Friday, March 30, 2012

JIONI NJEMA NA KIPANDA HIKI CHA MZIKI/UJUMBE!!!


Najua Mwanamke akipenda anapenda kweli.....nimepapenda hapa...halafu anapomalizei eeh eeheeee.. mziki si mziki tu ni starehe, pia kuna ujumbe mwingi tu...tiwonage be´!!

SWALI LA WIKI HII!!!!

Umewahi kufanya maamuzi magumu sana kwenye maisha yako? ilikuwa ni kuhusu nini?haya funguka sasa!
NAWATAKIENI WOTE KILA LA KHERI NA MUWE NA MUDA MZURI NDANI YA MWISHO WA JUMA HILI LA MWISHO WA MWEZI HUU WA TATU.UPENDO DAIMA.

Thursday, March 29, 2012

JIONI NJEMA NA WIMBO HUU WENYE UJUMBE MWANANA!!!


Jioni njema jamani........

POROJO YA LEO !!!

Bwana mmoja karudi nyumbani toka kazini amechoka ile mbaya, akaingia ndani na kujitupa kochini ili aangalie TV. Akamwambia mkewe:-
- Niletee bia, karibu inaanza .
-Mkewe akapumua na akampa bia.
- Baada ya dakika kumi na tano akasema :-
-Nipe bia nyingie maana karibu inaanza.
Mke wake akamwangalia kwa kuchoka choka lakini akampa bia nyingine:
Alipokuwa amemaliza ile bia baada ya dakika kadha akasema:-
- Nipe bia nyingie, kwani itaanza dakika yoyote ile.
-Mkewe akachukia na kumpigia kelele, akasema.
- Yaani huna kazi nyingine ya kufanya jioni hii, zaidi ya kukaa na kuangalia TV na kunywa bia?
Wewe huna lolote isipokuwa ni mvivu, mwanaharamu mkubwa.......
Yule bwana akapumua na kusema:-
-Sasa imeanza.......
Je wewe pia unajiuliza kama mimi ni nini kilichoanza?

Wednesday, March 28, 2012

PIKINIKI MAKABURINI! Je ukimchungulia mtu mzima Utapofuka macho?

HAYA JAMANI NI ILI JUMATANO YETU YA KIPENGELE CHA MARUDIO MBALIMBALI NA PIA NI JUMATANO YA MWISHO YA MWEZI HUU. MADA KATIKA PITAPITA ZANGU NIKAKUTANO NA MADA HII SIO KWINGINE TENA BALI NIMEIPATA MAWAZONI KARIBUNI SANA.
Naamini mila na desturi zetu wabongo bado zina nguvu sana ingawa watu wanadai hizi ni zama ya bongo fleva. Naamini kuwa katika shule zetu za jadi mbinu mbalimbali zilitumika kuwezesha mambo fulani katika jamii kwenda shwari na kulindwa kwa nguvu zote na jamii. Mimi ni mchanganyiko wa Kipare na Kijita na katika makabila yote haya mawili njia za kuelimisha zilitumia mbinu nyingi ikiwa pia na vitisho. Mfano kwa Wapare maswala ya kufundishwa kuwa mwanamume wa shoka yaliendana na vitisho na maumivu. Kama wewe ni mwanamume basi lazima uweze kuvumilia maumivu .Nadhani kwa walioenda jando watakumbuka! Kulikuwa mpaka kuna simba wamsituni akumezaye ukishindwa kufanikisha mambo fulani ya kidume. Hii maana yake ulikuwa unauawa ingawa ilidaiwa umeliwa na Simba. Sasa njia hizi za kutufundisha heshima , maisha na hekima nyingine nyingi zikajakuuawa na wakoloni na wengine walioleta tamaduni mpya. Basi unaweza kudhani kwa sababu Wakoloni waliua shule za jadi basi na baadhi ya mambo tuliyokuwa tunatishiana yamekwisha!Utadhani mpaka sasa tumeweza kuelewa au hata kujiuliza ni kwanini mambo mengine yalitishalo kabila moja, hayalitishi jingine hata hivi sasa baada ya makabila ya Tanzania kuchanganyika na kutawanyika katika mikoa mbalimbali . Jibu bado tukopalepale. Tunaamini wachawi wanapaa na ungo ingawa hata kushuhudia hatuja shuhudia. Tunaamini kibibi fulani kichawi kwasababu macho yake mekundu bila kushuhudia aliyelogwa. Tuna chanja na kuvaa hirizi kibao bila ya uhakika hata wa ni nini hasa tunakiogopa. Sitaki kukataa kuwa hakuna uchawi kwa sababu hili ni jambo lililorekodiwa miaka mingi tu na vitabu vingi vimelizungumzia. Lakini mimi ninachoamini ni kwamba uchawi mkubwa ni hofu ya kibinadamu itokanayo naupungufu wa kibinadamu wakutokujua. Na upungufu huu kwa bahati mbaya hauna dawa. Upungufu huu umefanya wengine waabudu miti ili kuujazia, wengine Yesu, na Wengine Mtume Mohamedi. Tatizo jingine la upungufu huu uko kama njaa, kila siku unahitaji kupewa chakula ilikujazilizia pengo la upungufu wa kibinadamu ilikupata uhaueni. Mimi naamini pamoja na kuwepo wachawi, moto wa ahera na mambo yote hayo, lakini upungufu wa kibinadamu wenyewe hulenga binadamu kitofauti kutokana na binadamu mwenyewe alivyo na mazingira yake katika kumuelekeza binadamu huyu kuamini nini kinampa ujazo na uhaueni. Basi utakuta huku wanaogopa makaburi, kule wanaogopa mbuyu na hata wengine kukimbia vifuu vya nazi kutokana na mazingira yao. Basi unaweza ukakuta kutokana na mlengwa hirizi ikajazia na kuziba hofu hiyo, dini au hata kujinyonga. Naamini ubongo wa binadamu unanguvu kiasi kwamba hufanyia kazi hofu za binadamu na kuzipa uhai na uhalisi.Na naamini asilimia kubwa ya wajulikanao kama wachawi, waganga wa kienyeji au hata uchawi wenyewe haukuthibitika ingawa una uhalisi. Halafu si kweli zote ni zakufundisha maana nyingine ni zakutishana kwa madhumuni yakutishana tu.Na nyingi za mila na desturi hizi hatakama zilikuwa zinafundisha zamani hazina mchango mkubwa sasa hivi katika kuifundisha jamii ya leo.Na kama kuna sababu zakuzikubali hizi dini za kuletwa moja ni kwamba kwa sasa ndio zimeshikilia ukanda katika kuipa jamii muelekeo, ingawa hata kwa hili sina uhakika zitaweza jukumu hili mpaka lini kama jamii haifumbui macho nakuelewa mchango wake bila ya kukariri na kufuata kiulimbukeni. Lakini hizi mila za kutishana kwa dhumuni la kufundisha kitu haziko afrika pekee. Na rafiki yangu Myahudi alikuwa anatishwa na wazazi wake asiweke Tattoo kwa sababu hata weza kuzikwa kiyahudi akiwa na tattoo, kitu ambacho baadaye akagundua hakina ukweli. Nakumbuka pia nilipotembelea Russia mitaa ya Viborg nishawahi kuwatisha wenyeji wangu kwa kuwa nilipiga mluzi ndani ya nyumba na wao waliamini kabisa kwa kupiga mluzi ndani ya nyumba unaleta bomba la balaa. Kitu ambacho mimi siamini, kwani mimi nilifundishwa usipige miluzi porini. Hivyo hizi mila na desturi ambazo zina mambo haya ya kutishana haziko Afrika tu. Duh !Unakumbuka kitabu kiuzacho kuliko vyote siku hizi cha Harry Potter kinastori gani za kichawi?Sasa ngojea nikupe stori fupi kuhusu uoga wangu wa makaburi.Nakumbuka tokea utotoni nilizoea kusikia habari za kutisha kuhusu maeneo ya makaburini. Nakumbuka kunakipindi nilikuwa nang'ang'ania kutokwenda kulala mapema ilikuendelea kusikiliza stori za wakubwa, basi ilikutaka kunifanya niondoke wanaanza kusimulia stori za kutishatisha. Sehemu kubwa za stori hizi zilikuwa zinalenga maswala ya majini mashetanishetani na maeneo ya stori yanakuwa makaburini. Basi nisitake kukuongopea mara nyingi ilivyokuwa inaingia giza nilikuwa natishika kukatizia njia yoyote inayokatizia makaburini.Kilichokuja kunishinda ni pale nilipokuwa natembelea Upareni kwani kule ni kawaida kabisa marehemu kuzikwa katika eneo la nyumba. Sasa kutokana na kukulia mikoani ambako kunatamaduni za kuogopa maeneo ya makaruri ilinichukua muda kidogo kuzoe mpaka kuona ni kawaida.Kama nakumbuka vizuri Wachaga nao hawana uoga sana na makaburi hivyo nadhani kwa waogopa makaburi wanaweza kupata taabu sana uchagani na Upareni pia. Lakini akipata tabu Uchagani atatokwa na jasho akikatiza katika anga kama za Ufini ambako kuna mpaka siku katika mitaa ya krismasi ambapo makaburini ndio pakwenda sio kikilio bali kimatembezi. Mila na desturi zetu nyingi ni nzuri lakini hatuzisomi na kuzielewa sasa hivi tunapo ingia katika tamaduni za bongo fleva. Tatizo linalojitokeza ni kwamba mila nyingi nzuri zitapotea, halafu na zipo mila na desturi nyingi zisizo na manufaa sana kwetu tutaendelea kuzitunza. Bahati mbaya mila ambazo zitatunzika ni zile tuziogopazo! Je ukimchungulia mtu mzima utapofuka macho?Je , utakwenda pikiniki makaburini?

