Wednesday, October 5, 2011

Sasa tunakaribia Miaka 50 ya uhuru na mfumo huu wa upishi?

Huyu ni kati ya wanake aliyekutwa katika Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma akipika ugali wa mahindi kwa mtindi wa wa kutumia mafiga matatu,kutumia kuni ambazo zinatoa moshi mwingi kwa mama huyu. Katika karne hii ya 21 ambayo inasisitiza maendeleo katika teknolojia Je? huu ni uungwana kweli? au Je una maoni gani katika hali hii? picha kutoka HAPA

9 comments:

John Mwaipopo said...

au ndio kusema jasiri haachi asili

isaackin said...

YAANI DADAA WE ACHA TU,NA ITAFIKA MIA KWA MWENDO HUU HUU

Rachel Siwa said...

Mungu ibariki Tanzania!!!

Abdul husein said...

Kwa mwendo huu hatujaona mafanikio ya miaka 50 ya uhuruuhuru

Goodman Manyanya Phiri said...

Mapishi ni mapishi tu. Mimi sioni tatizo hapa ni nini: tena ugali ule ni mtamu kuliko ninaopika mimi kwa kutumia umeme na kama huyu mama akitaka kutengeneza chipsi, pale ni mambo chapuchapu kabisa!


Labda tungeuliza kihalali kwamba: "Wanaume wako wapi ili wamsaidie huyu mwanamama?"


Lakini kusema eti kwasababu siku nyingi tumepata uhuru kwa hio asiwepo anaepika namna ile ndio kudai haki isiekuwepo hata katika nchi za Ulaya.

emuthree said...

Nimechungulia mara moja, ndugu yangu!

ray njau said...

Mhhh hii mada ni nzito sana hasa ukizingatia kuwa ni tathimini ya miaka 50 ya uhuru.Hapa napata kigugumizi kwa kuwa miaka 50 ya uhuru ni maisha na mafanikio ndani ya changamoto kwa watanzania wote.

Penina Simon said...

Hata tukiendelea sana hadi tuwe sjui kama nini, Lakini yahsinta mtu asikwambie kitu, ugali wa dona na tena ummeusongea kwenye mafiga ni mtamu na una raha yake.

Anonymous said...

kwani hapo cha ajabu nini.. hiyo ni sehemu ya maisha acheni ujinga