Wednesday, October 12, 2011

ETI MALI NI YA MWENYEWE?

Kipengele cha JUMATANO cha MARUDIO YA MADA, baada ya kuweka hiyo hapo ya kaka Kitururu nikawa natembea tembea tena mitaani nikakutana na hii hapa kaaazi kwelikweli ebu tujadili kwa pamoja hii nayo nimeikuta kijijini kwetu

Inaonekana kuwa mara baada ya kufa mfanyibiashara mkubwa basi aghalabu biashara hiyo huenda sawa.

Hivi majuzi nilipanda moja ya mabasi mabasi ya safari ndefu ambayo wakati wanaanza safari zao ilikuwa na huduma mbalimbali kama za kutoa maji, kuonyesha sinema/video, pipi, biskuti nk.

Huduma kwa wateja pia zilikuwa safi ambapo mlikuwa mwatangaziwa mlipofika na kadhalika. Nilishangazwa na hali ya sasa ya basi hili na nilipouliza nkaambiwa...'huna habari? Mwenye mali keshakufa so watoto ndo wanaoendesha kampuni'

Swali: kwani mwenye kampuni asipokuwepo ndo mambo yaende ndivo sivo?

Je yawezekana yatokeayo Tanzania kwa sasa ni kwa kuwa mwenye mali-Mwl. Nyerere-hayupo? Je kuna siku nasi biashara ya kulinda rasilimali zetu na kuiongoza nji vema ikawa swafi kama biashara nyingine?

4 comments:

ray njau said...

Asante kwa kuweka mada mezani ili majadiliano yaendelee.Kwa ujumla utawala na siasa siyo uga wa kila mtu na hakuna mwenye hakika sana na kinachoweza kuwepo kesho.

sam mbogo said...

Nina hakika kweli sasa hivi Tanzania hakuna mtu ama kiongozi ambaye akisema kauli yake ya weza ogopwa/sikilizwa. raisi wa nchi tunaye lakini ndo hivyo anaangushwa na baadhi ya watendaji wake.nikweli nyerere kwa kiasi fulani alikuwa ana saidia kuwa kumbusha viongozi wetu wajibu wao kwa watu wao na taifa kwa ujumla.,kipindi cha fungulia mbwa nikibaya sana.kaka s

Godwin Habib Meghji said...

Nchi ina wenyewe, Nimemsikia kwa masikio yangu kiongozi mwandamizi wa CCM akisema hii nchi ni ya kina nani.

Inawezekana Zamani enzi ya mwalimu ndio ilikuwa ya watanzania wote. Ndio maana wazee wengi leo wasomi waliweza kusoma kwa kulipiwa mpaka nauli ya kutoka kijijini kwao.

Wewe kama haupo huko hii nchi haikuhusu. kuwa mpole. wewe upo pale kwa hisani tu

ISSACK CHE JIAH said...

Haya tena mimi nilijuwa kuwa mambo yatakuwa ni hivyo kwakweli si kufa tu kwa mwenye mali ata waswahili husema paka akitoka panya hutawala ,hivi ndivyo kwa nchi au tuseme kwa ujumla Afrika ndivyo hivyo nilikuwa natoka kule tunduru nikaona mambo yanayoendelea pale mimi wakati nasoma miaka ya 80 tulikuwa tunasikia kuwa pale kilimasera kuna madini yale ya mlipuko ila leo yameshauzwa na hata faida yake kwa watu wa maeneo yale hakuna watu ni duni maji yashida na hata miundo mbinu ni shida
kwamaana inaonyesha kuwa mwenyewe waliokuwa wanamwogopa baada ya kufa tu ile migodi ndipo imeanza kuchimbwa mbona wakati ule hakuthubutu mtu kuingia japo kukata kuni eneo lile,haya migodi yote huko bulankulu ,kahama ,nega geita n.mara kote huko mambo ni kuchukuwa michanga ya sampuli ati kweli we mchanga utoe tanganyika kwenda ulaya kuupima kisha hata msimamizi hatuna .leo tumeambiwa wanyama wamepelekwa sijuwi wapi we inakuingia kweli wanyama watatokaje mbugani wapande ndege na kama baba yetu angekuwepo je maliasili hizo zingekwenda huko kusikojulikana mimi nasema kufa kwa mwenye mali sisi watoto tunateseka sijuwi kama hawa tunao walea na kujinyima kula kwaajili ya kuwasomesha kweli watikuta hiyo mali aliyotengeneza BABA
MAONI YANGU HAIWEZEKANI MAJI KUPANDA CHITUMBIIIIIIII