Friday, August 31, 2012

TUMALIZE MWEZI HUU WA UJUMBE HUU: MWAISHA WAKUMBUKE WAZAZI!!


Nachukukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kunilinda/kutulinda katika mwezi huu bila ya magonjwa makali sana. Pia kwa kuweza kunipa/kuwapa nguvu wale wote waliopoteka na kuweza kurudisha mioyo yao na kuomba msamaha. NAWATAKIENI WOTE MWISHO MWEMA WA JUMA/WIKI NA PIA MWEZI.  IJUMAA NJEMA!!!

9 comments:

sam mbogo said...

Mdundo ni mtamu sana,na ujumbe wake ni safi.wazazi ni muhimu sana,pia walezi nao ni muhimu.tusijisahau kama bado tunao wazai, tuwa tunze, bila wao kwa asilimia mia tusingekuwepo hapa duniani,pamoja na mapungufu yao.kaka s

Yasinta Ngonyani said...

kaka Sam! ni kweli kabisa tusijisahau sana hata tu kuwaambia kuwa twawapenda na kuwashukuru. Kuwakumbuka mara tu unapopata nafasi...hakuna kama wazazi/walezi...

Emmanuel Mhagama said...

Isifike mahali mzazi wako akakununia, ni balaa. Watu wengine wakishajua tu kuoga na kupaka mafuta ya kunukia basi wanajiona high class hata hawataki rafiki zao wawafahamu. Swala siyo kuwaficha, bali kuwaweka katika hali ambayo uanataka unataka wawe nayo, basi.

Dada Yasinta, mie kesho Lundusiiii!! Nyumbani ni nyumbani tu, na mwenda kwao si mtumwa.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhagama! Yaaani watu wa namna hiyo wapo tena wengi tu...Salimia sana wote huko Lundusi..mweh umenitamanisha kweli...

sam mbogo said...

kwa uzoefu kidogo,hakuna kitu huwa vijana/watoto hujisahau ,hasa kipindi mmoja wa mzazi wako akiugua na ikatokea kulazwa sibitali.kipindi hicho huwa ni kigumu na mara nyingi usipokuwa mwangalifu unaweza kukufuru hasa kutokana na mahangaiko ya kumuuguza mzazi wako huyo.kuna mengi huwa yanajitokeza ambayo mzazi anayafanya ambayo wewe kwa wakati huo utayaona kama ni upuuzi,kwani huwa wanakuwa kama watoto wadogo.nimuhimu kujipanga kiakili nakisakolojia ili umuuguze mzazi wako vizuri ,pesa haisaidii kukamilisha upendo nauvumilivu katika muda wote huo wa kuuguza. haya upendo na uvumilivu kwa wazazi wetu utawale daima. kaka s

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! ulichosema ni kweli kitu hapa si pesa au zawadi..ni kama huo mfano ulioutoa pia inatosha sana kwa kuwatembelea kama huishi nao ni zawadi kubwa sana kuwataka hali na kuwasaidia vikazi vikazi na kuwapa ushauri na kubwa zaidi kuwajali na kuwathamini.Uvumilivu unatakiwa sana kwani kama kaka Sam alivyosema hapo sasa huwa tunabadilishana...kazi.

ray njau said...



1Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika muungano na Bwana, kwa maana hilo ni jambo la uadilifu:2“Mheshimu baba yako na mama yako”; ambayo ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi:3“Ili mambo yakuendee vema nawe ukae muda mrefu duniani.”4Nanyi, akina baba, msiwe mkiwakasirisha watoto wenu, bali endeleeni kuwalea katika nidhamu na mwongozo wa akilini wa Yehova._Waefeso 6:1-4

Salehe Msanda said...

Shukrani
Tunashukuru kwa kutukumbusha kuwakumbuka wazazi maana bila wao na mapenzi yao mema tusikuwepo pamoja na kujidai kwetu.

kila la kheri.

Anonymous said...

It's in fact very complicated in this full of activity life to listen news on Television, so I simply use the web for that reason, and take the most up-to-date information.

Have a look at my page ... Mohamed Jaquez