Thursday, June 22, 2017

MLO WA MCHANA WA LEO:- UGALI,TEMBELE NA DAGAA

 Kuna watu tembele wanaona kama mboga duni sana, wanakosa uhondo kwa kweli. Ni hivi:- kwanza chambua vizuri, kisha osha tembele lako, mimi huwa naanika kidogo lakini kuna wengine wanapika moja kwa moja baada ya kuosha yaani bila kuanika. Weka sufuria/chungu motoni, weka mafuta ya kutosha, maana tembele linahitaji mafuta la sivyo utalichukia na ndio sababu wengi hulalamika matembele sio mazuri, kumbe mapishi duni. Tia kitunguu geuza geuza kisha tia nyanya zako na chumvi kidogo. Nyanya zikiiva weka tembele lako. Ligeuze hapo mpaka linywee weka maji kidogo sana kisha funika, sio sasa ndo utoke....utaunguza. Watakiwa uwe hapo hapo unalichungulia kama limeiva. Ukiona bado ongeza maji kidogooo usiweke maji menge, ukiona linanywea zaidi hapo mambo tayari/limeiva.
Mwisho mwidho kamulia kipande cha ndimu au limau geuza dakika mbili -tatu  tayari kwa kula sasa.
UGALI,TEMBELE NIMEONGEZA NA DAGAA
Weka mezani kama hutakipenda hiki chakula, basi nimeshindwa. NATUMAINI UTAJILAMBA VIDOLE:-) MCHANA MWEMA.

2 comments:

Anonymous said...

Nimekitamani chakula, mate yananitoka.
Matembele yanaitwaje kwa kiingereza?

Yasinta Ngonyani said...

karibu sana usiye na jina...jaribu k-google kwani hata mimi sijui