Saturday, October 15, 2011

MAJIBU KWA NDUGU MANGI NA KAKA SIMON KITURURU!!!

Kutokana na maoni ya ndugu zangu Mangi na kaka Simon Kitururu ambayo yanatoka katika picha hizi nimeona niweke hii picha labda itasaidia. Maoni yenye yalisema hivi:Ndugu Mangi anasema "Akina msitudanganye kabisa!Tuonyesheni kitu kipya na kamili kwa kuvaa mavazi ya wanawake katika picha kamili kuanzia juu kwenda chini mkionyesha uwakilishi wa kitanzania." Na kaka Simon naye anasema "Ghafla naamia upande wa mtani wangu MANGI ,...... nahisi kuna kitu hamjatuonyesha. Na neno la MANGI liheshimiwe nanyi. Amen.
JUMAMOSI NJEMA WAPENDWA!!!!!

14 comments:

ray njau said...

Wadau mpo hapo.Yasinta katoka kivingine kabisa tena na miguu ya bata sijui kasahau ndala/viatu.Lakini raha ya lizombe ucheze peku.Hapo,hapo ni lizombe mpaka bombambili kwenye nyumba yenye madirishi na pale nje utakutana na kajogoo keusi kadogo kanawika kokoliki!Hapo umefiki!

Jacob Malihoja said...

Nafurahi kuona mwanamke wa kitanzania katika mavazi ya kiheshima ya Kitanzania. Hebu endelea kuwafundisha wadada wa hapa bongo namna ya kuvaa maana hivi sasa inatisha .. kila wanachoona kwenye runinga wamedaka.. hizo model jeans, legging jeans, vipedo .. hadi inatisha! na jamii inakaa kimya kabisa .. hamna anayefungua mdomo .. hivi sasa nguo za kulalia na zile za kuvaa ndani mnaita skin tight zinavaliwa na kutokea... yani mmmh! jasho linanitoka .. kama ni kutegani kumepitiliza! tunashindwa kutegeka tunaishia kupata kichefu chefu .. hata wakati mwingine inafikakia unamchenga mtu unayemfahamu!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

tabasamu lako bibi...kwa raha zako


halafu pozi hilo kama la Bikira Maria mkingiwa Dhambia ya asili a.k.a Maria Imakulata...lol!

sam mbogo said...

sifa ya vitenge,uwe na bodi,tako,wowo ,nk maranyingi wamama wenye miili ya wasitani hupendeza sana wakivaa vitenge. haya dada wawa watu umetoka vizuri na vitenge. walio toa ombi watakuwa wameridhika. jumamosi njema.kaka s

Simon Kitururu said...

Mambo ndio haya sasa!Ila ngojea nifikirie kidogo,.. isijekuwa ushantia majaribuni kwa dhambi ya kutokwa udenda!:-(

Jumamosi njema Mdada!

Rachel Siwa said...

haahaha haya kaka Njau na kaka Simon nami nimeshajibu.

Simon Kitururu said...

@Rachel :Nimeona na umependeza kweli!

EDNA said...

Umependeza kweli kweli mwanakwetu.

Goodman Manyanya Phiri said...

Wape, Dada! Wape, tu! Wasithubutu kusema tena! Safi saba!

Nampangala said...

Mlongo upendizi sana, nimelipenda sana hili vazi na Mama Afrika linakubali sana dada yangu.

Penina Simon said...

Umependeza mdada, umekumbusha hako kamshono ni ka miaka mingi lkn kama kawaida ya kitenge kila ukivaa mshono hauchushi

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii na kuwapa Shukrani wote.Pamoja daima:-) Rachel nimekuona pia mdada umependeza nawe mwenzangu.

ray njau said...

Asanteni wadau na asante Yasinta kwa kukidhi kiu ya wadau wako.Yale yote mema yaandikwe kwenye mawe ili yasifutike na yale mabaya yaandikwe mchangani ili upepo uyachukue.

Anonymous said...

hivi dhambi ya asili ni ipi?nijuze walimwengu kwauelewa wangu si alisema nendeni mkaijaze dunia? au...... batamwa