Picha hii ilikuwa mwaka "1955 mama huyu amebeba bonge la kikapu, na inasemekana ndani ya kikapu kuna ndizi na kama kawaida mgongoni kabeba mwanae. Hapa ni kando ya ziwa nyasa"
Na hapa ni sasa napo ni vivyo hivyo akina mama /dada wakitoka shamba wengine wamebeba vikapu na kitu ndani na wengine kuni na pia baadhi wamebeba watoto mgongoni ..Je hapa si kweli kwamba akina mama ni ngozo ya familia/jamii?
7 comments:
Kilimo ndiyo uti wa mgongo katika jamii yetu na akina mama wapo mstari wa mbele katika dhana hiyo.Akina mama hongereni sana na wanawake hakika wanaweza!
Hakika kweli wanawake watanzania wanafanya kazi sana,mungu awasimamie mama zangu,dada zangu,mnahitaji kupokewa katika shughuli zenu hasa za shamba nk. jana nilikuwa naangalia katiak u tub,jinsi marehemu Thomas Sankara rais wa Bukinafaso, alivyo anzisha siku ya mapumziko kwa wanawake nchini kwake.umuhimu unakuja pale wanaume walivyo chukua mjukumu ya zilekazi zote wazifanyazo wanawake sokoni,yaani kuza bidhaa,wanawake sikuhiyo ni kukaa nyumbani baba ndo anafanya miangaiko yote aliyotakiwa kufanya mwanamke.niliipenda sana hiyo staili inawapa wanaume kujua upande wapili wa shilingi.kaka s.
Kweli mama ni muhimili wa familia na taifa. Picha hizi zinanikumbusha mbali hasa wakati ule tukilima kwenye mashamba ya shule. Nilisifika kwa kutega.
Nikweli kabisa,Asante da'Kadala na woote. kaka Mhango umenichekesha!!!!!
Nanchukua nafdasi hii na kuwashukuruni wote mliopita hapa na kusema lililo moyoni mwenu na pia wale waliopita tu pia azanteni..Hata mie mwal. hapo nimecheka kweli kumbe tulikuwepo wengi wategaji..wanaweke tunaweza haswaa..
Zamani kulima shuleni ilikuwa ni kitu cha kawaida sana hasa kwa shule za vijijini. Siyo tu mashamba ya shule, bali hata mashamba ya walimu na ya wanakijiji waliokuwa na uwezo wa kulipia huduma hiyo ili kutunisha mfuko wa Elimu ya Kujitegemea. Ninachokumbuka kwa habari hii kwamba kuna watu waliokuwa na yale yanayoitwa MAGONJWA YA KUDUMU kama moyo, pumu (athma) na mengine yanayofanana na hayo. Ikifika siku ya shamba kila mtu ni mgonjwa. Enzi hizo nilikuwa nasumbuliwa na athma, basi shamba pakawa ni kama police post. Ila Namshukuru Mungu kwa nimepona. Cha kushangaza siku ambayo kazi ni kuvuna karanga, mwee!!! Hata wagonjwa wa kudumu wanakuwa na nafuu. Ajabu na kweli.
wananikumbusha mbali sana,
Post a Comment