PANAPO MAJALIWA TUTAONANA JUMATANO NYINGINE TENA. KILA LA KHERI!!!!

Tuesday, March 27, 2012

RANGI NA UZURI WAKE!!!!!!!!!

Nimependa mchanganyiko huo wa rangi … kwa kutazama pia kuvaa … . ni ubunifu mzuri sana. Hivi hizi ni rangi za taifa fulani au ni kwamba imetokea tu mbunifu akabuni namna hiyo?
Pamoja Daima...

Monday, March 26, 2012

TANZANIA YETU NA UZURI WAKE...MBUGA ZA WANYAMA!!!


NAWATAKIENI WOTE JIONI NJEMA SANA AU SIJUI MCHANA MAANA MASAA YAMETOFAUTIANA KILA NCHI.... Je kweli hakuna tu haja ya kujivuna hapa??

UJUMBE WA JUMATATU YA LEO!! MATATIZO KATIKA MAISHA!!

Ulijua kwamba:- Matatizo ni mazuri kwa vile hukufanya uwe mbunifu. Pili huwezi kukwepa matatizo kama unaishi hapa duniani. Matatizo ni sehemu ya maisha, tatizo kubwa linakuja jinsi unavyoliona tatizo, ukiliangalia tatizo tofauti basi tatizo huwa kubwa zaidi na ukiliangalia tatizo kama sehemu ya ufumbuzi au ubunifu au hamasa ya kufanikiwa na kupiga hatua basi ukipata tatizo badala ya kulalamika na kuona unaonewa utachangamka na kuanza kushughulikia. Nahisi matatizo yangu ninayokutana nayo ni makubwa kuliko yako ila naamini yangu ni yangu na nikiyashinda tu nitakuwa mbali zaidi na nitakuwa mtu wa mafanikio.Mara nyingi matatizo nayo huwa yanazalisha stress sana kwa hiyo inabidi daima uwe imara kuyatatua lakini siyo matatizo ambayo yanakufanya uumie huku wanaokuumiza hawana chembe ya haki ya kukuumiza angalia usianguke.
Tumalizie na wimbo huu usemao MATATIZO NIMEYAZOEA

JUMATATU NJEMA !!!!!!!

Sunday, March 25, 2012

LEO NI JUMAPILI YA TANO YA KWARESMA!!


Napenda kwatakieni wote jumapili njema na upendo wenye baraka za Mungu utawale nyumbani mwenu!!!JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGU.

Friday, March 23, 2012

LEO NI KUMBUKUMBU YA NDUGU YETU ASIFIWE NGONYANI!!!

Asifiwe alizaliwa 26/11/1989 na alitutoka 23/3/2011

Ni mwaka mmoja sasa tangu mpendwa wetu Asifiwe atutoke.Umetuacha na majonzi na maumivu moyoni mwetu.

Tunakukumbuka sana uwepo wako. Tukiamini Mungu angekuacha japo kwa miAka michache. Midomo yetu haiwezi kuelezea jinsi tulivyokupenda.

