ulianza lini au ulituringishia maana kuwapata msimu huu ni kazi kweli au wale wa kutengenezwa maana wenzetu hawashindwi kitu hata uyoga wanatengeneza ,sina maana ya kuwa umeninyima ila umetutamanisha kweli wamependeza na wanatamanisha kwakweli ila nina wasi wasi mbogo hajawahi kuwala maana hata hajaunga mkono msosi huo
che jiah

Jacob Malihoja said...

Mau yoyooo! Na ne Ngumbi! Lyuva lo lenili ngumbi vihuma kwoki? Ahaa nimanyili .. kuulaya mwivika mu jokofuuu!

Yani we acha tu .. inabidi ziara yangu ya Songea niifanye msimu muafaka kabisaa. Unajua nakumbuka Kudapa Ngumbi .. Siku moja nimekaa kwenye kakichuguu kadogo niko bize nakamata kumbi kumbi .. nimevaa kaptura nyepesi .. likatokea ligenge .. likaningata kwenye tako .. wacha niruke!

Anonymous said...

hiyo uyosema yakukausha huko bukoba linaitwa "ISHAMI" NITAMU KAMA UNAVYOSEMA

Simon Kitururu said...

Kumbikumbi nimekula Ila sijawahiona kumbikumbi wakiliwa kwa ugali!:-

Likungu hiyo kitu ndio nasikia hapa kwa mara ya kwanza.Itabidi nitembelee huko. Likumbi inapanda kwa pombe aka KILAJI cha huko?

Samahani wengine fani yetu ya vinjwaji bado hatujaacha.:-)

Unknown said...

Nmebaki kinywa wazi.