Nimeipenda picha hii imenikumbusha Mgazini, huu udongo jinsi ulivyo mwekundu hapo kuvaa nguo nyeupe inabidi uwe msafi sana. Wanafunzi walikuwa/wanapata shida sana maana ukivaa shati jeupe siku moja tu ni lazima kufua. Halafu nimeipenda hii picha jinsi mama huyo anavyosafiri huku mbwa wake katangulia kama mlinzi. Mlinzi wa asili.
5 comments:
yaani hii picha imenikumbusha kijijini kwetu na bibi akiwa kwenye msafara tukitoke shamba, duh
Huyo kweli ni mlinzi wa asili, na mlinzi wa ndani ni Paka. Wenzetu wazungu paka ni rafiki mkubwa, lkn huku kwetu paka kageuka kuitwa `mwanga'...hebu ni kweli paka anaweza kuwa mchawi?
sijui mabodigadi wa viongozi wangekuwa wanakaa mbele ingekuwaje teh teh teh!
Kumbukumbu nzuri sana hiyo
mlinzi wa asili na mlinzi muaminifu na mwenye upendo,paka sio mchawi ila wachawi wanamtumia yaani wanajigeuza paka
NDIYO..ha ha haaa kaka Chacha umenichekesha kweli hapa nililiwaza hili kwa vile naona kwa hapooooo nyuma kuna mtu anakuja ..Kaaazi kwelikweli
Na wengine wote ahsanteni ..ila hilo la paka ndo kwanza nalisikia leo labda tulifanyia uchunguzi..LOL
Post a Comment