Tuesday, October 4, 2011

PICHA YA WIKI...MAZOEZI NI MAHIMU KWA AFYA YAKO!!!

Picha hii imenikuna sana na pia nimejikuta natamani pia kukimba kwani nimekuwa mzembe sana. Ngoja nikurudi kutoka kazini nami nikimbie. Safi sana ..ila sasa usiache endelea hivyo hivyo :-)

16 comments:

Simon Kitururu said...

Halafu MDADA HUYU ni MZURI jamani!

sam mbogo said...

kweli mazoezi ni muhimu,pale upatapo muda.kwani Yasinta unamgogoro na mwili wako,mi naona una mwili mzuri tu,labda kama usemavyo mazoezi kwa afya. kitu kingine naona unanizamu/nidhamu kweli kweli na mavazi hebu kula pensi sikumoja halafu nitakuambia kitu. pia msisahau umri nao ukifika kuna baadhi ya mazoezi yana kuwa taabu,nibora kuanza mapema.kaka s.

Yasinta Ngonyani said...

Simon kitururu! Ni kweli huyu dada ni mzuri:-)

Kaka Sam! Kwanza AHSANTE sana kwa wasifa kuwa nina nidhamu kwa mavazi.....ha ha ha ha haa kwa vile tulionana ndo unasema au uliza kama nina mgogoro na mwili... haya bawana ila mimi napenda sana kukimbia ni kama hoby yangu kama vile kuchuma uyogo. Kuvaa pensi? Kwani huwezi kuniambia bila kuvaa hilo pensi? UMENIUMIZA MBAVU KWELIKWELI:-)

ISSACK CHE JIAH said...

naona leo nami nichangie kama ni mpango wa mazoezi basi tuanze ule mimi naita zamaini wa kupokezana vijiti maana siku hizi sijuwi kama wanafanya huko kwenye shule zetu maana ndo kisa nilikacha hiyo fani ya uwaaalimu wenyewe ,siku zile tulikuwa tunakimbia na mimi zile fupi nilikuwa naziokota lakini sasa duu kwakweli dada umefanya jema kutukumbusha mwambie mbogo asitegemee mabavu ya umbogo afanye mazoezi utuuzima ukimfika haya siku hizi kuna kaugonjwa kanaitwa kupaaaalaaaizi hako kaogope sana
sisi wengine tumebahatika kuwa na kamwili kadogooo ila tusijidanganye fanyeni mazoezi siyo ya kwenye bia tuu na kula
nakupongeza dada Yasinta kwa kuweka ratiba ya mazoezi mshauri na huyo bwana kaka mbogo
Issack che Jiah

sam mbogo said...

Che nani!!? aaaa che Issack,safi kabisa kwa maoni yako,nitayafanyia kazi.kweli kaugonjwa ka kupooza si mchezo,mazoezi ni muhimu.ubabe wa jina mbogo/nyati wala usikutishe afya ni muhimu. Yasinta nina mengi ya kunena ila we acha tu ,naomba utakapokuwa una kimbia vaa pensi mazoezi yata kuwa kabambe!!.niombi tu kama baridi itakuwa kali basi vaa kama Da Mija. haya ngoja nikawajibike.kaka S.

Yasinta Ngonyani said...

Ngoja nisijifanye kujua nilifikiri najua pensi ni nini ila sasa naana kuwa na mashaka. Je? kaka S pensi ni nini(vazi la aina gani)? naamini kuuliza si ujinga

Simon Kitururu said...

Pensi ni aina tu ya Kaptura kiujazo katika kufunika mwili aka kubwa zaidi ya chupi.

Ila kumbuka kwa Kiislamu kinidhamu magoti yakionekana inamaana MDADA tayari utakuwa uko uchi!

Yasinta Ngonyani said...

Oh! Ahsante kwa ufafanuzi kaka Simon...ila sijajua kwa nini nivae hiyo na kukimbia..maana kimsingi inatakiwa kuvaa kama alivyovaa Mija hapo...mmmmhh????

Simon Kitururu said...

Ngojea Sam arudi akueleze faida za bukta. Ila kwangu moja yapo ni kuwa watu watapata fununu una bonge la paja au la!:-(

Yasinta Ngonyani said...

BUKTA, kaaazi kwelikweli haya ngoja aje na tujee kwa nini anataka iwe hivyo:-)

SAm mbogo said...

Haya wajmeni!! nimerudi.kwa dada zetu wa kiswahili/watanzania ukimuona katinga pensi ujuwe kajiamini kupita kiasi,wengi huwa na vijimaswali kama vile kuvaa pensi ni uhuni,wengine huona aibu kutokana na maumbile ya usafiri/mguu,nk. I la mimi nilikuwa na angalia faida za kuvaa pensi,kama moja ya vazi ambalo kwa umbile lako mimi navyo amini Yasinta utatoka mchicha sana.pia ukiwa ndani ya pensi/bukta kuna uhuru fulani unaupata katia mwili,fikiria kipindi chote cha baridi ya ulaya,hukuupa mwili nafasi ya kuwa huru namifuniko mbalimbali,ukipata hali ya hewa kama bongo,tafaadhali Yasinta vaa pensi.kama mija hatimaye nayeye kajiachia kimavazi,na kaonekana mrembo zaidi.ni mawazo yangu tu.kaka S.

Yasinta Ngonyani said...

Haha h ahaaa Kaka Sam umenichekesha kwelikweli...unajua kwa nini? kwa sababu hujawahi kuniona nikimbiapo ni nini navaa?:-)

Rachel Siwa said...

Kaka S na kaka Kitururu mna visa sana nyie kwikwikwi, da'Yasinta kaka zako wamekuomba uvae pensiiiii!!Kweli kanofu aka kamwali nyehh,sijui mazoezi yanamfanya aonekane kamaliza la Saba mwaka jana, Ngoja nami nianze!!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Rachel! nakuambia yaani haswa wana visa hata sio kidogo.. Anza bwana wewe, mimi na yeye Mija halafu kaka Samu na kaka Simon . Yaani hapo tayari timu:-) Safiii eeehhh!!!

Mija Shija Sayi said...

Sio siri wala nini Yasinta kaumbwa akaumbika ila tatizo ndo hilo hana masihara kabisa suala zima la mavazi ya nidhamu...

Asante kaka S kwa kuanzisha hoja na asante kitururu kwa kuitilia mkazo..

Yasinta Ngonyani said...

Mija nilijua utakuwa upande wangu...LOL. Jamani wote mnanivamia...mnataka....basi naacha haya jamani nawaachieni mjadala..LOL