Saturday, September 1, 2012

MWEZI MPYA:- TUANZE HIVI TUSISAHAU KULA MATUNDA NI MUHIMU KWA MIILI YETU!!

Matunda, tusisahau kula matanda jamani....kwa kawaida inatakiwa tule angalao kila siku matunda kama matano hivi. Lakini kwa bahati mbaya si wengi tuna nafsi ya kula hata tunda moja kwa siku. Na pengine wale wanye nafasi hawali. Jambo hili la kutokula matunda huhatarisha miili yetu kuto jengeka yaani vile virutubisho vya kuujenga mwili na kuuimarisha. kikinga. Na ndio hapo tunapojikuta miili yetu haina kinga za kutosha.
Wote tunajua mwili uwapo dhaifu ni rahisi sana kushambuliwa/kupatwa na maradhi hatari. Kama vile saratani, pia mboga majani nazo husaidia tuzile kwa wingi nazo pia. Kuna wakati unaweza kushangaa, kuona mtu anamaliza mwezi mzima hajala hata tunda moja. Tuchukue ule msimu wa machungwa, unaingia mpaka unaisha hajala hata chungwa moja. Ukija msimu wa maembe nao ni hivyo hivyo. Halafu utakuta maembe yanadondoka tu chini na kuoza na pia wengine wanayaokota na kulisha nguruwe. Au wanyama wengine lakini yeye mwenyewe anajisahau.

Wengi huona ya kwamba matunda siyo sehemu ya vyakula muhimu. Tuache tabia hii tule matunda na tuepukane na maradhi. Ukitaka kulifaidi tunda, basi kula pale ambapo tumbo lipo tupo/kabla hujala kitu chochote tanguliza matunda kwanza na baada ya nusu saa au saa moja, ndiyo unashauriwa ule mlo wako kamili.
NAWATAKIENI JUMAMOSI HII YA KWANZA YA MWEZI HUU WA TISA IWE NJEMA SANA!!!

3 comments:

Anonymous said...

Yasinta, asante kutupa elimu ya umuhimu wa kula matunda. Watu wakubwa wengi hawatilii maanani ulaji wa matunda kabisa hasa nyumbani TZ. Sijui ni kutojua umuhimu wake? Au ni uzembe tu mtu akijishibia ugali wake au ubwabwa haoni sababu tena ya tunda? au wanaamini kwenye heavy diet na matunda yanaonekana kama kitu kidogo sana ila umuhimu wake ni mkubwa sana hata kuliko ugali/ wali nk.Au ni kuwa yana bei kubwa hasa sehemu za mijini kama Dar na kwingineko. Kosa vitamin mwilini hayo magonjwa sasa? Tunapougua mafua unaambiwa kale matunda kwa wingi tena na juice za matunda pia, nk.Nadhani tunahitaji elimu ya ktosha kuhusu umuhimu wa kula matunda hasa kwa sisi wa TZ.

ray njau said...1Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia.

2Dunia ilikuwa bila umbo, na ukiwa, na giza lilikuwa juu ya uso wa kilindi cha maji; na nguvu za utendaji za Mungu zilikuwa zikienda huku na huku juu ya uso wa maji.

3Mungu akasema: “Kuwe na nuru.” Kukawa na nuru.4Kisha Mungu akaona ya kuwa nuru ilikuwa nzuri. Mungu akatenganisha nuru na giza.5Mungu akaanza kuiita nuru Mchana, lakini giza akaliita Usiku. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.

6Mungu akaendelea kusema: “Kuwe na anga kati ya hayo maji na mtengano uwepo kati ya maji na maji.”7Ndipo Mungu akalifanya anga na kutenganisha maji yaliyo chini ya anga na maji yaliyo juu ya anga. Ikawa hivyo.8Mungu akaanza kuliita anga, Mbingu. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili.

9Mungu akaendelea kusema: “Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, nayo nchi kavu ionekane.” Ikawa hivyo.10Na Mungu akaanza kuiita hiyo nchi kavu Dunia, lakini mkusanyiko wa maji akauita Bahari. Kisha Mungu akaona ya kuwa ilikuwa vyema.11Mungu akaendelea kusema: “Dunia na itoe majani, mimea inayozaa mbegu, miti ya matunda inayozaa matunda kulingana na aina zake, ambayo mbegu yake imo ndani yake, juu ya nchi.” Ikawa hivyo.12Nayo dunia ikaanza kutokeza majani, mimea inayozaa mbegu kulingana na aina yake na miti inayozaa matunda, ambayo mbegu yake imo ndani yake kulingana na aina yake. Kisha Mungu akaona ya kuwa ilikuwa vyema_Mwanzo 1:1-12

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina na pia kaka Ray Ahsanteni kwa kuungania nami na pia wengine waliopita hapa kimyakimya ahsanteni.