Lakini Mwenyezi Mungu anajua ni jinsi gani tulikupenda/tunakupenda. Na jinsi gani tunakukumbuka. Mapenzi yako kwetu pia wema wako ni baraka kubwa kwetu.

Unakumbukwa sana na sisi wanafamilia wote pamoja na ndugu wote na pia marafiki. Kimwili hauko nasi, bali kiroho uko nasi daima. MWENYEZI MUNGU AIPUMZISHE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI!! AMINA!!!

Thursday, March 22, 2012

UNALIKUMBUKA SHAIRI HILI?:- KAMA MNATAKA MALI

Karudi Baba mmoja, toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali
Wakataka na kauli, iwafae maishani.

Akatamka mgonjwa, ninaumwa kweli kweli
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali
oho naona yachinjwa, kifo kimenikabili,
kama mwataka kauli, semani niseme nini.

Yakawatoka kinywani,maneno yenye adili,
Baba yetu wa thamani,sisi tunataka mali,
Urith tunatamani,mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani.

Baba aliye kufani, akajibu lile swali,
Nina kufa maskini, baba yenu sina mali,
Neno moja lishikeni, kama mnataka mali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
Akili yetu nyembamba, haijajua methali,
Kama tunataka mali, tutapataje shambani.

Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
Haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali mtayapata shambani.

Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Fumbu wakatafakari, watoto wale wawili,
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili,
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali,
Tangu zile za mibuni, hata zitupazo wali,
Na mvua ikaja chini, wakona na dalili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Shamba wakapalilia, bila kupata ajali.
Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia, usemi wakakubali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakawanunua ngómbe, majike kwa mafahali,
Wakapata na vikombe, mavazi na baiskeli,
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali,
Walikiweka kibao, wakaandika kauili,
KAMA MNATAKA MALI, MTAYAPATA SHAMBANI.

Ahsante kaka Mjengwa kwa kunikumbusha shairi hili ni kweli mimi nizikumbuka beti zote na ilikuwa darasa la nne nikumbukavyo mimi. kulikumbuka Shairi ni kutokana na hapa.

Wednesday, March 21, 2012

UTAFITI: KUNYONYESHA HUZUIA KANSA YA MATITI KWA ASILIMIA 25-60

Tusiacha kunyonyesha vichanga wetu jamani


Mara nyingi nimekuwa najiuliza hivi kwa nini akina mama hapa niishipo hawapendi kunyonyesha watoto wao. Utakuta mtoto ana miezi mitatu amekwisha achishwa kunyonya. Anapewa hii mipira (kidanganyio) kutwa nzima kisa eti akima mama wanaogopa matiti yao yatakuwa kama "chapati"....kwa mimi wala sielewi kabisa . Ebu soma hii makala hapa chini.......
Ambayo nimeipata kutoka kwa kaka Matondo nikaona si mbaya kama tukijikumbusha na pengine kuna waliokosa kuisoma. SI WOTE TUNAKUMBUKA NI JUMATANO NI KIPENGELE CHA MARUDIO
----------------------------------------------------------------------------------------------
Mbali na ukweli kwamba kunyonyesha ndiyo chanzo cha lishe bora kabisa kwa mtoto, wanasayansi sasa wanadai kwamba kunyonyesha pia kunaweza kupunguza uwezekano wa mama kupata kansa ya matiti kwa asilimia 25 hadi 60.

Hizi ni habari njema kwa akina mama wa Afrika ambao kimsingi huchukulia kunyonyesha kama mojawapo ya wajibu wao baada ya kupata mtoto. Pengine hii inaweza kuwa ndiyo sababu iliyofanya saratani ya matiti isijidhihirishe sana Afrika.

Wasiwasi wangu ni juu ya kizazi kipya ambacho kinaiga mambo ya Kimagharibi kwa pupa. Nimeshasikia kwamba mabinti wengi sasa hawana hamu tena ya kunyonyesha vichanga vyao wakichelea kuharibu matiti na miili yao. Ukijumlisha na vitu vingine vinavyoingia Afrika vikiwemo vyakula vilivyolimwa "kisayansi", madawa na mabadiliko mazima ya mfumo wetu wa maisha, sitashangaa kama kansa itafumuka na kuwa ugonjwa wa kawaida tu muda si mrefu ujao. Hili likitokea, atakayefaidika bila shaka ni makampuni ya madawa ya nchi za Kimagharibi - na naamini kwamba hiki ndicho wanachotaka. Tuweni waangalifu na tuache mambo ya kuiga vitu kiholela bila kuelewa hasa kiini chake.Ukitaka kusoma zaidi gonga hapa. TUKUTANE TENA WAKATI MWINGINE!!!!!

Tuesday, March 20, 2012

PICHA ZA WIKI:- MWAKA JANA 2011 NILIPOKUWA NYUMBANI SONGEA/PERAMIHO/RUHUWIKO!!!!

..Ebu angalia bonge la mti hapa ni Peramiho wale walofika Peramiho kilimo cha mseto ...sijui nami naweza kunenepa /kuwa kama mti huu....

Au ngoja tumwangalia mdada akikagua shamba lake la ndizi au matunda kwa ujumla pia miti..ni mkulima pia mdada huyu:-)


UMEWAHI KUFIKIRI KUWA HAKUNA KITU KIBAYA KAMA KUPOTEZA MAWASILIANO NA RAFIKI, MPENZI, MUME/MKE AU LABDA NISEME JAMII KWA UJUMLA?

Basi mwenzenu yamenikuta nimempoteza rafiki yangu mpenzi . Namtafuta kwa kila hali na mali lakini simpati. Na jinsi ukimya uzidivyo nazidi kukosa raha. NAMPENDA SANA RAFIKI YANGU HUYU. KAMA UMESOMA UJUMBE HUU TAFADHALI NTAFUTE SITAKI KUKUPOTEZA.....Dada Yasinta nifanye nini ili rafiki yangu aongee tena nami?
-------------------------------------------------------------------------------------------------Ujumbe huu nimetumiwa na mdau ambaye ni msomaji wa Maisha na Mafanikio...nikaona niweke hapa ili mnisaidie ni ushauri gani kumpa mwenzetu.

Sunday, March 18, 2012

Neno La Leo: Mungu Hahusiki Na Umasikini Wako!

