Friday, March 9, 2012

NGOMA ZA ASILI NI NZURI JAMANI HAYA EBU TUANZA MWISHO WA WIKI NA HII!!!!


Hapa ni ngoma ya mganda hii nimecheza sana wakati nipo shuleni ila ni maalufu kwa wavulana/wanaume.

Au labda tuwasalimie ndugu zetu huko Botswana ebu sikiliza hizo sauti hata kama huelewi utainuka tu na kucheza.....


Kama nilivyosema hata kama huelewi utacheza au utasikiliza tu NAIPENDA AFRIKA NA TAMADUNI ZAKE..
Ngoma nyingine za asili nazozitamani ni Muhambo, Beta, Chomanga, Lindeko, Madogili, Limbamiza nk. HAYA JAMANI IJUMAA NJEMA.....

13 comments:

ray njau said...

Jasiri haachi asili na muacha asili ni hasidi na hana akili.Kwako ni kwako na wazazi wako japo maisha na mafanikio ndani ya pango la Ruhuwiko.

sam mbogo said...

ngoma za asili ni kweli zina utamu wake,hasa ukizijuwa kucheza. nashukuru kuzifahamu kuzicheza,na hasa baada ya kupita na kusoma chuo cha sanaa Bagamoyo,kunanaraha ya ajabu hasa pale unapo cheza,Lizombe,mangaka,sindimba,bugobogobo,nkinita,ukala,mawindi,malivata,lipango,mkwaju ngoma,chikocha,masewe,msewe,nk hizi ngoma nimezicheza na nyingine nishaanza kuzisahau ila zinakupa nidhamu fulani katika maisha ukizisomea kama taaluma. kaka s.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray kweli umesema, naongezea najivunia sana uasili wangu na tamaduni zake....
Kaka Sam! umenikumbusha masewe nilisahau kwelikweli...na nashukuru kwa hizo ngoma nyingine ulizozitaja sikuzijua....

Anonymous said...

Da Yasintha halafu hii ngoma inafanana na lizombe some of their steps hasa pale mwishoni walipoamka wote.mi nimecheza sana ngoma ya lizombi nilipokuwa mdogo,asante kwa post hii nimefurahi.
mdau mlongo ku USA.

Yasinta Ngonyani said...

Mlongo wa USA. Hujakosea kabisa yaani step zao kama lizombe kabisa ndio maana niziganili sana na hapa nikina kweli namuyaku.

emuthree said...

Mwenye kuacha utamaduni wakeni mtumwa, tupo pamoja dada Yasinta

Ausal said...

Asiyejali asili na tamaduni za kwao ni mtumwa!Hongera Yasinta nakupenda sana kwani pamoja na maisha na mafanikio bado ujivuni wala kujikweza najifunza mengi kutoka kwako.

Rachel Siwa said...

Duuhh nimechezaa mpaka nimechoka, kaka S mwana wa mbogo,Hongera kwakuzijua kucheza zoote hizo,Natamani siku moja niwaone wewe na da'Yasinta mkiserebuka,Timwilika, mimi nichukue pichaaa,tena hii iwe bonga kwani nafasi ni nzuri zaidi.MTU KWAO!!!

Rachel Siwa said...

Samahani nilitaka kuandika BONGO!!

Yasinta Ngonyani said...

emu3! Siku nitakayoacha uasili wangu ni siku ile nitapoiacha dunia hii. Pamoja daima
Ausal! Ahsante ni furaha kwangu kusikia unajifunza mengi kupitia hapa. Tamaduni ni msingi wa mtu na sitaacha wala kusahau asili yangu kamwe.

Rachel! umenichekesha wewe nakwambia hiyo siku utaponiona naselebuka hutanijua halafu hiyo ngoma sasa inabidi usivae kiatu hapo ndo utafaidi utamu wake...Tumsubiri kaka Sam asema lake:-)

sam mbogo said...

mimi niko tayari kucheza ngoma mojawapo katika hizo nilizo zitaja,nakuongezea nyingine,ngokwa nakwambia sikuhiyo hapatatosha. hii siyo kungojea bongo tu,Rache l,bisikuti yangu wanawake/kinamama oyeeee! niambieni popote nitakuja kwa gharma zangu mzuka umepanda. kaka s

Simon Kitururu said...

Mie nimenogewa!

Rachel Siwa said...

Duuuhh Sam mwana wa mbogo, Mzuka umeshampanda, inabidi da'Yasinta aje huku kwani tupo wengi!!!!hehehehe Sipati pichaa,kaka wa mimi Kitururu umenogewa na nini?