Tuesday, September 4, 2012

UJUMBE WANGU:-KUTHUBUTU KUONYESHA MAPENZI/UPENDO NDIYO NGUZO YA MAHUSIANO BORA!!

Kuthubutu kuonyesha upendo wako sio tu maneno mazuri, na sio tu upendo wa matendo au maua na chokleti. Ni kuonyeshana heshima, uaminifu na imani. Pia kuonyesha wepesi wa kuona huruma wakati mwenzako anapokuwa na msongo/matatizo. Kuwa msaidizi mwema na mwenye kusema ukweli.
Kuthubutu kuonyuesha masikitiko yako. Sio kila wakati kujifanya mwenye nguvu(mvumilivu).
Tukumbuke kukaa pamoja  na kupeana mawazo ya maisha..ikibidi kuwa watoto ndani yetu.
Tuwe sisi kwa dadika chache. Dakika chache za furaha., dakika chache za huzuni.Tufanye siku iwe ya sherehe.Tushirikiane katika raha na taabu maishani. Tujipe uaminifu. Tukaribiane na ili kuwa pamoja.

4 comments:

sam mbogo said...

Asante kwa ujumbe. upendo katika mahusiano ni muhimu.ila kwa mtazamo wangu katika mahusiano upendo ni swala binafsi sana kiasi kwamba usipo jitambuwa wewe binafsi unaweza potoka. kaka s

ray njau said...

15Unywe maji ya birika lako mwenyewe, na maji yanayotiririka kutoka katikati ya kisima chako mwenyewe.16Je, chemchemi zako mwenyewe zitawanyike nje, na vijito vyako vya maji katika viwanja vya watu wote?17Na yawe yako peke yako, wala si ya wageni pamoja nawe.18Chemchemi yako ya maji na ibarikiwe, na ushangilie pamoja na mke wa ujana wako,19paa mwenye kupendeka na mbuzi wa milimani mwenye kuvutia. Na maziwa yake yakuleweshe nyakati zote. Upendo wake na ukufurahishe sikuzote.20Basi mwanangu, kwa nini umfurahie mwanamke mgeni au kukumbatia kifua cha mwanamke wa kigeni?_Methali 5:15-20

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! Ni kweli Upendo ni kitu cha ajabu. na wengi tu hupotoka kwa hilo.

Kaka wangu Ray..Ahsante sana kwa neno!!

gadiel mgonja said...

THNX DADAA,NIMEUPENDA UJUMBE WA LEO BE BLCD.