Wednesday, September 19, 2012

SHUKRANI ZANGU...Chacha wambura Ng´wanambiti
Katika maisha, watu wengi hufikiri watu wa karibu yaani ni familia tu. Leo nimehakikisha kitu ambacho sitaweza kusahau maishani mwangu. Watu/mtu anachukua muda wake na kufanya kitu ambacho wengi hawangefanya. Huyu kaka sijawahi kuonana naye lakini kama alivyosema hapa kwake hakika ni wachache sana wanafanya hivi. Mwenyezi Mungu na akubariki na akuzidishie upendo. Ahsante sana.

6 comments:

John Mwaipopo said...

nimetembelea kwenye blogu ya chacha. nami nimegundua kitu. yatosha kusema undugu ni kufaana na sio kufanana.

ray njau said...

@Wadau;
Hapa Chacha kathibitisha kuwa daima undugu ni kufaana wala siyo kufanana.Acha wenye masikio wasikie na wenye macho waone aliyoyatenda Chacha kwa moyo wa kupenda bila urafiki wa kinafiki.

Rachel siwa Isaac said...

kaka Chacha MUNGU azidi kukubariki,yaani NDUGU MWEMA UTAMUONA WAKATI WA SHIDA!!!!!Ahsante kwakutuwakilisha.

ray njau said...

‘Upendo huvumilia mambo yote. Upendo haushindwi kamwe. ’—1 KOR. 13:7, 8.
=================================================================
Mambo mengi yameandikwa na kuchapishwa kuhusu upendo. Sifa hiyo imetukuzwa na kutungiwa nyimbo za mahaba. Upendo ni uhitaji wa msingi wa wanadamu. Lakini mara nyingi vitabu na sinema zimeonyesha hadithi za uwongo kuhusu upendo, na kuna habari nyingi kama hizo zinazouzwa kwa wingi. Hata hivyo, inasikitisha kwamba watu wengi hawampendi kikweli Mungu na jirani yao. Tunaona mambo ambayo Biblia ilitabiri kwamba yangetukia katika siku hizi za mwisho. Watu ‘wanajipenda wenyewe, wanapenda pesa, wanapenda raha badala ya kumpenda Mungu.’—2 Tim. 3:1-5.
==============================================================
Nafsi yenye ukarimu hiyo yenyewe itanoneshwa,naye anayenywesha wengine kwa ukarimu yeye mwenyewe pia atanyweshwa kwa ukarimu,_Methali 11:25

gadiel mgonja said...

habari my DADA! samahani naomba kuuliza swali kidogo kwamba Kwani kufanya kama alivyofanya CHACHA kunafaida gani?je hyo faida ni kwa huyo ambae ashakufa ua ni aliye hai.

Mija Shija Sayi said...

@ Gadiel Mgonja

Kitendo alichokifanya Chacha kinaonyesha Upendo. Faida za upendo nadhani unazifahamu..

Hilo swali la mwisho, labda ungetuambia wewe unafirikiriaje kabla hatujaanzisha mjadala..