Wednesday, August 22, 2012

WANAWAKE KUTEMBEA NUSU UCHI, KUMBE WANA LAO JAMBO.....!

Leo katika KIPENGELE CHETU CHA JUMATAN YA MARUDIO YA MADA AU MATUKIO MBALIMBALI.  KATIKA PITA PITA ZANGU LEO NIMEPAMBANA NA HII  KWA MZEE WA UTAMBUZI.

 Kuna wakati wanaume hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nusu uchi huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume. Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba, sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo.


Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao. Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo. Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.

Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri. Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa.

Hebu angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya. Huvaa nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura zao, bado wao ni wazuri sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo wanaume na hata wanawake wengi huyapenda au kutamani kuwa nayo.
Wengi hawavai tu nguo hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni kimbilio la udhaifu wao.
PANAPO MAJALIWA TUONANE TENA JUMATANO IJAYO KATIKA KIPENGELE HIKI CHA MARUDIO.!!!



34 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

duh! bonge la darasa...

nikiwaona sitawacheka ama kuwachukia bali nitawahurumia...lol!

Emmanuel Mhagama said...

Hili linaonekana limekaa kisaikologia zaidi na pengine linahitaji kuangaliwa kwa undani zaidi. Binafsi naamini kwamba kila mmoja ana udhaifu wa aina yake, tofauti yetu ni namna gani tunaweza kukabiliana na madhaifu hayo. Hata wale ambao hawavai hizo nguo fupi na za kubana siyo kwamba hawana udhaifu, sidhani hivyo. Hapa ningesaidiwa sana kama ningepata maoni ya wahusika, yaani akina dada. Je, ni kweli swala kwamba swala la kuvaa nguo fupi na za kubana linachangiwa kwa upande fulani na nia ya kuficha madhaifu. Hata kama wewe siyo ya mtazamo huo lakini inawezekana unajua jambo hili vizuri hasa mnapokuwa katika mazungumzo ya akina dada. Nipeni maoni.

Anonymous said...

Hakika hii ni aibu kwa mama na dada zetu wapendwa. na kwa staha na maadili si hakika kama ni vema picha hii kuwekwa hapa kwa ajli ya majadiliano.

Anonymous said...

Yasinta!!
Unaheshimika sana lakini nasikitika sana kuwa umeamua kuitundika picha hii ya aibu hapa kibarazani kwako bila aibu ukiwa ni mwanamke wa kiafrika katika malezi ya kikristo.Hii ni aibu tena ni aibu kwako na wapenzi wa kibaraza chako.

Anonymous said...

Hakika picha hii imemshushia heshima mama wa kibaraza hiki.Hivi familia yake wanapoangalia picha hii wanamuonaje mama yao???

Anonymous said...

Annony hapo juu, naomba mtambue kwamba kilicho muhimu kilikuwa ni kufikisha ujumbe kwani ni kipi cha ajabu katika hizo picha wakati kila siku hao watoto wentu wanaona picha za utupu kila kona kuanzia mitaani hadi kwenye luninga zetu.

Mlichoandika hapo juu ni unafiki tu na ndio maana mmeficha hadi ID zenu.

Yasinta endelea kutuelimisha bana......

Ni mimi

Ramson Kayanda

Anonymous said...

Yasinta inabidi uwe unachuja mada za kuweka hapa kujadiliwa!Kama alivyosema aliyetangulia kweli wanao wakiona hivyo hawawezi kukuelewa. Mie nilipofungua tu kuona hizo picha hata sikutaka kusoma kinachozungumziwa. Endelea na mila na desturi zetu za kiafrica ´na mambo mengine ya kutuelimisha tunayafurahia kulikoni hizo picha za aibu.

Anonymous said...

Anonymous said...
Yasinta inabidi uwe unachuja mada za kuweka hapa kujadiliwa!Kama alivyosema aliyetangulia kweli wanao wakiona hivyo hawawezi kukuelewa. Mie nilipofungua tu kuona hizo picha hata sikutaka kusoma kinachozungumziwa. Endelea na mila na desturi zetu za kiafrica ´na mambo mengine ya kutuelimisha tunayafurahia kulikoni hizo picha za aibu.

