Thursday, September 13, 2012

UJUMBE WA LEO:- HUU NDIYO UPENDO!!!

Ufafanuzi mmoja kuhusu upendo ni, ‘uhusiano mchangamfu na wakibinafsi au shauku yenye kina, kupendezwa sana na mtu mwingine.’
Ni sifa ambayo huchochea watu wafanye mambo yanayowanufaisha wengine, nyakati nyingine wakifanya hivyo kwa kujidhabihu sana. Kulingana naufafanuzi wa Biblia, upendo wahusisha akili na moyo.
Akili, au uwezo wa kufikiri, hutimiza fungu fulani kwasababu mtu anayependa hufanya hivyo akitambua kwamba yeye pamoja na wanadamu wengine anaowapenda, wana udhaifu na vilevile sifa zenye kuvutia.

Uwezo wa kufikiri wahusika hata zaidi kwa kuwa kuna wale ambao Mkristo huwapenda—nyakati nyingine, hata ingawa nyutu zao hazimpendezi—kwa kuwa kutokana na kuisoma Biblia anajua kwamba Mungu anataka afanye hivyo.
Hata hivyo, kwa asili upendo hutoka moyoni. Upendo halisi kama uonyeshwavyo katika Biblia hautegemei tu uwezo wa kufikiri. Wahusisha unyofu mwingi na kujitoa kabisa kihisia-moyo.

Ni nadra sana kwa watu ambao ni wenye ubinafsi kudumisha uhusiano wenye upendo wa kweli kwasababu mtu anayependa huwa tayari kutanguliza masilahi ya mwingine.
Maneno ya Yesu “kuna furaha zaidi katika kutoa kuliko kulivyo katika kupokea” ni ya kweli hasa wakati wa kutoa kunapokuwa tendo la upendo.Upendo ni kifungo chenye nguvu. Mara nyingi upendo hutia ndani urafiki, lakini vifungo vya upendo ni vyenye nguvu zaidi ya vifungo vya urafiki.

Uhusiano wa kimahaba kati ya mume na mke wake nyakati nyingine husemwa kuwa upendo; hata hivyo, upendo ambao Biblia hututia moyo tusitawishe hudumu kuliko uvutio wa kimwili.
Mume na mke wanapopendana kwelikweli, huendelea kuwa pamoja hata isipowezekana tena kuwa na uhusiano wa kimwili kwa sababu ya udhaifu unaosababishwa na uzee au kwa sababu mmoja wao hajiwezi.
UPENDO DAIMA!!!

4 comments:

ray njau said...

Asante sana kwa mada ya leo mama wa kibaraza cha maisha na mafanikio.Hakika upendo ni nguzo ya dhahabu katika mchakato wa maisha na mafanikio.
Mwandishi wa mada hii anataka tujadili eneo moja la upendo au maeneo yote manne kulingana na orodha iliyopo chini?

==================================
1.GODLY LOVE [AGAPE]

2.FRIENDSHIP LOVE [PHILEO]

3.ROMATIC/SEXUAL LOVE [EROS]

4.FAMILY LOVE [STORGE]
================================

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! Ahsante kwa mchango wako..Na kwa kweli tunaweza kusema :
Upendo huvumilia, hufadhili.
Upendo hauhusudu,
Upendo hautabakari,haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya, haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli. Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote hustahimili yote....Kuna mifano mingi ya upendo wa kweli katika maisha ya kila siku. Kuna upendo wa baba unaojihakikisha kwa kumpeleka mtroto wake mgonjwa hospitalini. baba anapaswa kutembea porini maili kumi na tao bado baada ya safari ndefu, lakini baba anasukumwa na upendo, anapata nguvu na ananuia kufika hospitalini. Wala hawezi kusema, "Inatosha sifanyi zaidi ya hapa." Upendo una hatua nyingi sana...

Rachel Siwa said...

OOHHHHHH dadake Asante sana Upendo neno dogo lenye mambo na maana nyingiii nani siraha kuu MAISHANI!!!!!!!!!

ray njau said...

@Yasinta;
Jambo kuu hapa ni kila mhusika kutambua aina ya tafsiri sahihi ya neno UPENDO na ni aina gani ya upendo unaofaa kulingana na wakati na tukio.