Tuesday, September 18, 2012

UJUMBE WANGU WA LEO:- WASICHANA NA WANAWAKE WANA HAKI!!

Watu wote ni sawa, watu wote wana thamani sawa. Hii ina maana kuwa wanawake na wanaume, wasichana na wavulana, wana haki sawa. Lakini katika jamii zetu wanawake na wasichana wananyimwa haki zao.
Hatua ya kwanza kuleta usawa ni kuielewa na kutokuukubali unyanyasaji wa wanawake na wasichana
JUMANNE NJEMA NDUGU ZANGUNI!!!

5 comments:

emu-three said...

Ni kweli ujumbe umefika,

Rachel siwa Isaac said...

Asante kwa Ujumbe Kadala!!!!

Anonymous said...

Ujumbe ni mzuri lakini wanawake na wasichana hawataki kujithamini.Wanajitembeza nusu uchi na kujiuza!!

Anonymous said...

Baadhi wa wanawake hawataki kusoma kwa bidii wakitegemea kusomewa na wanaume na kuwa tegemezi kwao.Kwa hiyo wanawake himizaneni ninyi wenyewe kusoma kwa bidii(Hisabati,Fizikia...)na kuthaminiana na kujithamini na si tu kuchangamkia Miss Kinondoni,Miss Miss,Miss.Wanawake pendaneni ninyi kwa ninyi

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana wote kwa kuupokea ujumbe huu na kusema yunu yaliyokuwa moyoni. Na pia ahsanteni mliopita na bila kusema kitu. Nachukua nafasi hii na kusema machache t. Ni kwamba mwanamke ni nguzo ya familia lakini tangu mwanzo mwanamke amewekwa kuwa mtu wa chini sana na wa kunyanyaswa..Na kuna baadhi nchi ni mwiko kabisa kusomesha mtoto wa kike kisa eti tukimsomesha hawezi kumaliza atapata mimba tu. Lakini tukumbuke ya kwamba ni hawa hawa kaka,baba zetu ndio wanaowadanganya watoto wa kike wanajua yupo shule lakini wanamdanganya.
Halafu katika ndoa mwanamke ananyanyaswa kupigwa kila siku na minyanyaso mingine ambayo astahili kupata. Wote wanasahau ya kwamba wanawake pia ni binadamu na wanaweza.....