==================================
Yasinta;
Hakika sasa umechoka na umeanza kupotoka na hata leo wadau wako tunaogopa kuonyesha majina yetu kwa jinsi ulivyoamua kutuabisha dada zako wa kiafrika.Ama kweli mgema akisifiwa sana mwishowe tembo hulijaza maji tena ya chooni.Mungu wangu,Mungu wangu aibu gani hii binti wa kikatoliki uliayesomeshwa hadi ngazi ya usista leo unaamua kuasi mila za wazazi wako na muumba wako kule mbinguni.

Anonymous said...

Duh;
Madudu na uchafu mtupu na sikutegemea blogu hii inaweza kutuwekekea mambo haya ya umalaya wa kutuonyesha makalio ya wanawake.Wewe Yasinta unaonyesha makalio ya wanawake wenzio bila hata aibu?Asante sana kwa kutuabisha!!

Anonymous said...

Hakika hii ni aibu ya karne kwa wapenzi wote wa kibaraza cha dada Yasinta!!!!!!!!

Rachel Siwa said...

Duhh Wanawake tuna mambo sana, Mbona Wanaume/kina kaka hawavai hivyo? kama ipo ipo tuu.

ray njau said...

Asante sana da'Rachael;hakika mtoto wa kike umenena.Hapa tuseme wanawake wanadhalilishwa na jamii au wanaidhalilisha jamii yao?
-------------------------------------
9 Vivyo hivyo natamani wanawake wajipambe kwa mavazi yenye mpangilio mzuri, pamoja na kiasi na utimamu wa akili, si kwa mitindo ya kusuka nywele na dhahabu au lulu au mavazi yaliyo ghali sana, 10 bali kwa njia inayowafaa wanawake wanaodai kumheshimu Mungu, yaani, kupitia matendo mema._1Timotheo 2:9,10.

Rachel Siwa said...

Asante kwa Neno kaka Ray.

Anonymous said...

Jamani tumsaidie dada yetu. Kweli umepitiliza sana dada yetu hapo. Ila mbona hatuoni Yasinta akizijibu comments kama ilivyo taratibu yake kujibu kwa kumtaja kila mmoja na hata asiye na jina. Tunaomba dada Yasinta utupe feedback kutokana na hizi comments. Waliosupport ni wanafiki usiwasikilize hata kidogo.

Anonymous said...

Dada Yasinta uko wapi? Tunasubiria utoe maoni yako kama hukubalianai au unakubaliana na hizo picha. Tusikie toka kwako.

John Mwaipopo said...

somo zuri. tusifiche kichwa kwenye mchanga mithili ya mbuni huku mwili wote uko nje na kujiaminisha eti hatuonwi. somo zuri yasinta. elimu zingine zinahitaji kujifanya kichaa kidogo kuziwasilisha (kama ulivyofanya yasinta). pia pole in andvance maana kuma wadada hapo juu kwenye comments wamekasirika sana.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mimi binafsi sipendezewi na mavazi hayo lakini nadhani si VEMA kwa wale wote WAOGA wa kuonesha majina wanaojifanya wanajua maadili na kushambulia mwenye blog kwa ksingizio cha UMEVUKA MIPAKA

1. Hawajiamini kwa kuwa ndo sababu wameficha majina yao
2. Hawajasoma habari hiyo...macho na akili yao kwa kuwa yamezowea kuona upuuzi yamejikita hapo tu

Ikumbukwe kuwa habari hiyo si ya Yasinta bali ni kipengele cha marudio ambacho amekichukua kwa Mtambuzi Kaluse. Mlitegemea atafute picha nyingine wakati Kaluse keshaweka ya kwake iendanayo na habari?

tuache unafiki kwa kuwa hivo mnavoviongelea kinadharia haviko hivo.

Anonymous said...

