Monday, August 27, 2012

BARANI AFRIKA:- UTAMADUNI WA KUSIMULIA HADITHI BADO NI MUHIMU!!!

Hadithi kama tujuavyo ni njia ya maridhiano isiyo na gharama na ya kudumisha utamaduni.

Wengi wetu tunakumbuka nyakati ambazo wazazi au mababu na mabibi zetu walipokuwa wakitusimulia hadithi za kufurahisha zilizotokea zamani. Nilipoiona picha hii nimekumbumbuka sana zamani nilipokuwa mdogo wakati wa jioni wote mnakusanyika na kusikiliza hadithi na hapo hapo mnamenya karanga au kupukuchua mahindi na hapohapo mnaota moto.....

3 comments:

Ester Ulaya said...

huu utaratibu ulikuwa bora sanaaaaaaaaa
yaani nimemisss haya mambo

ray njau said...

@Ester;
----------
Mhubiri 1:1-11

1 Maneno ya mkutanishaji, mwana wa Daudi, mfalme katika Yerusalemu. 2 “Ubatili mkubwa zaidi!” mkutanishaji amesema, “ubatili mkubwa zaidi! Kila kitu ni ubatili!” 3 Mwanadamu anapata faida gani katika kazi yake yote iliyo ngumu anayoifanya kwa bidii chini ya jua? 4 Kizazi kinaenda, kizazi kinakuja; lakini dunia inasimama mpaka wakati usio na kipimo. 5 Pia jua limechomoza, na kushuka, nalo linajitahidi kwa nguvu kwenda mahali pake ambapo litachomoza tena.

6 Upepo unaenda kusini, nao unazunguka kuelekea kaskazini. Unaendelea kuzungukazunguka sikuzote, nao unairudia mizunguko yake.

7 Mito yote ya wakati wa majira ya baridi kali inaenda baharini, hata hivyo bahari haijai. Mahali inapoenda mito hiyo ya majira ya baridi kali, hapo ndipo inarudi ili iende tena. 8 Mambo yote yanachosha; hakuna mtu anayeweza kuzungumza juu yake. Jicho halitosheki kuona, wala sikio halijai kwa sababu ya kusikia. 9 Lile ambalo limetokea, ndilo litakalotokea; na lile ambalo limefanywa, ndilo litakalofanywa; na kwa hiyo, hakuna jambo jipya chini ya jua. 10 Je, kuna lolote ambalo mtu anaweza kusema juu yake: “Ona hili; ni jipya”? Tayari limekuwako tangu wakati usio na kipimo. Jambo ambalo limetokea lilikuwako kabla ya wakati wetu. 11 Watu wa nyakati zilizopita hawakumbukwi, wala wale watakaokuja baadaye hawatakumbukwa. Nao pia hawatakumbukwa kati ya wale watakaokuja baadaye.

Yasinta Ngonyani said...

Ester yaani inasikitisha sana mila hii inafifia...
Kaka Ray! Ahsante kwa neno/Somo.