Sunday, September 16, 2012

Ngoja leo tusali Sala ya Wazazi wakiwaombea Watoto wao

Tunawaangalia , Ee BwanaHawa uliotujalia.Katika hawa tunajiona sisi wenyewe. Je, kweli tulikuwa hivi sisi
Tulipokuwa watoto? Tulipigana hivi? Tulipaiga kelele hivi? Tulileta furaha namna hii. Na mateso namna hii kwa wazazi wtu? Tunashangaa na kujiuliza....Tunajaribu kukumbuka-----Kukumbuka jinsi ilivyokuwa
Tulipokuwa watoto wadogo bado. Tukiwatazama watu wakubwa.

Wakati mwingine wanatutia wasiwasi, Bwana. Au kwa namna nzuri zaidi, tunajitia wasiwasi sisi wenyewe
Kwani si rahisi kuwa sawa daima. Lakini kuna furaha pia, furaha kubwa wanayotuletea. Nao hutufanya tuone fahari,kwani ni watoto wema.

Tunakushukuru kwa ajili yao Bwana, wao ndiyo zawadi yako bora kwetu,baada yetu sisi wenyewe. Utusaidie tuunganisha mikono yetu na mkono yako Ili, Ee Baba,Wawe kweli Watoto wetu.
Amina.
JUMPILI NJEMA KWA WOTE

2 comments:

Rachel Siwa said...

Ameeen! asante da'Yasinta j'2 njema kwenu pia.

Interestedtips said...

Amen dada, nawe pia J2 njema