Friday, June 30, 2017

TUMALIZE WIKI HII NA PICHA HII......IJUMAA NJEMA

Kama hamogopi njoeni ukutane na mawe...:-) duh  kaaaazi kweli kweli maana hayo mawe yenyewe yanaonekana makubwa haswaaa likikupata hilo kichwani ...mmmmhhh.....NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA....KAPULYA WENU!

Thursday, June 29, 2017

NYUMBA ZA KALE ZA WANGONI

Leo nimekumbuka kwetu ungonini na nyumba zetu za asili....nyumba aina hii huitaji kiyoyozi  safi sana....

Wednesday, June 28, 2017

KUMBUKUMBU : - UNAKUMBUKA HADITHI HII MANDAWA NA MANENGE....

Hapo  zamani palikuwa na mtu na mkewe, mtu huyo aliitwa Manenge na mkewe aliitwa Mandawa. Siku hizo chakula kizuri kilikuwa maziwa na nyama.
Lakini vyakula hivi vilipatikana kwa shida shida. Maziwa yaliweza kupatikana tu kama mtu alikuwa na ngòmbe. Na nyama  iliweza kupatikana tu kama mtu alipewa zawadi  na jamaa yake au alinunua. JE  ? UNAIKUMBUKA HADITHI HII?

Tuesday, June 27, 2017

KITENDAWILI........!

Kitendawilii!!!!!!
Ni cheupe kama Barafu,
Na ni cheusi kama giza,
Kuliwa ni haramu na kunywa ni halali kina herufi 5 
na kinaanza na herufi ( M ) kinatumiwa na wanaume mara 3 kwa siku,
Na kinatumiwa na wanawake mara 1 kaitka umri wao,
Je?,Ni kitu gan hicho???
TAFADHALI TAFADHALI NI KITU GANI HICHO?

Monday, June 26, 2017

KUMBUKUMBU:- KARIBU TUNYWE PAMOJA MTANI

Leo nimekumbuka ubenani au niseme MATETEREKA KWETU kwa babu MBOZA...ULAZI. ILA huyu dada duh! kazi kwelikweli...nawatakieni JUMATATU NJEMA WOTE MTAKAOPITA HAPA!

Thursday, June 22, 2017

MLO WA MCHANA WA LEO:- UGALI,TEMBELE NA DAGAA

 Kuna watu tembele wanaona kama mboga duni sana, wanakosa uhondo kwa kweli. Ni hivi:- kwanza chambua vizuri, kisha osha tembele lako, mimi huwa naanika kidogo lakini kuna wengine wanapika moja kwa moja baada ya kuosha yaani bila kuanika. Weka sufuria/chungu motoni, weka mafuta ya kutosha, maana tembele linahitaji mafuta la sivyo utalichukia na ndio sababu wengi hulalamika matembele sio mazuri, kumbe mapishi duni. Tia kitunguu geuza geuza kisha tia nyanya zako na chumvi kidogo. Nyanya zikiiva weka tembele lako. Ligeuze hapo mpaka linywee weka maji kidogo sana kisha funika, sio sasa ndo utoke....utaunguza. Watakiwa uwe hapo hapo unalichungulia kama limeiva. Ukiona bado ongeza maji kidogooo usiweke maji menge, ukiona linanywea zaidi hapo mambo tayari/limeiva.
Mwisho mwidho kamulia kipande cha ndimu au limau geuza dakika mbili -tatu  tayari kwa kula sasa.
UGALI,TEMBELE NIMEONGEZA NA DAGAA
Weka mezani kama hutakipenda hiki chakula, basi nimeshindwa. NATUMAINI UTAJILAMBA VIDOLE:-) MCHANA MWEMA.