Ndugu zangu,
Matatizo yetu mengi yanatokana na sisi wenyewe. Wenzetu Ulaya na Marekani wanasema; “Time is Money”. Kwa tafsiri ya moja kwa moja, unamaanisha kwamba muda ni pesa. Lakini, tafsiri sahihi hapo ni umuhimu wa muda.
Kwamba muda ni kitu cha thamani sana. Na hakika, kwa mwanadamu, jinsi unavyoutumia muda wako hivi leo ni ishara tosha ya jinsi kesho yako itakavyokuwa.
Tumekuwa watu wa kulalamika sana. Na tumemwachia Mungu jukumu la kutukomboa kutoka kwenye umasikini wetu. Hapana, Mungu hausiki na umasikini wako. Jukumu la kwanza la kujikomboa kutoka kwenye umasikini ni lako mwenyewe. Na hakuna njia ya mkato, bali ni kufanya kazi, kufanya kazi na kufanya kazi. Achana na ndoto za kuamka na kuvuna mamilioni. Bila kufanya kazi!
Inakuwaje basi kwa mwanadamu mmoja awe na muda na mwingine asiwe nao?
Kuwa au kutokuwa na muda inatokana na mipangalio yako ya maisha. Binadamu unapaswa kuwa na bajeti ya muda wako. Ni jinsi unavyoutumia muda wako. Jinsi unavyopangilia mambo yako, ratiba zako na mengineyo.
Ukiwa na utaratibu huo, basi, waweza kabisa kuwa na muda wa kutosha kufanya mambo mengine mengi uyapendayo ikiwemo mapumziko, kuwa na muda na familia yako, kuwa na muda wa kujisomea na mengineyo.
Ndio, lililo muhimu ni kuwa na vipaumbele. Unapoandika orodha ya shughuli zako za siku, juma, mwezi na hata mwaka, basi weka kipaumbele katika mambo ambayo ni muhimu zaidi. Hayo yaweke juu kabisa katika orodha yako. Kipaumbele kinaweza kutokana na umuhimu wako binafsi kwa jambo fulani.
Usiwe mtu unayesukuma mambo mbele. Mtu mwenye hulka ya kuahirisha mambo. Linalowezekana kufanyika lifanye. Kauli za ’ hili nalifanya kesho’ au ’ namwachia Mungu,’ ni kauli za mtu aliyekata tamaa kwenye mapambano ya maisha.
Wahenga walinena; ’’Linalowezekana leo lisingoje kesho!’’ Hulka ya kusukumia mbele mambo ina tafsiri moja tu; kuwa unaongeza mzigo wa mambo ya kufanya. Huna unachokipunguza. Ni mwanzo wa kupatwa na msongo (stress). Ni mwanzo wa kuchanganyikiwa. Ndipo hapo utamwona mwanadamu mwenzako akitembea huku akiongea peke yake.
Ni muhimu pia kuwa na muda na marafiki. Naam, weka bajeti ya muda. Okoa muda upate muda wa ziada. Na baadhi ya marafiki zako waweza kuwa sababu ya matumizi mabaya ya muda wako. Ndio, marafiki wengine ni marafiki wa kukupotezea muda tu. Angalia, ni marafiki wa aina gani ulio nao.
Inasemwa, ukitaka kumfahamu mtu alivyo, basi, angalia aina ya marafiki zake. Kwa mfano kama una rafiki ambaye hazingatii muda, hana miadi ya uhakika, basi, huyo anaweza kuwa mzigo katika suala zima la matumizi ya muda.
Usiwe mtu mwenye kufuata mkumbo, eti kwa vile wengine hawazingatii muda, basi, na wewe unajifanya ni mtu usiyejali muda. Hapo utakuwa unajipoteza mwenyewe. Ni muhimu, hata unapokuwa na marafiki zako, uwe mbele katika kuhakikisha mnatumia muda wenu vizuri.
Uwe tayari na mipango kichwani hata kabla hujakutana na rafiki au marafiki zako. Kisha mshirikishe rafiki au marafiki zako katika mipango uliyoifikiria kwenye mambo ya kufanya. Na usiwe mtu mwenye kupanga mambo mia moja kwa wakati mmoja. Uwe na mipango miwili au mitatu ya kujadili na wenzako. Kesho ndio uje na mingine.
Ni bahati mbaya kwetu wanadamu, kuwa muda mwingi sana huwa tunaupoteza kutokana na kutopangilia vizuri mambo yetu. Upo umuhimu kwa mfano wa kupangilia shughuli zetu kutokana na sehemu za kijiografia.Kwa mfano, kama una shughuli ambazo zinahitajika kufanyika mjini, hakikisha kwamba unapokwenda mjini, unazikamilisha zote kwa wakati mmoja. Kwanini uende mjini zaidi ya mara nne kwa siku?
Naam, Mungu hahusiki na umasikini wako. Muda ni mali. Panga bajeti ya muda wako, sasa! Na hili ni Neno La Leo.
( Makala haya yamechapwa kwenye gazeti Mwananchi, leo Jumapili) NA MIMI NIMETUMIWA NA KAKA MJENGWA........

NI JUMAPILI YA NNE YA KWARESMA SASA: WOTE MUWE NA JUMAPILI NJEMA NA BARAKA ZA MWENYEZI MUNGU ZIWE KATIKA NYUMBA ZENU!!


Ni kipindi ambacho watu wahitaji kusameana na kuwa pamoja ...muwe na amani wote na baraka za mwenyezi Mungu ziwe kwenu. JUMAPILI NJEMA!!!

Saturday, March 17, 2012

MWONEKANO MPYA WA KAPULYA....

Hapa ilikuwa mwaka huu 2012/5/1 nilipopiga picha hii nikiwa nimesuka nywele za kimasai ......
...na hapa ni leo nimefumua zile nywele za kimasai na sasa nipo naturel /yaaani na nywele zangu nilizozaliwa nazo. Watoto wangu wameshangaa kwani nilifumua zile rasta minywele yangu ilikuwa mirefu si kawaida baada ya kuosha zikashiling/rudi na kuwa fupi...Yakajia maswali umenyoa mama?...ila wote wamependa mwonekano wangu mpya . Je wewe unayeangalia ni mwonekano upi unaupenda niendelee nao? JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE....NA KUMBUKENI WOTE MNAPENDWA :-)

Friday, March 16, 2012

UNAJUA KISA CHA WANGONI KUAMKIANA MONILE??