Ilikuwa sio lazima kuweka hiyo habari hata kama ameitoa kwa kaluse. Kwani kila kitu wanachofanya wengine lazima kichukuliwe na kuwekwa hapa? Hakuna habari mbadala ambayo ingewezwa kuwekwa hapa? hapa namaanisha kuisoma hiyo habari kwa Yasinta imemshushia sifa/hadhi yake, heri waliotaka wangeisomea huko huko, tunajali sana kinachowekwa humu na sio kuwa amekitoa kwa fulani! maadali yazingatiwe ya hii blog, msimharibie Yasinta kumsifia mambo yasiyofaa humu. Kingine mwenyewe Yasinta hajibu chochote kama hakuna tatizo hapo angeishazijibu comments mda ila hajacomment hata! Watanzania tu watu wa ajabu sana jambo halipendezi watu wanasifia na wakati mwingine ni UNAFIKI tu. Tumasaidie na sio kumharibia dada yetu. Nyie mnaocomment kusuppport naweza kusema mnasupport KINAFIKI. Watanzania tu watu wa ajabu, kitu hakifai watu watasupppport ili ukaaibike mbele ya safari.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Pole sana Anony! Ungekuwa si mnafiki usingejificha nyuma ya pazia ukielekeza mashambulizi yasokuwepo.

ninachokiona ni kuwa wewe na wenzio mnakimbia kivuli chenu wenyewe...kwa kuwa aidha ndivo mvaavyo ama habari inawahusu

anyway, ambaye hajawahi KUTENDA DHAMBI(kuvaa hivo ama kuficha madhaifu yake katika vilivyotajwa navisivyotajwa kwenye habari hiyo) na awe wa KWANZA kumlaumu (kumtupia jiwe la kwanza) Yasinta!

Anonymous said...

Kwanza wote wanaosifia hii mada ni wanaume! yani tabu sana na nadhani mmefurahia hayo. Hapa Mie sijawahi na sitawahi kuvaa kiaina hiyo. Naishi ulaya navaa nguo za heshima kama niwapo Tanzania. Sithubutu kugeza huo uozo wa mavazi, sivai nguo fupi, za kubana, siweki nywele dawa,nk. napenda utanzania wangu sana na najiheshimu. Nadhani huna cha kuongea na unaendelea kuandika sababu zisizoendana na hii mada, tunajaribu kumsaidia na sio kumtupia mawe, kama biblia inavyosema. kwa kuandika hivi ni moja kwa moja kuwa Dada Yasinta amekosea mana hii ina mana hiyo,narudia ulichoandika
"anyway, ambaye hajawahi KUTENDA DHAMBI(kuvaa hivo ama kuficha madhaifu yake katika vilivyotajwa navisivyotajwa kwenye habari hiyo) na awe wa KWANZA kumlaumu (kumtupia jiwe la kwanza) Yasinta!"
waTZ tuache unafiki, tena wanaume hasa! Yasinta tunaomba maoni yako mana uko kimyaaaa vipi?

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

ha ha ha ha ha haaaaaaa! Majibu yako yanatutanabahishia kuwa wewe ni mtu wa aina gani...

Pole annony!

Anonymous said...

Hapa tayari matatizo yameaanza na haya malumbano sasa yanakoelekea si hakika sana na matokeo yake.Mada imeachwa na watu wanatafutana majina.Wewe changia mada na usonge mbele.Yasinta kaamua kujifunua kuwa yeye ni mwanamke wa aina gani na hayo ndiyo ayapendayo.Kazi ni kwake na watu wake.Muacheni jamani......

Anonymous said...

Huyu mama ni mcharuko wake mwenyewe na hakulazimishwa kuchukua hiyo picha.Kama mwanamke ameamua kuonyesha aibu ya wanawake wenzake ili kujifurahisha au hizi ndizo tabia zake mwenyewe?Mnamtetea hata bila aibu!

Anonymous said...

john mwaipopo hebu rekebisha hapo mwisho kidogo ni ashakum si matusi umeandika k...a badala ya kuna

Fadhy Mtanga said...

