Thursday, September 6, 2012

WANADAMU NA TABIA ZETU/CHUKI ZETU....KUSENGENYANA/KUSEMANA HADI MAOFISINI...

Jana nilikuwa naangalia kipindi fulani na hapo ndipo nilipokumbuka. Ya kwamba watu wengi wanasema akina mama/wanawake ni watu ambao wanapenda sana kusemana/kusengenyana. Hapana si wanawake tu nimeona mwenyewe kwa macho yangu na kusikia kwa masikio yangu. Yaani mtu anakuwa rafiki yako na unaongea naye, na unacheke naye na unamwamini kabisa lakini kumbe sio unavyofikiri wewe. Na watu wengi wamekuwa wakigombana/gombanishwa kwa kitu ambacho si cha kweli na mwisho kuishia kuwa madui wakubwa. Kwa nini kusema ya wenzio na yako nani atasema.? Na kwa nini kama tuna nguvu  basi tuchukue jembe na kwenda kulima kuliko kutumia muda na kusema wengine? Na kwa nini mpaka kumsema mwingine? Ni afadhali kuchukua jukumu na kumwambia/kumuuliza tu. Kuliko kusengenya sengenya ...
Ngoja mr. Nice amalizie  kwa TABIA GANI .....

UNAPOMSEMA MWENZAKO JIFIKIRIE MWENYEWE KUWA JE? KAMA NINGESEMWA MIMI NINGEJISIKIAJE?

2 comments:

ray njau said...

Huo ndiyo udhaifu wa kiumbe mwenye jina la binadamu.Hapa wa kumuonyesha mwingine kidole hayupo.Kama yupo anyoonyeshe mkono na asimame kwa ajili ya utetezi au awasilishe hoja binafsi.

Yasinta Ngonyani said...

kaka T´Ray! Ndiyo viumbe/binadamu tuna udhaifu mwingi. kama wasemavyo hakuna aliyekamilika. Lakini kwa nini kupoteza muda na kuumiza akili kwa jambo lisilokuudhi? je ni chuki au?