Ni hivi:- Kulikuwa na mzungu pale Peramiho aliyejenga lile kanisa. Na aliishi miaka mingi pale Peramiho. Mzungu huyo alikuwa na tabia ya kuamka asubuhi na kupita kuwatembelea watu majumbani mwao. Yaani kwa nia ya kuwajulia hali wazee na vijana. Yeye alipenda sana kutembea kwa mguu, toka Peramiho Hospitali mpaka njia panda ya kwenda Mbinga. Kijiji kimoja kiitwacho Lipokela. Na baadaye kurudi.
Sasa yeye kwa kuwa alikuwa hajui kiswahili na alitaka kujifunza. Basi alikuwa ana wasalimia ile GOOD MORNING!
Kwa mkato yaani MORNING na wale wazee wakawa wanamuuliza tukujibuje? Naye aliwaaambia mujibu MORNING. Basi wale akina BAMBU wakawa sasa ni kila mtu wakimuona asubuhi wanasema MONILE.... wanajibishana MINILEEE...Kisha wanamalizia TUWAONE....jibu lake ..YEOO..Yaani tumemwona leo mzungu ndiyoo.
Basi toka miaka hiyo mpaka leo WANGONI wanasalimiana hivyo. Ikiwa Asubuhi MONILE...MONILE ..TUWAONE BAMBU ...YEOOO
SIKU NJEMA NDUGU ZANGUNI!!!!

Thursday, March 15, 2012

KUNA ANAYEJUA NI NINI KUNAMSIBU DADA SUBI?

Ndugu zanguni wapendwa, nimepatwa na mstuko jana baada ya kusoma ujumbe wake ambao ni huu hapa. Je? kuna anayejua ndugu yetu Subi ni nini kinamsibu/sumbua..?

Uganda yaanza 'kutibu watoto wanaosinzia'

Watoto Uganda, wanakumbwa na,

ugonjwa usiojulikana chanzo wa 'kusinzia'

Uganda imefungua vituo vya afya vya kwanza maalum kwa kusaidia maelfu ya wattoto ambao wana dalili za ugonjwa ambao haujajulikana chanzo chake wa 'kusinzia.’
Vituo hivyo vilivyo kaskazini mwa nchi, ambako ugonjwa huo umeenea, vinakusudiwa kudhibiti dalili mbaya za ugonjwa huo.
Chanzo cha ugonjwa huo hakijajulikana lakini unawapata watoto pekee, wanaoshambuliwa na dalili za kudumaa kiakili na kimwili na kusinzia.
Kuna taarifa za ugonjwa huo kuwa upo nchi za Sudan Kusini na Tanzania.
Kudhibiti dalili
Zaidi ya watoto 200 wenye ugonjwa huo walijitokeza Jumatatu kwa ajili ya matibabu katika vituo hivyo katika wilaya za Kitgum, Pader na Ramor, Kamishna wa Huduma za afya nchini Uganda Dr Anthony Mbonye aliiambia BBC.
Wafanyakazi wa afya hawawezi kutoa tiba yoyote maalum mpaka madaktari wagundue chanzo halisi cha ugonjwa huo –lakini Dr Mbonye anasema wamewapa mafunzo kusaidia maisha ya watoto kwa kudhibiti dalili za fadhaa kwenye mfumo wa neva.
Dawa za kupambana na kifafa zimekuwa na nguvu kutibu wagonjwa wa kusinzia, kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani.
Ugonjwa wa kusinzia unasababisha watoto kufaidhika na kutetemeka na hatimaye kufa.
Mwandishi wa BBC mjini Kampala Ignatius Bahizi anasema mbunge wa jimbo hilo Beatrice Anyor, amekuwa akiongoza kampeni kwa serikali kushughulikia zaidi tatizo hilo ambalo anasema limesababisha wasiwasi mkubwa maeneo ya vijijini.
Wizara ya Afya nchini Uganda imerekodi matukio 3,000 ya ugonjwa huo na karibu vifo 200 vimetokea tangu mwaka 2010.

NIMELIPENDA GAUNI HILI MNO....

.......ebu angalia hizo rangi na jinsi lilivyorembwa, nimelipenda mno . Swali sijui nami nitapendaza kama lilivyompendeza huyu dada?:-)

Wednesday, March 14, 2012

KUVAA SHANGA... NI UREMBO AU?

Ndiyo ndugu zanguni ni JUMATANO TENA na ni kile kipengele chetu cha MARUDIO..katika pita pita nimekutana na mada hii nikaona si mbaya tukirudia kujadili tena . Nimeipata hapa.
watu huvaa shanga kwa maana nyingi naamini, hivi shanga zina maana ngapi? najua maana za nyekundu, nyeusi na nyeupe je nihizo tu ama na rangi nyengine pia zinamaana tofauti? na wanaume hupendelea nini kwenye shanga? na wanawake waova je hujisikiaje kuwa nazo..


kuna wakati nilikuwa navaa shanga kwenye kiuno sio kwamba nilipenda ila mpenzi wangu kipindi hicho ndio alikuwa anapenda nivae akisema anapoziona anasisimuka lakini baada ya kuachana naye nikaachana nazo kwakuwa sikuwa nazipenda kuvaa bali kumridhisha tu..

kitu cha kushangaza ni kwamba kuna rafiki yangu anaolewa karibuni mchumba wake amemletea shanga avae, anasema yeye anapenda kumuona mpenzi wake akiwa amevaa ndipo nilipo mshauri azivae baada ya kumpa story yangu hapo juu..

wanaume kuna raha gani ambayo mnaipata pindi wapenzi wenu wanapo vaa shanga????na je ni wanaume wa makibala fulani ama wote kwa ujumla? maana rafiki yangu huyo mchumba wake mkuria na ndicho kilicho zidi nishangaza...na mwanaume aliyenifanya mimi nivae ni mmakonde ndio inazidi kunichanganya..

sio vibaya nikufahamishana tu ili tujuwe kama tutaendelea kuzivaa ama tuziweke kapuni.....

TUTAONANA TENA JUMATANO IJAYO KATIKA KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO!!!

Tuesday, March 13, 2012

UMEWAHI KUJIULIZA HIVI.....

Kwanini Nguruwe Hana Pembe?

Monday, March 12, 2012

JUMATATU HII TUANZA HIVI:- MATUNDA NA VIUNGO!!