Kufikisha ujumbe kwa jamii kuna mambo mengi sana. Wengi wanapendwa wafikishiwe ujumbe uliopakwa pakwa rangi na kuuficha ukweli. Lakini ujumbe ambao una rangi zake halisi huwakasirisha baadhi yas watu kwa kuwa kikawaida huwa hawapendi kuambiwa ukweli.

Tukiweza kuustahimili ukweli, hatutouogopa hata usipovalishwa nguo.

Ahsante kwa hili darasa.

Rachel Siwa said...

Mimi sioni sababu ya kutukana hapa,Sasa tunakuelekea siyo kabisa, kwani kama mtu hupendezwa na kitu si mmwambie kistarabu Waungwana?

Yasinta si mmbaya kama mnavyomdhania/mchukulia wengine mnamfahamu ila mmeamua kuficha majina kwa sababu zenu.yaani ni wadau wa blog hii.

Vyema kuambizana/kuelimishana kwa Amani.lakini si kwa matusi,kashifa na kumdhihaki.

Hivyo hatujengi wapendwa tunazidi kuboa.

Nafikiri yeye hakuwa na maana mbaya kwa kuwadhalilisha/kutudhalilisha lakini kila mtu anaupokeaji wa Ujumbe kwa Mitazamo tofauti.Pia naye ni Bin'Adamu mtazamo wake kama umekwenda vibaya ni kumwambia tuu da'Yasinta picha za leo hazitupendezi/hazinipendezi kwa Upendo tuu.

Haya ni Maoni/Mtazamo wangu Wapendwa sina nia ya kukosoa mtu.

KAMA NIMEMKWAZA MTU NAOMBA NISAMEHEWE.PAMOJA SANA.

Simon Kitururu said...

Mada poa! Na wadada pichani wako poa sana!Asante kwa shule Yasinta! Kumbuka huwezi kufurahisha kila mtu duniani! Mie umenifurahisha na kunifunza kwa kuweka hii mada!

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu zangu wapendwa hapa hakuna mtu ananitetea mimi kila mtu anasema kwa niaba yake. Nimeona mshtuko wwenu na nilikuwa nasubiri nafasi nzuri ili niweze kusema kitu. Kuhusu hiyo picha kama wasomaji wa blog hii naomba niwaulize wote walionitaka kuitoa hii picha je ni picha ndio kikwazo? je mmesoma kilichoandikwa? Na kama alivyosema dada Rachel kwa nini tusiambizane kwa uungwana? Nia yangu hapa haikuwa kuwaumiza watu ila kuwakilisha ujumbe. Ahsante!!

Anonymous said...

pole sana nangonyani hiyo ndio siri kubwa ya uandishi kuwa unakuwa kama jalala kila mtu anatupa lake huko na hii huchangiwa na upeo finyu wa sisi binadanmu mimi nakupongeza kwa asilimia zote na za nyongeza juu lengo ni ujumbe na hayo yapo na hao wote wakosoao wanajua sana basi ni hurka za kibinadamu nani asiyejua kama hali hizo zipo tena hapo bongo kwetu wapite mitaa ya ohio na ostabey international school kariakoo sinza kinondonijioni kwa picha ulizoweka mbonna zinanafuu sana baki ktk mitandao ambayo ipo wazi kila kona yaonyesha vibweka zaidi ya hizo picha kwa taalifa zao sasa hivi chinga wote wauzao cd katika makutano ya barabara zote wanauza cd zenye picha chafu hizo zako ni nzuri kwanza zinatizamika lakini hizo hazitizamiki etu mtu anajinasibu kwa kusema eti maadili ya tanzania labda watu wengine wapo gizani sio tanzania sasa hivi maadili ki tanzania ni katika familia yako tu achana nao hao endeleza libeneke lako na kutuhabarisha kama kawa nabambu mbawala

ray njau said...

