Saturday, August 25, 2012

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO KUOMBA RADHI/SAMAHANI!!

Nachukua nafasi/fursa hii na kuwaomba wote radhi kwa picha niliweka hapo jumatano 22/8 katika KIPENGELE CHA MARUDIO. ILE PICHA IMETOLEWA. Nia yangu haikuwa /sikulenga kuwaumiza au kuwa/kumdhalilisha/aibisha mtu. Bali ni kutoa elimu kwa jamii nasema tena KWA TAARIFA HII NAOMBA SAMAHANI KWA WOTE WALIOATHIRIWA kwa namna moja au nyingine. Nami nimejifunza kitu kupitia maoni yenu.Naomba tuendelee na safari pamoja.Yasinta/kapulya.

11 comments:

isaackin said...

nilichoona nikwamba kuna mtu alipost coment ya kwanza ambayo ina link ya porn site!sijui kama ni hiyo inafanya uombe msamaha au vipi,by the way mada yako uliiyoongea pale ilikua muafaka kabisa naona wadada wengi wamekasirika sababu imewagusa.ni kweli wadad wengi wanatembea nusu uchi siku hizi,tena bongo ni nusu uchi na makufuli hawana kabisaa.sasa sioni haja ya wewe kuomba msamaha kwa ukweli ulioongea,kwa hilo la mchangiaji kuweka link ya porn ni kosa ambalo sidhani kama niwww umefanya hivyo,bali mchangiaji aliyeweka ametake advantage kwako kwani hujaweka striction kwenye comment post hapa kwako zinajitokeza pindi ukipost tu,so jaribu kuweka uwe unazipitia kwanza kabla ya kuzipost,vile vile kazi ya kublog ni ngumu dada lawama na matusi inabidi tuzoee tu,ila mwishowe we ndio unajua unafanya nini.weeek end njema,
na nyie wakina dada acheni kuvaa nusu uchi tumewachoka!

Rachel siwa Isaac said...

Hahahaha Kaka ISAACKIN umeongea kwa Ukali sana tofauti na sikunyingine,Najua nanyi kina kaka hampendwezi na Mavazi ya kinadada/wanawake wa leo,Asante kwa Ushauri kaka yangu.

Pia niungane nawe, kweli kazi ya kublog ni ngumu utakuta mtu anatukana pasipo sababu kabisa,
unaweza kuweka picha ya mtu kavaa vyema tuu lakini kumbe wanasababu zao binafsi ataanza kunanga na matusi juu.
Au kukutukana mwenye BLOGU. Hii inanikera sana sana.

Yaliyopita yamepita Waungwana Pole KADALA na Pole Waulioumizwa.Tuendelee kwa UPENDO NA AMANI.PAMOJA SANA.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

@Isack &Rachel: hakuna kitu kinachoitwa tusi.
Binafsi sijaona matusi ya walioguswa na mada/picha kwani wamejipambanua nayo na kutujulisha walivyo.

Nikiambiwa kwa mfano 'malaya' nikakasirika nitakuwa mjinga wa kutupwa kama yalosema ni ukweli na ntakuwa mpumbavu kama nikikasirika ilihali kilichosemwa ni uwongo

Anonymous said...

Yasinta, vizuri umeomba radhi. Ushauri wa bure siku nyingine uweke mada zinazodhalilisha wanaume tu, mada yenye aibu kama ile uliitoa kwa mwanaume na walioiunga mkono ni wanaume wengi hapa kwako. Je hujajifunza kitu hapo? mambo ya aibu wanayofanya wanawake, wanaume wanayafurahia mno na wanakuwa wakali kwa kina mama walio against. Soma comments za kitururu na mwaipopo na wengine. Hivyo kuwa mwangalifu sana unapoamua kuweka mada za aina hiyo hapa. Wanawake ndio taifa la kesho, walezi wa watoto wetu, wanamajukumu ya kuwafundisha watoto wao tabia njema nk. Sasa wanaume au wakina baba hawakai na watoto kuwafundisha hasa kwa sisi waafrica. Ndio mana wanaume wengi walikuunga mkono, ambao ni unafiki. Mie nimejifunza kitu kikubwa sana tena sana na nilikuwa against. Wanaume mmbadilike pia mkiona vitu hivyo kwa kina mama waambieni na sio kufurahia na kushinda mnavitazama. Samahani Yasinta nitarudia tena kuna mchangia mada mwanaume siku moja aliandika ungevaa nguo ya kukushika mwili inayoonyesha miguu na pia kaptula ungependeza zaidi! ila ulijibu kuwa huwezi kuvaa hayo mavazi kamwe. Walioomba uvae hivyo ni wanaume wa humu humu na sio wanawake..huoni kama hao wenzetu wanashida jamani! Tuendelee kulisukuma gurudumu la maisha na mafanikio wadau.

