Tuesday, August 7, 2012

HAYA TWENDEE, TWENDE,TWENDE USICHOKE...!!!!

 Huyoooo anakuja, huyooo anakuja..anakuja anakuja....
.....na hapa ndiyo nimefika  golini...hii ilikuwa leo asubuhi...nimepanga kupata dhahabu ya olimpiki ..LOL
mazoezi tu kwa ajili ya afya ..ngoja nikapalilie bustani yangu sasa...

10 comments:

Anonymous said...

Hongera kwa mazoezi ya kuuweka mwili katika afya njema. Ni leo tu au kila siku?

batamwa said...

ya hapo lazima upate medali ya olimpiki

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina hapo juu...hii ni kila siku na ni tangu nilivyoanza mchakamchaka shule ya msingi na sasa imekuwa desturi yangu...

batwana!nitachukua medali ya olimpiki kwa ajili ya Tanzania yangu.....

emuthree said...

Jitahidi uje utuokoe maana sisi ni kichwa cha mwendawazimu , sijui tunaweza kushinda fani gani, labda ya kuongea,na kuongea kwenyewe....

Interestedtips said...

nadhani ulikuwa unaimba...mchaka mchaka chinja, alimselema alija.....hahahah, safi sana nimependa ufanyaji wako wa mazoezi, jiandae mwakani tupate medali

Unknown said...

haya tuhamasishe na wengine uuuuuwwwwwi

Fadhy Mtanga said...

hongera sana. Nami nipo bustanini wakati huu nalimalima.

Rachel Siwa said...

Alisemaaa alisemaa Alisema Nyerere Alisemaa Vijana wangu wote mmelegea Sharti tuanze Mchaka mchaka chinjaaaa!!

hahahaha dada Kadala lazima upate Medali!!!!!!Hongera sana.

Ahsante kwa kutuhamasisha, haya da'Jennifer mwana Chinga1 tumuunge mkono da' Yasinta.

Yasinta Ngonyani said...

emu-3! wewe ngoja tu yaani hapa hakuna mchezo...ni kweli kuongea twaweza sana.
Ester! kama ulikuwepo huo wimbo halafu nikabadili adiamini akifa mimi siwezi kulia ntamtupa kagera awe chakula cha mamba....Ahsante kwa kupenda ufanyaji wangu mazoezi na kweli najiandaa si mchezo sasa mchezo umekwisha..nawe unakaribishwa kujiunga nami...
Dada Changi1! hakuna uwiiii haya twende dada...
Mtani Fadhy..Ahsante. Bustani ndio sehemu yangu nishindayo...hongera nawe..
Kachiki! yaani nawewe ndo kama ulikuwepo huo wimbo na halafu kama ulivyosema mpitie J.mwana wa Changi na muje lazima tupate medali taratibu ndio mwendo tutafika tu...

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Pamoja sana yani...nami kila asubuhi hukimbia baharini kwa nusu saa lakini mmmh...shughuli