Tuesday, September 4, 2012

Tafakuri Ya Usiku; Je, Uwezo Wetu Wa Kufikiri Umepungua?


Ndugu zangu,

Yanayotokea nchini mwetu yanatutaka sio tu tufikiri, bali, tufikiri kwa bidii. Lakini swali ni hili; Je, uwezo wetu wa kufikiri umepungua?
Yumkini si kwa aliyekuwa na
ujasiri wa kuipiga picha hiyo hapo juu. Alifikiri sana pia. Na si kwa aliyekaa chumba cha habari na kuumiza kichwa, kisha akaamua picha hiyo ipambe sura ya mbele ya gazeti la Mwananchi la juzi. Hapa Iringa gazeti hilo liligombaniwa kama njugu, na bila shaka sehemu nyingine za nchi.
Naam, siku hizi utasikia ikisemwa; " Tumefika pabaya!" Mwingine atasema; " Tunakokwenda ni kubaya!". Lakini, ni Watanzania wangapi wenye kuuliza maswali haya; " Tumefikaje hapa?" Na " Je, tunaendaje?" Maswali hayo yanamtaka mwanadamu afikiri kwa bidii.
Wakati mwingine nafikiri, kuwa Watanzania tumechoka kufikiri. Hata kwenye maswali magumu yenye kutuhusu tunataka wengine wafikiri kwa niaba yetu. Unaweza kukutana na Mtanzania mwenzako ukamwuliza; " E bwana ee, unafikiri nini juu ya jambo hili?". Jibu lake; " Kwani wewe unaonaje?"- Ni moja ya maswali yenye kuashiria anaykujibu swali lako amechoka kufikiri.
Na wakati mwingine tatizo si kutofautiana kifikra, bali kutofautiana namna au jinsi ya kufikiri. Swali moja, lakini unaweza kuona namna tunavyotofautiana katika kuchagua njia ya kulisogelea ( approach) swali husika.
Na kuna wenye kukimbilia kutafuta njia za mkato. Ndio, majawabu ya mkato. Na baadaye itakuwaje? Inshallah na BwanaYesu Asifiwe!
Maggid Mjengwa,

Iringa
0788 111 765

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Naweza nikasema nakubaliana na mwenyekiti hapo juu hicho alichoandika. Ni kweli Watanzania bado hatujafunguka.. nimependa sentensi hii nanukuu "Unaweza kukutana na Mtanzania mwenzako ukamwuliza; " E bwana ee, unafikiri nini juu ya jambo hili?". Jibu lake; " Kwani wewe unaonaje?"- Ni moja ya maswali yenye kuashiria anaykujibu swali lako amechoka kufikiri." mwisho wa kunukuu..Hivi kwa nini tupo hivi?..

Ester Ulaya said...

uwezo wa kufikiri umepungua......roho ya ubinadamu inapepea......kuuana inakuwa ni kitu cha kawaida kabisa.....kwanini lakini?????/

imeniuma sana hii issue

NN Mhango said...

Uwezo wetu wa kufikiri kama watanzania umekufa. Heri ungepungua huenda kuna siku ungeongezeka. Yaani tunauawa kama swala na watu tunaoishi nao kila siku halafu tunashindwa hata kuwalipizia kisasi! Angalia Kenya wanavyowalipizia kisasi kiasi kwamba ngoma ni droo. Ingawa si vizuri kuhimiza watu kufanya maasi, kama serikali tena inayokula na kuishi kwa kodi zao inayafanya wao wanachelea nini? Jogoo aliwafundisha vifaranga kunya ndani ashakum si matusi. Jino kwa jino na jicho kwa jicho ndipo kitaeleweka.