Tuesday, September 11, 2012

TUSISAHAU VITENDAWILI VYETU/TUWAFUNZE NA WATOTO WETU!!!KITENDAWILI ...TEGA!!

Unganeni nami ili tupata majibu ya VITANDAWILI HIVI HAPA CHINI. KARIBUNI SANA!!
1. Nyumbani mwangu mna shetani ambaye daima anakunywa maji yangu...
2. Mama nieleke.
3. Nenda huko na nikirudi nimshike ngómbe wa mama mkia.
4. kipo lakini hukioni.
5. Nilikuwa nikitembea njiani niliposimama nikasikia mtu akiniita "wifi! wifi!, lakini nilipogeuka sikumwona mtu.
6. Bibi mweupe ametupwa mibani.
7.Mzazi ana miguu bali mzaliwa hana.
8. Wanabgu wote wamevaa vizibao, wasiovaa si wanangu.
9. Ni nini  hutupwa juu ya meza wakati watu wapo ndani?
10. Huku ngó na kule ngó.
JUMANNE NJEMA KWA WOTE!!!

14 comments:

Emmanuel Mhagama said...

Duh!! Vitendawili vigumuuuu!!

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Emanuel jaribu tena mlongo kimoja utakuwa unaweza tu nina imani haswaaa...

ray njau said...

Kitendawili tega ukishindwa nipe mji nata kwenda Ruhuwiko!

ray njau said...

@Yasinta;
Umeamu kuturudisha kule shule ya msingi kwa vitendawili vigumu.
Nikikumba kule shule ya msingi darasani mkiona kitendawili cha mwenzenu ni kigumu mnampa mji ili awape jibu.
-------------------------------------
Kitendawili chako tega; nimeshindwa nakupa mji; nenda Ruhuwiko!
-----------------------------------

ray njau said...

"Hakika umeamua kuturudisha kwenye zama zetu za elimu ya msingi."
Asante sana Yasinta.

Yasinta Ngonyani said...

Ndiyo kaka Ray,,Leo nimekumbuka na nimetamani sana kuwa mwanafunzi wa shule ya msingi. Na naona tusubiri kidogo labda kutakuwa na anayeweza angalao kitendawili kimoja tu...:-)

ray njau said...

Wifi wifi ni mbaazi hizo.Na vingine naendelea kuwaza zaidi.

Anonymous said...

mbona vitendawili rahisi sana, tupatie vingine vigumu ili tukupe mji.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray hiyo umepatia...ila usiendelee kusiazea sana..

Usiye na jina! kama ni rahisi sana mbona hujatoa majibu yake?

Yasinta Ngonyani said...

ndugu zangu wapendwa naona vitendawili vilikuwa vigumu mno maana jibu limekuwa ni moja tu..kwa hiyo naona nitegue vitendawili hivi:-
1. Mafuta ya taa.
2. Kitanda.
3. Kata ya maji
4. Kisogo
5. Mbaazi kavu.
6. Machicha ya nazi
7. Kuku na yai
8. Kunguru wenye mabawa meupe.
9. Kitambaa
10. Giza.
haya ndiyo majibu ya vitandawili vyetu. Ahsanteni kwa kuwa nami..

ray njau said...

Asante sana mwalimu kwa somo la leo.

gadiel mgonja said...

duuh! dadaa umenikumbusha mmmbaaaali sana ile miaka nipo mdogo zaidi ya wadogo daah!.gdday.

Anonymous said...

hapana chakwanza sio mafuta ya taa ila ni koroboi ndio inakunywa mafuta kwahiyo KOROBOI NDIO SHETANI ANAKUNYWA MAFUTA

Anonymous said...

hapana chakwanza sio mafuta ya taa ila ni koroboi ndio inakunywa mafuta kwahiyo KOROBOI NDIO SHETANI ANAKUNYWA MAFUTA