Nadhani wote mnajua hapa ni mti wa malimao angalia jinsi yalivyo yaani nashindwa hata kuelezea hapa ni mwaka jana wakati nilipokuwa nyumbani na ni Matema beach kwa rafiki yetu....

....na hapa bila kiungo hiki kachumbali hainogi ni pilipili kichaa ...swali la kizushi hivi ukila hizi unakuwa kichaa kweli? na kwanini zinaitwa pilipili kicha?..


Bado tupo Matema Beach bonge la mkungu wa ndizi mpaka nikatamani nipata na unajua nini? niliupata:-)
..Hapa ni Mdunduwalo mti wa machungwa ...naipenda Afrika yangu kwa kweli matunda na chakula ni kutoka tu nje na kuchukua....JUMATATU NJEMA JAMANI ILA MWENZENU LEO NIMETAMANI kwelikweli nyumbani...
Sunday, March 11, 2012

SALAMU ZA JUMAPILI YA LEO : MASIKINI NA PESA YA KUOKOTA!!!

MASIKINI MMOJA ALIKWENDA MAPORINI KUTAFUTA RIZIKI YA KAWAIDA KAMA UJUAVYO KULE VIJIJINI KWETU RUWILA. BASI ALIPOFIKA KATIKA KICHAKA KIMOJAWAPO ALIKUTA KITU KIMEFUKIWA CHINI KATKA KUFUKUA BASI ALIKUTA SANDUKU LA CHUMA LIMEJAA PESA YAANI KAMA NI DOLA BASI NI ZILE DOLA MIA MIA TUPU ,KAMA NI ZILE ZA KWAETU BASI NI WALE WEKUNDU WA MSIMBAZI WATUPU,
BASI YULE MTU ALIKUWA NA IMANI SANA YA KUMWAMINI MUNGU. HIVYO ALIPOZIONA ZILE PESA AKAMWAMBIA MUNGU ,,, HIVI WEWE BWANA MUNGU KWANINI UNANIPIMA MIMI IMANI YANGU KIASI HIKI ? SASA NAKUAMBIA MIMI SICHUKUWI PESA HII HATA CENTI. KAMA NI SHIDA WEWE UNAJUWA NIIPATAVYO. BASI KAMA UMEPANGA KUNIPATIA PESA HII MIMI. UTANILETEA PESA HII NYUMBANI KWANGU. BASI YULE BWANA ALIONDOKA MPAKA KWAKE ,,NA AKAMWELEZEA MKE WAKE YALIYOMKUTA KULE MAPORINI. DUH! MKE WAKE AKAMWAMBIA WEWE MUME WANGU NDIO MJINGA KABISA. SASA KAMA ULIONA NI MZIGO MKUBWA KWANINI HUKUCHUKUA JAPO KIDOGO? YEYE ALIMJIBU KUWA ZILE NI PESA ZANGU KAMA MUNGU ALIIPANGA ZIWE ZANGU, BASI ATAZILETA HAPA NYUMBANI KWANGU.BASA WAKATI WANA BISHANA NA MKEWE AKASIKIA SEBULENI KITU KIMEANGUKA KWA KISHINDO KIKUBWA ,AKAMWAMBIA HAYA PESA IMEKUJA MKEWE AKACHEKA KWA KEBEHI .. YAANI UMEZIACHA PESA HUKO NANI AKULETEE? AKASEMA, MUNGU NIMEMWAMBIA ATAZILETA TUU ,KWELI BWANA KUMBE WATU WAWILI WALIPITA PALE WAKAZIONA WAKAWA WAMECHUKUZANA ,WAKAWA WANA PITA NYUMBANI KWA YULE BWANA KATIKA KICHOCHORO BASI WALIPOFIKA KATIKATI TA NYUMBA ILE KUANGALIA MBELE WAKAONA POLISI WAKATAKA KUGEUKA WALIKOTOKA WAKAONA POLISI DUH! WAKASEMEZANA BWANA HII PESA YA SERIKALI ,,, SASA ,,TUFANYEJE? WAKASEMA HII PESA TURUSHIE KWENYE NYUMBA YA HUYU MASIKINI KAMA KUKAMATWA AKAMATWE YEYE ,, BASI NDIPO WAKAIRUSHIA MLE NDANI NA NDIPO MASIKINI ALIPOSEMA PESA AMELETEWA KUMBE BWANA WALE WALIKUWA MALAIKA SI POLISI MASIKINI AKAWA TAJIRI KWA IMANI YAKE KWA MWENYEZI MUNGU ,,,,,,, TUNAJIFUNDISHA NINI???
Hii nimetumiwa na ndugu yangu kaka CHE JIAH. NA SIKUTAKA KUWA MCHOYO.
Labda dada Rose Muhando amalizie na wimbo huu IMANI.............


JUMAPILI NJEMA KWA WOTE !!!!!!!!!!!!!

Saturday, March 10, 2012

UJUMBE WA LEO:- NI VYEMA KUIJUA SIRI HII!

Huu ndio ukweli, ukitaka kupata furaha ya maisha

1.Sema kweli

2.Furahia maisha na furahisha wengine, Penda kwa dhati bila unafiki na bila masharti

3.Jiamini

4.Chukia kusema uongo

5.Tetea unachokipenda na kukiamini

6.Ukiwa dhaifu wa kukumbwa na mawazo potofu usichukie kumbuka mawazo potofu yameumbiwa na Binadamu

7.Jitahidi kufikiri na kuwaza vyema ili uzidi kujiamini, kujipenda na na kuwapenda wengine. Yote yanawezekana.

Kumbuka usemi huu “ukivuliwa nguo chutama. Ukikosea tubu haraka.Wastara huwa haumbuki……………

JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE....NA MNAPENDWA SANA!!

Friday, March 9, 2012

NGOMA ZA ASILI NI NZURI JAMANI HAYA EBU TUANZA MWISHO WA WIKI NA HII!!!!


Hapa ni ngoma ya mganda hii nimecheza sana wakati nipo shuleni ila ni maalufu kwa wavulana/wanaume.

Au labda tuwasalimie ndugu zetu huko Botswana ebu sikiliza hizo sauti hata kama huelewi utainuka tu na kucheza.....


Kama nilivyosema hata kama huelewi utacheza au utasikiliza tu NAIPENDA AFRIKA NA TAMADUNI ZAKE..
Ngoma nyingine za asili nazozitamani ni Muhambo, Beta, Chomanga, Lindeko, Madogili, Limbamiza nk. HAYA JAMANI IJUMAA NJEMA.....

