Monday, August 6, 2012

TUANZE JUMATATU HII KIHIVI:- KILIMO....UKIITUMIA MIKONO YAKO KAMA INAVYOTAKIWA :-MATOKEO YAKE NDIYO HAYA...UTAKUWA MLO WA MCHANA WA LEO MBOGA/MAJANI YA MABOGA!!!

MBOGA YA MABOGA KWENYE UNGO...
Ni furaha ilioje kuweza kula chakula ulichopande mwenyewe, hapa ni majani ya maboga na ndiyo yatakuwa mlo wa mchana wa leo:-) Napenda kuwakaribisheni wote karibuni tujumuike..Si mnajua kulima analiama mmoja lakini walaji ni wengi.... Ndiyo nimeanza  kuitengeneza....

7 comments:

Ester Ulaya said...

sisi huwa tunauita MSUSA, ukipika na karanga tamuuu, ukichanganya na bamia inakuwa mrenda, yaani ni full enjoyment mdomoni, kweli siku imekuwa njema hadi sasa, naombea hadi jioni iwe njema

Yasinta Ngonyani said...

Sisi tunaita Pitiku yaani ukiipika na maji chumvi halafu uwe na pilipili mbuzi weweeeeee...na kama ulivyosema Ester ukichanganya na bamia inakuwa mlenda..Ndiyo unaweza kuweka karanga ila kwangu mimi ukifanya hivyo basi nitashinda njaa sio mboga hii tu zoteeeeeeeeee...Ila kuipika naweza sanaaa maana ungonini Karanga ndo kwenyewe...

Rehema said...

Mlongo mlongo pitiku hiyo nene mata kihulula waka.

Yasinta Ngonyani said...

Rehema! kwani uvi kwako tolei tu lupalu ubwelayi kuto kuhululusa mata waka:-)

ray njau said...

Akina huko jikoni hamjambo????????????

Rachel siwa Isaac said...

Mwahhhhhhhh oyeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!uwiiiii.hizo kelele nilizopiga hapa. Njaa dada Kadala.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray, wala usiwe na shaka hatujambo kabisaaaaaa. Na makaangizo yanaendelea.

Kachiki, Kachiki Njoo sasa kuna bonge la UGALI NA MBOGA si unakumbuka kuna ubenani wanaita "nyamuza" halafu najua wewe unapenda ya kutia tui la alzeti:-)