Yasinta;
Asante sana kwa utetezi wako nami nakushauri ujipange vizuri uje na utetezi makini zaidi kwa manufaa ya wadau wa blogu yako.
-------------------------------------
Unaweza kusema hivi:
Asanteni sana kwa maoni yenu na kila mdau kwa nafsi yake.Sina uwezo wa kumlazimisha mtu aweke imani katika imani yangu lakini nilicholenga mimi ni kutoa elimu kwa jamii yangu lakini picha iliyotumika haikuweza kuwakilisha kile kilichotarajiwa.Kwa taarifa hii naomba samahani kwa wote walioathiriwa kwa namna moja au nyingine nami nimejifunza kitu kupitia maoni yenu yote.Tafadhali tuendelee kusafiri pamoja katika jehazi la maisha na mafanikio.Karibu sana!
Wenu katika utendaji;
Yasinta Ngonyani.
===================================

John Mwaipopo said...

vidole vilikosea. haikuwa dhamira yangu. kukosea huko hakuna uhusiano na mada yenyewe inayohusu 'utupu'

Anonymous said...



Kimsingi hili ni tatizo sugu ambalo linaepukika lakini kuna ugumu kidogo katika kuliepuka moja kwa moja. Mitaani tunakoishi wapo wanaume ambao wasione msichana mrembo akipita, lazima wataanza kumsumbua kwa kumuita na wengine kufikia hatua ya kuwafanyia vitendo vichafu. Mbaya zaidi ni kwamba wanaume hao hufanya hivyo hata kwa wanawake ambao ni wake za watu au wenye wapenzi wao.

Tabia hii huwakera sana baadhi ya wanawake hasa wale wanaojiheshimu na kuziheshimu ndoa na mahusiano yao.
Hata hivyo, kuwaepuka wanaume wakware wakati mwingine huwa ngumu kwa kuwa wengi wao ni micharuko, yaani hawajali wala kufikiria kinachoweza kuwapata baadae.

Niseme tu kwamba, wanaume wa aina hii wapo wengi tu huko mtaani ila kwa mwanamke anayeiheshimu ndoa yake au uhusiano wake na akaweka nia ya kuwaepuka, inawezekana! Nikupe tu baadhi ya mbinu ambazo zinaweza kukusaidia kuondokana na usumbufu kutoka kwa wanaume wakware.

Punguza ukaribu, acha utani na wanaume

Wanawake wengine ni wa ajabu sana. Unamkuta anajenga ukaribu sana na baadhi ya wanaume na kufikia hatua ya kutaniana nao katika mambo ambayo mwishowe huwa kutongozana.

Mwanamke aliyeolewa ama mwenye mpenzi wake hatakiwi kujenga ukaribu sana na wanaume wa pembeni. Cha msingi ni kuwaheshimu na kuwachukulia kama watu amambo akiwachekea anaweza kuja kuvuna mabua.

Unapopita sehemu ukakuta wavulana wamekaa, wasalimie kisha chukua hamsini zako, utani utani wa kijinga epukana nao kwani mwisho wa siku watakutongoza na ukionesha kuchukia watadai walikuwa wanakutania kumbe wako ‘sirias’.

Usijishebedue kwao
Baadhi ya wanawake hujitakia wenyewe usumbufu kwani tabia zao huwafanya wasiheshimike mbele ya jamii na kuonekana kwamba ni jalala. Unakuta mwanamke anapita mbele za wanaume kisha anatembea kwa kujishebedua huku akitingisha mauno yake makusudi, hapo unatarajia nini?

Achilia mbali hilo, wapo baadhi ya wanawake ambao ni rahisi kuchukuliwa na wanaume. Yaani hawawezi kusena hapana! Ukiwa na tabia hiyo tambua tu kwamba, kila mwanaume atakusumbua. Jiheshimu na wanaume nao watakuheshimu na hawatakuwa na muda wa kukutamkia maneno yasiyofaa.

Mavazi ya kimitego yapotezee
Wanawake wengi sana hukosea katika suala zima la uvaaji. Baadhi yao hupendelea kuvaa mavazi yanayoonesha maungo yao kiasi cha baadhi ya wanaume kuwachuklulia kuwa ni machangudoa.

