Habari za jioni ndugu zanguni ..kama wote mjuavyo rafiki, mwanablog na kaka yetu Shaban Kaluse alipata ajali ya gari jana asubuhi wakati akiwa anaenda kazini. Baada ya kuwasilliana na kwa kutaka kujua anaendelea? Ni kwamba bado ana maumivu kifuani na mbavuni. Amesema kwamba kwa vile mkono huu amekwisha vunja mara moja na hii ni mara ya pili. Kwa hiyo kesho alfajiri atafanyiwa upasuaji kwenye mkono ili kuweka vyuma.
Pia anasema ya kwamba Dereva kakimbia, mwenye gari kamfuata ili wayamalize nje ya Mahakama. Trafik ameshauri kwamba ni vema wayamalize kwa sababu maswala ya bima huchukua hata miaka mitatu na malipo yako ni kidogo sana. Pia wanamuomba atoe ruhusa gari liachiliwe. Ametuomba sisi ndugu/wanablog wenzake ushauri au labda nisema je ?tuna mtazamo gani kwa hili?
11 comments:
Huyu Bwana augue pole, ndilo la muhimu. Na asiwe mvivu kwa masuala ya fizio (PHYSIOTHERAPY) na atapona tu.
Mengine, tumuachie Mungu na mipangilio yake.
Asante kwa uungwana wako, Da'Yasinta, Maisha Na Mafanikio yake!
Pole Kaluse!
Mimi sBIMA za Bongo sizijui sana na siziamini kutokana na stori za waliodakwa nazo. Kwa misingi hiyo naweza sema ``CHUKUA CHAKO MAPEMA´´.
Kona ya uungwana inamtakia Kaka Kaluse arts njema na kupona haraka... Mambo ya bima za bongo sielewi vizuri...
nami naungana na wadau wengine kumtakia kaka Kaluse kupona haraka.
mambo ya magari na bima yana longolongo sana. kwa ushauri wangu ni vema lingefanyika linalowezekana. lakini angalizo langu, asikubali gari liachiwe kabla hajakamilishiwa malipo watakayokuwa wamekubaliana vinginevyo ataingizwa mjini.
zaidi, nazidi kumwombea Mwenyezi Mungu amuafu.
Huyu kamanda augue pole ila kwa upande wa bima siyo longolongo san kinachotakiwa tu ni ufuatiliaji. Mbona wabongo tunapenda kupindisha sheria? nashauri protocol!!
@Goodluck: Tatizo liko hapo kwenye ufuatiliaji. Stori za niwafahamuo katika kufuatilia ndiko kwenye mpaka hongo na mambo kibao kitu ambacho unawezakujikuta umepoteza muda na malipo yenyewe ndio hayo tena ya kugawana na maafisa wa bima na polisi wathibitisho ajali.
Niangalizo tu wakati umuhimu wa protokali upo pia.
Muafaka rasmi wa kisheria ndiyo hitimisho sahihi.
R.Njau
Je gari iliyomgonga ina bima gani?
Kwa jinsi alivyoumia anaweza kupata Bima kiasi kikubwa sana kisheria cha msingi awe mvumilivu tu. Huyo mwenye gari anataka wamalizane nje kwa sababu hataki aharibu rekodi yake ya Bima. Au inawezekana hiyo gari iliyomgonga haina Bima imewekwa stika feki tu. Asikurupuke kutoa maamuzi, ingekuwa ni gari ndio imeharibika ningesema akubali makubaliano nje ya mahakama ya kutengenezewa gari lake kwa masharti kuwa iwapo halitatengenezwa kinachofuata ni kesi kubwa zaidi.
Lakini hili la kuumia alivyoumia awaone wataalamu wa Bima wamwambie kuwa kama ni kulipwa na bima angelipwa kiasi gani. Sasa akishapata kiwango ambacho ni halali yake kisheria ndio atakuwa amepata mahala pa kuanzia majadiliano.
Bi Mkora
Aah jamani nilikuwa na usongo na huyo mwenye kutaka gari lake litoke haraka maana anachelewa mahesabu mpaka nikasahau kumpa pole na kumtakia apone haraka mhusika.
pole kwa ajili bwana Kaluse
ndugu zanguni kwa habari nilizozipata mchana huu ni kwamba kaka Kaluse amepasuliwa jana usiku na anaendelea vema. Bi Mkoro nitafanya utafiti kuhusu ulilouliza na nitakujibu. Ahsanteni wote kwa niaba ya kaka Kaluse.
Pole mkaka, tanzania lolote linawezekana. Kama unadhani kutoka moyoni hauta jiumiza kulalamika, tafadhari malizania nje ya mahakama.
Post a Comment