Sunday, August 19, 2012

KAPULYA LEO ANAWATAKIENI JUMAPILI HII KWA TASWIRA HII AU NISEME KWA MTINDO HUU/MWANAMTINDO WA JUMAPILI HII!!!!

 Haya hapa sijui ilikuwa ni ukaguzi wa meno....
 ...hapa kama vile alikuwa anakimbia  maratoni? 
na hapa naona alikuwa anampungia jirani mkono  au labda alikuwa anaota jua maana ndo kwanza ile miezi ya jua inaanza...kaazi kwelikweli au sijui tusea raha jipe mwenyewe...JUMAPILI NJEMA KWA WOTE NA PIA UPENDO NA FURAHA VITAWALE NYUMBANI MWENU....

7 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Jumapili njema nawe pia pamwe na familia yako hapo kunyumba!

Rachel siwa Isaac said...

J'pili njema na Asante kwa picha.kADALA Unavituko saaaana.ooohh nilisahau, Eid Njema.

EDNA said...

Jumapili njema kwako pia mdada,nimecheka vituko vya hizo picha mpaka basi.

Emmanuel Mhagama said...

Nawatakieni Jumapili njema pia pamoja na Eid Mubarak kama mnahusika.
Ila kwetu sisi watanzania kwa jinsi tulivyo wavivu wa kufanya kazi, kama tungeweza kubadilisha tarehe ya sikukuu basi sina shaka tungeihamishia kesho Jumatatu ili tupate siku mbili za kupumzika badala ya moja. Ndiyo maana zamani tulikuwa na mtindo wa kufidia. Tunakula sikukuu Jumapili kama leo halafu tunapumzika kesho. HUU NI UVIVU ULIOKITHIRI. Amani kwenu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Chacha! Jumapili yangu ilikuwa ya kawaida.. namshukuru nyumba na naamini nawe ulikuwa na jumapili njema hapa kunyumba.

Kachiki! si unajua mtu unaishi mara moja tu na kama kufanya kile ambacho hujakifanya na unatamani kufanya wakati ndio huu...Na nina imani jumapili yako pia ilikuwa njema ...

Edna! nafurahi kama hizo picha zimekufanya ucheke..kucheka ni afya..Ahsante na nina amani j2 yako ilikuwa njema ambayo iliandamana na kicheko...:-)

Kaka Mhagama! Ahsante kwa yote ..kweli jumapili hii ilikuwa na matukio mawili jumapili ..pia idi..halafu umenichekesha kweli kuhusu kutaka kupumzika...

Ester Ulaya said...

Mimi hilo shati nimelipenda sanaaaaaaaaaa, limekutoa kwakweli na umependeza sana

Yasinta Ngonyani said...

Ester! si shati ni gauni /Tunika..ahsante kwa kulipenda na kuona limenipendeze...