Anonymous said...

Swala ni kuwa Yasinta unaheshimika sana tena sana, sasa hatutegemei kuona madudu kwako wacha wengine waendelee kwa mida yao. Kwako ukiweka hayo wakina dada wengi watakuhama na utabakia na wanaume tu wanasupport. Tunashukuru tuendeleze maisha na mafanikio.

Anonymous said...

Inawezakana ni kweli yaliyosemwa.Hivi ni kweli? au hivi ni kweli? kwani yanahusu wanawake na aliyeandika ni mwanamke je angelikuwa mwanaume je ingekuwa je? na je? je ingekuwaje na je????????

Anonymous said...

Yasinta, umeandika picha imetolewa mbona tunaiona kwenye you might also like to see....umeamua kuibakisha kwenye kumbukumbu zako?

Anonymous said...

yasinta, jaribu kupunguza au kuacha kabisa COPY na PASTE ona sasa ilivyokugharimu

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii na kuwashukuruni waote mliopita hapa na pia nasema ahsante kwa yote pia kwa ushauri wenu.

Anonymous said...

Mhh tena imekuwa aibu ya Yasinta? Hebu wanawake tuache unafiki humu, maana hali huko nyumbani kwa wasichana na hata wamama watu wazima ni aibu tupu. Utakuta mwanamke ana mijinyama imetapakaa mwili mzima anakwenda kuvaa skin tight inayombana au anavaa kikaptura kidogo (hot pant) eti anakwenda na wakati. Na hao nao ni Yasinta kawatuma au kawaonyesha? Nyie mnaomlaumu Yasinta mna lenu jambo na mlikuwa mnatafuta pakuhemea au pakupumulia. Maana badala ya kuajadili mada mnakaa mnamjadili Yasinta na picha aliyoiweka na hivi si vitu kuwa Yasinta katunga au kenda kuwaambia hao wanawake wapige hizo picha. Wamepiga wenyewe kwa viranga vyao na wengine wazitundika kwenye facebook, wengine kwenye mablogu yao na msijifanye watakatifu sana kuwa hamuwendi kwenye hayo mablogu ya wanawake wanaovaa vimini au vichupi.

Kitu cha msingi kilichotakiwa ni kuangalia tatizo lilipo na jinsi gani tunaweza kulitatua ama kwa kuanzia kwenye majumba yetu. Watu mnamsema Yasinta eti ana tatizo wakati hapa hatujaona binti yake kavaa hot pants pamoja ya kwamba ni mzungu, lakini mabinti wa kiafrika kibao wengine wamama wazima wanavaa hot pants. Au wanavaa mini skirts bila hata ya kuvaa stockings kama wanavyofanya wazungu. Tunajifanya sisi ni wazungu zaidi ya wazungu wenyewe. Siku moja nilikuwa napata chai ya jioni na rafiki yangu wa kizungu akapita msichana amevaa hotpants pamoja na stockings na ilikuwa ni maeneo ya chuo, yule rafiki yangu mama mtu mzima wa kizungu akanambia "sijui kwanini wasichana wa kiafrika wanapenda kuvaa kama prostitutes" kwa kweli niliona aibu ingawa sikumjua yule mwanafunzi ametokea pande ipi ya Afrika.

Yasinta huna kosa wala hapa hakuna aibu yoyote wala hujamdhalilisha yoyote, kama hao wanaolalamika waliiona kwa Kaluse ina maana na blogu nyingine mpaka kwa Shigongo wanapitia na wameziona picha zaidi ya hii, these people are just picking on you. Aibu ni yake aliyepiga hiyo picha, yeye na wazazi wake maana ameamua mwenyewe kujiaibisha na kuwadhalilisha wazee wake.

Kitu kingine cha ajabu ni hiki je biblia inasemaje kuhusu sehemu zipi za mwanamke zifunikwe na sehemu zipi ziwe wazi? Kama wewe hufuniki sehemu zinazotakiwa kufunikwa basi na wewe ni aibu yako vile vile maana unatembea uchi; cleavage yote iko wazi, miguu na kichwa kiko wazi, so usimuone mwenzio ana dhambi sana simply because she sin differently than you!

Huu ni mtazamo wangu tu!!

ray njau said...

Huu ndio mwisho wa mambo, kila jambo limekwisha sikiwa: Mwogope Mungu wa kweli na kushika amri zake.Kwa maana huo ndio wajibu wote wa mwanadamu.Kwa maana Mungu wa kweli ataleta kila kazi katika hukumu, kuhusiana na kila jambo lililofichwa, liwe jema au baya._Mhubiri 12:13,14