Thursday, March 8, 2012

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI :- UJUMBE!!!

Mwanamke ni kama jua ambalo bila wao sayari ingekuwa bila watu.
Unapotoa, ni kama kutoa pumzi ya uhai.
Na kuzaliwa kwa mtoto, aliye tumboni mwake.
Wanawake ni watu wa kipee, kama watu wangejkuwa wema wangewapa wanawake thamani zaidi.
Wanaume/watu hawajui vipi kujivunia wanawake na ndio sababu wanawake hawasikilizwi hata kama wana la kusema.
Ba watu wanajifanya vipofu ili kuweza kurahisisha ushahidi wao katika neema ya kutambua uzuri wa wanawake.
HONGERA WANAWAKE WOTE KATIKA DUNIA HII. PIA TUSIWASAHAU WANAUME KWANI BILA WAO UWEPO WETU HAUNGEKUWEPO.

Wednesday, March 7, 2012

DADA SAIDA KAROLI NA UJUMBE WAKE ...MAPENZI KIZUNGUZUNGU:-(


Wimbo ingawa mwanzoni unaibwa kwa KIHAYA (nadhani) lakini nashukuru mwishoni amefafanua....ni maalumu kwa wapendanao wakiwa katika myumbisho....Jinsi nilivyousikiliza maneno yake ni kweli kabisa kama upo katika hali hii wimbo huu unagusa na kuumiza ila pia mzuri kucheza. Nami UJUMBE WANGU KWA WAPENDWA WANGU NI KWAMBA TUPENDANE NA PALE TUNAPOPISHANA TUSAMEHEANE/TUWE WEPESI KUSAHAU YA KALE NA KUANZA MAPYA. KILA MTU ANASTAHILI NAFASI YA PILI. SIKU NJEMA KWA WOTE!!! KAPULYA

Nikanusurika kwenda jela, lakini kikaja kisirani kingine…………

Ni JUMATANO TENA NA NI KILE KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO LEO NIMEKUTANA NA HABARI HII NIMEIPENDA NIMEONA NIWASHIRIKISHE. Nimeipata hapa
------------------------------------------------------------------------------------------------
Ilikuwa ni mwaka 1994 wakati nilipoingia kwenye kasheshe kubwa ambayo nusura tu inipeleke jela. Nikiwa ndio nina mwaka wa pili tangu kuanza kazi, nilimpachika binti mmoja mimba. Alikuwa ni binti wa shule akisoma darasa la sita wakati ule. Mwili wake ulikuwa mkubwa, kiasi kwamba, ungeambiwa yuko kidato cha nne usingebisha, lakini alikuwa bado mdogo kwa umri.Baada ya kumpachika mimba, mjombake ambaye ndiye aliyekuwa akiishi naye, alilifungia kibwebwe suala lile, akitaka nipelekwe mahakamani. Ndugu zangu na jamaa zangu walijitahidi kwa kadiri walivyoweza kuzuia jambo lile kufikishwa mahakamani. Mjomba wa binti alikubali, lakini kwa sharti la mimi kumwoa mpwa wake, mara moja. Nilikubali haraka kufanya hivyo, kwani nilishauona mlango wa Segerea ukiwa wazi mbele yangu. Nilimwoa binti yule kwa ndoa ya ‘mkeka.’ Wazazi wake hawakuwepo, kwani wanaishi Songea vijijini.Mwezi huo huo nililazimika kwenda mkoani Mbeya kikazi, ambapo nilitakiwa kuishi kwa miezi mitatu kwa ajili ya kazi ya mkataba ambayo kampuni yetu iliipata. Nilipokuwa Mbeya, nilipata mwanamke ambaye alionekana kuwa na adabu zile za kijijini kabisa. Huyu nilimpata hospitalini, ambako nilienda kutibiwa Malaria, wiki ya tatu tangu kufika pale Mbeya.Sijui tulizoeana vipi, lakini alikuja kuwa rafiki yangu. Alikuwa ni mwenyeji wa Mkoani Ruvuma na pale Mbeya alikuwa amekuja kumuuguza kaka yake, ambaye alilazwa hospitali ya rufaa Mbeya. Nilimpenda kwa kweli, hasa nidhamu yake na hekima. Kiumri alinizidi miaka minne. Mimi nilikuwa na miaka 29 wakati huo na yeye 33. Lakini kwa kutazama, mtu angedhani mimi ndiye nilikuwa mkubwa. Niliishi naye kama mke wangu, hadi miezi mitatu ikaisha, nilirudi Dar nikimwacha bado anauguza mgonjwa wake. Wiki mbili baadae tangu nirudi Dar tuliletewa taarifa kwamba baba wa mke wangu amefariki dunia. Tuliamua kusafiri kwenda kwenye mazishi Songea, wakati huo mimba ya mke wangu ilikuwa imetimiza miezi sita. Tuliondoka mimi, yeye, na ndugu zake wawili na ndugu yangu mmoja. Tulifika kijijini kwao jioni, ambapo tulikuta mazishi yakiendelea, tulienda makaburini tukimwacha mke wangu nyumbani kutokana na hali yake. Tulipofika makaburini ilikuwa ndiyo zamu ya kuweka mashada ya maua kaburini.Ilikuwa kama ndoton Fulani, kwani nilimwona yule hawara yangu wa Mbeya akiweka shada la maua na alitajwa kama mke wa marehemu. Nilihisi kama nataka kupoteza fahamu. Nilijikaza, ingawa nilikuwa natoka sana jasho. Baada ya mazishi tulirudi nyumbani, ambapo ilibidi nitambulishwe kwa mzazi wa mke wangu na ndugu zake. Nilitambulishwa kwanza kwa mama mkwe ambaye kule Mbeya alikuwa ni hawara yangu. Kila mmoja kati yetu alijikaza ili isifahamike kinachoendelea. Lakini, hiyo haikudumu, kwani bomu likalipuka sawia. Mama mkwe wangu alilazimika kusema kwa wazazi wake, ati akiogopa mkosi utokanao na jambo kama hilo. Ilibidi siku ya nne baada ya msiba tufanyiwe tambiko la kiasili kuondoa laana. Nataka nikwambie katika maisha yangu sijawahi kukabiliwa na mtihani mgumu kama ule. Ninaye bado mke wangu na tumesahau yaliyopita. Mama mkwe hajawahi kuja kwetu, ingawa sisi tunaenda na kukaa siku chache kwake, kila mwaka.TUTAONANA TENA JUMATANO IJAYO PANAPO MAJALIWA!!!!!