Ni kweli kwamba mavazi ya mtu hayawezi kumfanya akaingizwa katika kundi la watu fulani na pia kila mtu anao uhuru wa kuchagua avaeje lakini, kwa uhalisia mwanamke asiyeujali mwili wake kwa kuvaa nguo zisizokuwa na heshima, asitarajie kuuepuka usumbufu wa wanaume wapenda ngono. Ni lazima watamtongoza na wakati mwingine kumfanyia vitendo vya kumdhalilisha.

Nadhani ifike wakati uondokane na ulimbukeni wa kwenda na wakati hasa kwa wewe mwanamke ambaye umeolewa ama una mpenzi wako. Vaa mavazi ya heshima kila unapokwenda.

Mavazi yanayoonesha mauno yako yavae ukiwa na mpenzi wako chumbani. Naamini kwa kuvaa hivyo, kidogo utakuwa unapunguza ile kasi ya wanaume wakware kukusumbua.

Niseme tu kwamba, wanaume siku hizi wametawaliwa na tamaa zisizokuwa na msingi. Ukitaka wakusumbue watakusumbua kweli na wakati mwingine wanaweza kukushawishi ukamsaliti mpenzio wako.

Kikubwa ni mwanamke kuwa na msimamo. Kutokukubali kugeuzwa kiti cha daladala kwamba kila mtu anaweza kumchezea. Naamini msimamo huo pamoja na mambo hayo niliyoyataja hapo juu unaweza kuepukana na usumbufu huo kutoka kwa wanaume wakware.

Usipokuwa makini na haya niliyoyazungumza leo, inamaanisha uko tayari kusumbuliwa na uko tayari kuachwa na mpenzi wako. Kuwa makini.

Anonymous said...

Ni kweli kabisa dada uliyechangia mada hapo juu. Na ukiangalia hata hapa walio support hii mada positivley ilivyo ni wanaume, hawawi against it, nadhani ni mmoja tu alikuwa against it. Usikute ndio hao hao uliowataja hapo juu. Ila wanwake wengi hawakusupport kabisa. Jamani wanaume mjirekebishe. Kuna mmoja siku akuiandika Dada Yasinta angevaa nguo za kumshika mwili angependeza zaidi na kaptula, ila Yasinta alujibu haitatokea! Wanaume kweli mna shida zenu Mungu awasaidie.

Anonymous said...

Watu wanahoji Yasinta umepata wapi huu ujasiri wa kukubali hii picha ya Kaluse iwepo kwenye blogu yake?Muachie Kaluse mambo yake.Huyo Kaluse hakuna mchangiaji hata mmoja aliyeweza kukubaliana naye au kumkatalia lakini kwa tukio baya sana ni Yasinta pekee yake aliyeichaingia.Kwa kuwa kule kwa Kaluse hakukuwa na wachangiaji akaona afiche aibu yake kwa kuileta hii mada hapa kwake ili apate wafuasi katika kutangaza aibu ya wanawake wenzake.Wewe Yasinta hao watu wako hapo juu mnajidai kusema mada ni nzuri wakati hata sithubutu kuifungua mbele ya familia yangu hata cafe watanishangaa na ofisi naweza hata kufukuzwa kazi kwa kutazama picha mbovu.Unatuonyesha nini wakati wanawake sasa thamani imepotea kabisa kwa kujitandaza uchi wa mnyama kwenye mawebisite ya kutafuta wateja huku wakijieleza hata maumbile ya viungo vya kiume yanayowapa raha.Wengine wanajigeuza kama majongoo na kuanika maziwa yao na kutanua kabisa meoneo ya siri huku wakitabasamu na usodoma wao.Hivi sasa wanawake wameamua kuabisha familia zao na jamii kwa ujumla na Yasinta sasa hakika umepotea kabisa.Lakini kwa kuwa umeamua hivyo endelea na maisha bila mafanikio.Poleeeeee.
---------------
Hermanus Komba
Songea
TZ.