Wednesday, September 12, 2012

MKOA WA RUVUMA KUPATA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AUGUSTIN, MJINI SONGEA.!!!

Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustin ni mradi wa Kanisa Katoliki Tanzania. Binafsi nashukuru sana kwa uwepo wa chuo hiki kwa hiyo wana-Ruvuma sasa tuchukue/tuitumie nafasi hii muhimu ya ELIMU ipasavyo. Picha  kutoka hapa. Sitakosa nami kutembelea hapa punde nifikapo Songea.
Ngoja tumalizie na maelezo mafupi hapa....
KILA LA KHERI KWA WOTE.....

6 comments:

ray njau said...

Hapa sasa Songea itaongea na kusogea na kila mwenye kiu ya elimu sasa asogezee huko Songea!!

ray njau said...

@Yasii,Hakika sasa Ruvumaaaaaaaaaaaaaaaaa inavumaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,acha wenye masikio wasikie,wenye macho waone na wenye miguu wafike Ruvuma.

Yasinta Ngonyani said...

Songea songea ahhe songea ee ninayo furaha kuwa mzaa wa Songea SSS Songea Wilaya yangu . Songea ndipo nilipotoka siku zote nitawakumbuka najivunia nakumbuka mama alisema mkataa kwako ni mtumwa.Tena Songea ya sasa sio kama ya zamani Songea ya sasa ina songa mbele na sasa itavumaa kwelikweli...Na wote mnakaribishwa Songea ...

ray njau said...

Hakika siisahau Songea katika maisha japo sijafika huko lakini hakika siku moja nitafika.Nilipokuwa shule ya msingi msingi Mrieny kata ya Mamba,Wilaya ya Moshi tulichaguliwa kuiwakilisha shule yetu kwenye mashindano ya maswali na majibu ya moja kwa moja.Kabla ya shule yetu kuingia ulingoni nilijibu maswali mengi lakini nilipofika ulingoni na kuulizwa chifu wa Songea nilichemka.Kuanzia hapo hadi leo siisahau Songea na nitaisogelea Songea na nitavuma na Ruvuma.

Anonymous said...

Tunawapongeza wana songea kwani mmepiga hatua moja mbele ya maendeleo.

ray njau said...

Acha tusogee Songea;tukavume na Ruvuma!