Wednesday, June 21, 2017

HISTORIA- TUSIWASAHAU MASHUJAA WETU WA VITA YA MAJIMAJI

Kumbukumbu ya kihistoria maaskari wa vita ya majimaji walivyojitoa  kuikomboa jamii yetu.
Maaskari wa vita ya majimaji

Tuesday, June 20, 2017

UJUMBE KUTOKA KWANGU KAPULYA KUJA KWENU

Sisi binadamu ni wanasheria (mahakimu) wazuri kwa makosa yetu, lakini ni watu wazuri sana kuhusu makosa ya wengine
NAWATAKIENI HII SIKU YA LEO IWE YENYE AMANI NA FURAHA PIA. PANAPO MAJALIWA TUKUTANA PAPA HAPA. KAPULYA

Friday, June 16, 2017

NAPENDA KUWATAKIEN MWISHO WA JUMA HILI UWE MWEMA WENYE AMANI NA FURAHA KWA WOTE...


Binafsi bado nina uchovu kidogo wa shughuli za jana...ila nipo sawa..NAWAPENDA WOTE
NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA ...KAPULYA

Thursday, June 15, 2017

PONGEZI: BINTI CAMILLA LEO ANAMALIZA ELIMU YAKE YA SEKONDARI

Hapa yupo katika  maandalizi....kisherea hapa huvaa gauni nyeupe na kofia nyeupe...
Hapa ilikuwa juzi katika sherehe ya kuhitimu Sekondari ( GRADUATION)  Hapa huanza na sherehe na baadaye ndiyo kupokea cheti cha kuhitimu.

Na hapa alikuwa na msindikizaji wake kaka Philip. 
picha zaidi zitakuja  ambazo zitakuwa na maelezo zaidi na labdda maakuli na shamrashamra...haya baadaye kidogo

Monday, June 12, 2017

JUMATATU YA LEO TUANGALIE BAADHI YA METHALI/MISEMO ILIYOZOELEKA SANA HASA KWENYE KANGA

1. Penzi la mama haliishi

2. Mchimba kisima huingia mwenyewe

3. Zawadi pokea usahau yalotokea

4. Haraka haraka haina baraka

5. Haba na haba hujaza kibaba

6. Si kusudi ni tabia
7. Usilaumu dunia bali imani na nia.

Friday, June 9, 2017

IJUMAA: MITINDO YA NYWELE, UREMBO KWA UJUMLA NA VAZI LA SKETI ALIPENDALO KAPULYA WENU

 Nimependa mtindo huu wa nywele (MABUTU) na jinsi alivyojipamba kwa ujumla yaani ni kiasili haswaaa...SAFI SANA!
Na hii sketi duh! rangi za kitenge ni murwaaa na urefu wa sketi yaaani nikama ugalina samaki wa kuchuma kwenye mkaa!
NAWATAKIENI MWANZO  MWEMA WA MWISHO WA HILI JUMA

Thursday, June 8, 2017

KARIBUNI CHAI NA MBATATA/VIAZI VITAMU...

Nimeona nisiwe mchoyo karibuni tujumuike kwa mlo huu maalumu na mtamu pia mzito. Binafsi napenda zaidi mlo kama huu kuliko CHAI MIKATE (MABOFULA) ambayo ukila tu dakika kadhaa ni bonge la njaa tena. Halafu angalia viazi vilivyopikwa na maganda yake..Mmmmhhh ngoja niache maelezo na wengine waseme:-)  PANAPO MAJALIWA!

Wednesday, June 7, 2017

SERIKALI KUIFUNGA HOSPITALI YA KIBENA NJOMBE KWA HUDUMA MBOVU


Hii iliwekwa 14 feb. 2016
Ya kwamba ...Serikali huenda ikaifunga hospitali ya Kibena iliyopo mkoani NJombe kutokana na kutoa huduma zilizo chini ya kiwango

Saturday, June 3, 2017

LEO NI SIKU YA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KIJANA WETU ERIK..HONGERA

LEO KIJANA WETU ERIK ANATIMIZA MIAKA  MIAKA KUMI NA SABA (17)  AHSATE MUNGU. HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA MWANATU ERIK..