Wednesday, March 7, 2012

Nikanusurika kwenda jela, lakini kikaja kisirani kingine…………

Ni JUMATANO TENA NA NI KILE KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO LEO NIMEKUTANA NA HABARI HII NIMEIPENDA NIMEONA NIWASHIRIKISHE. Nimeipata hapa
------------------------------------------------------------------------------------------------
Ilikuwa ni mwaka 1994 wakati nilipoingia kwenye kasheshe kubwa ambayo nusura tu inipeleke jela. Nikiwa ndio nina mwaka wa pili tangu kuanza kazi, nilimpachika binti mmoja mimba. Alikuwa ni binti wa shule akisoma darasa la sita wakati ule. Mwili wake ulikuwa mkubwa, kiasi kwamba, ungeambiwa yuko kidato cha nne usingebisha, lakini alikuwa bado mdogo kwa umri.Baada ya kumpachika mimba, mjombake ambaye ndiye aliyekuwa akiishi naye, alilifungia kibwebwe suala lile, akitaka nipelekwe mahakamani. Ndugu zangu na jamaa zangu walijitahidi kwa kadiri walivyoweza kuzuia jambo lile kufikishwa mahakamani. Mjomba wa binti alikubali, lakini kwa sharti la mimi kumwoa mpwa wake, mara moja. Nilikubali haraka kufanya hivyo, kwani nilishauona mlango wa Segerea ukiwa wazi mbele yangu. Nilimwoa binti yule kwa ndoa ya ‘mkeka.’ Wazazi wake hawakuwepo, kwani wanaishi Songea vijijini.Mwezi huo huo nililazimika kwenda mkoani Mbeya kikazi, ambapo nilitakiwa kuishi kwa miezi mitatu kwa ajili ya kazi ya mkataba ambayo kampuni yetu iliipata. Nilipokuwa Mbeya, nilipata mwanamke ambaye alionekana kuwa na adabu zile za kijijini kabisa. Huyu nilimpata hospitalini, ambako nilienda kutibiwa Malaria, wiki ya tatu tangu kufika pale Mbeya.Sijui tulizoeana vipi, lakini alikuja kuwa rafiki yangu. Alikuwa ni mwenyeji wa Mkoani Ruvuma na pale Mbeya alikuwa amekuja kumuuguza kaka yake, ambaye alilazwa hospitali ya rufaa Mbeya. Nilimpenda kwa kweli, hasa nidhamu yake na hekima. Kiumri alinizidi miaka minne. Mimi nilikuwa na miaka 29 wakati huo na yeye 33. Lakini kwa kutazama, mtu angedhani mimi ndiye nilikuwa mkubwa. Niliishi naye kama mke wangu, hadi miezi mitatu ikaisha, nilirudi Dar nikimwacha bado anauguza mgonjwa wake. Wiki mbili baadae tangu nirudi Dar tuliletewa taarifa kwamba baba wa mke wangu amefariki dunia. Tuliamua kusafiri kwenda kwenye mazishi Songea, wakati huo mimba ya mke wangu ilikuwa imetimiza miezi sita. Tuliondoka mimi, yeye, na ndugu zake wawili na ndugu yangu mmoja. Tulifika kijijini kwao jioni, ambapo tulikuta mazishi yakiendelea, tulienda makaburini tukimwacha mke wangu nyumbani kutokana na hali yake. Tulipofika makaburini ilikuwa ndiyo zamu ya kuweka mashada ya maua kaburini.Ilikuwa kama ndoton Fulani, kwani nilimwona yule hawara yangu wa Mbeya akiweka shada la maua na alitajwa kama mke wa marehemu. Nilihisi kama nataka kupoteza fahamu. Nilijikaza, ingawa nilikuwa natoka sana jasho. Baada ya mazishi tulirudi nyumbani, ambapo ilibidi nitambulishwe kwa mzazi wa mke wangu na ndugu zake. Nilitambulishwa kwanza kwa mama mkwe ambaye kule Mbeya alikuwa ni hawara yangu. Kila mmoja kati yetu alijikaza ili isifahamike kinachoendelea. Lakini, hiyo haikudumu, kwani bomu likalipuka sawia. Mama mkwe wangu alilazimika kusema kwa wazazi wake, ati akiogopa mkosi utokanao na jambo kama hilo. Ilibidi siku ya nne baada ya msiba tufanyiwe tambiko la kiasili kuondoa laana. Nataka nikwambie katika maisha yangu sijawahi kukabiliwa na mtihani mgumu kama ule. Ninaye bado mke wangu na tumesahau yaliyopita. Mama mkwe hajawahi kuja kwetu, ingawa sisi tunaenda na kukaa siku chache kwake, kila mwaka.TUTAONANA TENA JUMATANO IJAYO PANAPO MAJALIWA!!!!!

5 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

hii kali kuliko...fundisho zuri hapo!

Aksante Da Yasinta kwa kutuletea kisa mkasa hiki!

ISSACK JIAH said...

hayo nimaajabu ya ulimwengu duu haya bwana pole sana kwani ukiwa safarini lazima ujitambulishe kwanza usivamie mambo kabla hamjajuana kama ungempa histori ya maisha yako japo kidogo yasingekuwa hayo
CHe Jiah

emuthree said...

Hili nii fundisho, tupo pamoja ndugu yangu

Anonymous said...

he..hii kali ya mwaka..nishangae kiwatani zangu!! WAJEMENI!!!!!

Anonymous said...

Muoe na yeye kwani kimebaki nini kama ni hadithi ya kweli?