Tuesday, March 6, 2012

J's JOY: Mavazi ya Kiafrika. Tujivunie. Tuunge mkono!!!!!

Ladies and Gentlemen,
I would like to take this great opportunity to introduce you to my niece, Karungi Mukurasi who has a renown business in Dar for making nguo za wakina mama na mashati ya wakina baba and some very interesting stylish African suits for men.
She is the one in the photos in the attachment.
From the time she was born she showed artistic proficiency and when school was done, she embarked into this voyage which has brought her to the heights of the design of premier African dressing. She gets her materials from West Africa where the best fabrics are woven and has dress-makers to her designs both in West Africa and in Tanzania.
Her dresses have been worn by prominent women in Tanzania and some international circles, as well as some shirts which some Wabunge have found very fashionable as they mingle in public circles.
Just as the advertisement on Mwananchi Newspaper shows (photo above, click to enlarge), these are African dresses with an African style which eclipse what you may see at a Hollywood movie premier or the Oscar's red carpet runway.
Please feel free to contact her for any additional info, specially for you who are abroad and would like to show the international community that African dressing is second to none!
Her email address is: kmukurasi@hotmail.com or k_mukurasi@yahoo.com Duka lipo Kinondoni Road, Kinondoni Muslim, Duka namba 37, jina la duka ni J's JOY. Namba ya simu ni +255 784 95 95 51
We hope to have a website soon!
Thanks,
Ben K.

LEO NIMEAMKA NA HILI SWALI AMBALO NAONA KILA NIKIJIULIZA SIPATI JIBU:- MIRATHI/URITHI

Kwanini watoto wa kiume hupewa mali nyingi na vitu muhimu kama vile ardhi na nyumba wakati watoto wa kike hunyimwa?
Nimewahi kuwasikia watu wengi wanadai kwamba sababu ya kutoa urithi kwa watoto wa kiume ni sababu wao hushika nafasi ya baba(marehemu) na kwamba ni HASARA ikiwa watoto wa kike wakirithi kwa vile wao huolewa na kuambatana na ukoo mwingine. Wanaona ya kwamba kuna hatari urithi wake kwenda kwa mumewe. Je huu ni uungwana kweli? NAOMBA TUJADILI KWA PAMOJA.....

Monday, March 5, 2012

NINGEPATA MLO KAMA HUU JIONI HII INGEKUWA RAHA ...


Ndizi za kuchoma , ukipata na kachumbali hapa mambo si mabaya nazimezea mate kweli hapa nilipo...au
sijui nikipata hawa senene ila sijawahi kula sijui ni watamu kama kumbikumbi au?
Picha kutoka kwa mwenyekiti Mjengwa.
JE? HAPA BORA ELIMU AU ELIMU BORA?

Picha hii imenirudisha mpaka enzi nipo shule ya msingi. Naweza kusema mie nilikuwa na bahati kwa vile baba yangu alikuwa mwalimu, tulikuwa tukiishi nyumba za shule ambazo zilikuwa karibu sana na shule. Lakini kulikuwa na wanafunzi walikuwa wakiishi mbali sana, na mwanzo wengi walikuwa wakishinda na njaa. Ila baadaye ndo wakagundua mtindo huu ya kwamba walikuwa wakichukua mboga na unga na shule ilijenga jiko wakawa wanapika pale shuleni. Ila ilikuwa kazi yao kuangalia kuna kuni maji na kadhalika.
Ama kweli maisha ni kujitegemea nikawa najisemea mwenyewe!!! Halafu nikawa najiuliza kweli hawa wanafunzi watasoma kweli au watakuwa wanafikiria jinsi ya kuanza kupika? halafu pia kusoma bila kula nako si vizuri.....maswali mengiiiiiiii....tujadili pamoja...

Sunday, March 4, 2012

UJUMBE WA JUMAPILI HII YA LEO NI HUU

Unapotafakari mema ya Mungu ya leo:-
WASAMEHE WALIOKUKOSEA,
WAKUMBUKE WALIOKUSAHAU na UILINDE AMANI YA MOYO ISIPOTEE.
Kwani utakuwa na furaha daima!!!
JUMAPILI NJEMA KWA WOTE NA MWENYEZI MUNGU AWE NANYI!!!

Saturday, March 3, 2012

KUPENDA KUNAWEZA KULETA MAWAZO MENGI!!!


MUWE NA JUMAMOSI NJEMA WOTE hata kama tutakuwa na mawazo sana tujitahidi kumtafuta rafiki ili kupoteza mawazo ili zisiwe pombe nyingi.

Friday, March 2, 2012

NIMELIPENDA SHATI HILI ALILOVAA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE

Nimelipenda sana hili shati ningemfahamu alishona au chora ningemtafuta safi sana...........Limeonyesha rangi zote za BENDERA TAIFA YA TANZANIA ingawa kwa mtindo wake wa kipekee..Nimelipenda sana..KILA LA KHERI JAMANI...

IJUMAA NJEMA KWA WIMBO HUU!! ZILIPENDWA NI TAMU!!


Ukiwa katika maumivu ya kupenda huu wimbo unaweza kupunguza maumivu au kuongeza...Nimeusikiliza jana zaidi ya mara kumi....Nangoja nini duniani bila kuwa na wewe mwenye shingo ya upanga....aahh naacha endeleeni nanyi pia.
IJUMAA NJEMA SANA!!!

Thursday, March 1, 2012

TAFAKARI YA LEO:-MILA NA DESTURI ZETU!

Nimekuwa nikiwaza jambo hili tangu nilipoanza kupata akili....Ni swali ambalo nimekuwa nimewauliza watu wengi nao hawajaweza kunijibu kwanini. Na leo nimeamka na naliona linazunguka kichwani mwangu na nimeshindwa kuacha kuuliza hapa kibarazani.
Ni hivi:- Hivi kwa nini msichana asimwombe kijana ampendaye kuwa anataka waoane? Najua ni mila na desturi zetu za kale kwamba ni mvulana/kijana /mwanaume afanye hivi. Je msichana/binti /mwanamke akifanya hivi kwa mvulana/kijana/mwanamume anayempenda itakuwa si sawa?