Wednesday, March 28, 2012

PIKINIKI MAKABURINI! Je ukimchungulia mtu mzima Utapofuka macho?

HAYA JAMANI NI ILI JUMATANO YETU YA KIPENGELE CHA MARUDIO MBALIMBALI NA PIA NI JUMATANO YA MWISHO YA MWEZI HUU. MADA KATIKA PITAPITA ZANGU NIKAKUTANO NA MADA HII SIO KWINGINE TENA BALI NIMEIPATA MAWAZONI KARIBUNI SANA.
Naamini mila na desturi zetu wabongo bado zina nguvu sana ingawa watu wanadai hizi ni zama ya bongo fleva. Naamini kuwa katika shule zetu za jadi mbinu mbalimbali zilitumika kuwezesha mambo fulani katika jamii kwenda shwari na kulindwa kwa nguvu zote na jamii. Mimi ni mchanganyiko wa Kipare na Kijita na katika makabila yote haya mawili njia za kuelimisha zilitumia mbinu nyingi ikiwa pia na vitisho. Mfano kwa Wapare maswala ya kufundishwa kuwa mwanamume wa shoka yaliendana na vitisho na maumivu. Kama wewe ni mwanamume basi lazima uweze kuvumilia maumivu .Nadhani kwa walioenda jando watakumbuka! Kulikuwa mpaka kuna simba wamsituni akumezaye ukishindwa kufanikisha mambo fulani ya kidume. Hii maana yake ulikuwa unauawa ingawa ilidaiwa umeliwa na Simba. Sasa njia hizi za kutufundisha heshima , maisha na hekima nyingine nyingi zikajakuuawa na wakoloni na wengine walioleta tamaduni mpya. Basi unaweza kudhani kwa sababu Wakoloni waliua shule za jadi basi na baadhi ya mambo tuliyokuwa tunatishiana yamekwisha!Utadhani mpaka sasa tumeweza kuelewa au hata kujiuliza ni kwanini mambo mengine yalitishalo kabila moja, hayalitishi jingine hata hivi sasa baada ya makabila ya Tanzania kuchanganyika na kutawanyika katika mikoa mbalimbali . Jibu bado tukopalepale. Tunaamini wachawi wanapaa na ungo ingawa hata kushuhudia hatuja shuhudia. Tunaamini kibibi fulani kichawi kwasababu macho yake mekundu bila kushuhudia aliyelogwa. Tuna chanja na kuvaa hirizi kibao bila ya uhakika hata wa ni nini hasa tunakiogopa. Sitaki kukataa kuwa hakuna uchawi kwa sababu hili ni jambo lililorekodiwa miaka mingi tu na vitabu vingi vimelizungumzia. Lakini mimi ninachoamini ni kwamba uchawi mkubwa ni hofu ya kibinadamu itokanayo naupungufu wa kibinadamu wakutokujua. Na upungufu huu kwa bahati mbaya hauna dawa. Upungufu huu umefanya wengine waabudu miti ili kuujazia, wengine Yesu, na Wengine Mtume Mohamedi. Tatizo jingine la upungufu huu uko kama njaa, kila siku unahitaji kupewa chakula ilikujazilizia pengo la upungufu wa kibinadamu ilikupata uhaueni. Mimi naamini pamoja na kuwepo wachawi, moto wa ahera na mambo yote hayo, lakini upungufu wa kibinadamu wenyewe hulenga binadamu kitofauti kutokana na binadamu mwenyewe alivyo na mazingira yake katika kumuelekeza binadamu huyu kuamini nini kinampa ujazo na uhaueni. Basi utakuta huku wanaogopa makaburi, kule wanaogopa mbuyu na hata wengine kukimbia vifuu vya nazi kutokana na mazingira yao. Basi unaweza ukakuta kutokana na mlengwa hirizi ikajazia na kuziba hofu hiyo, dini au hata kujinyonga. Naamini ubongo wa binadamu unanguvu kiasi kwamba hufanyia kazi hofu za binadamu na kuzipa uhai na uhalisi.Na naamini asilimia kubwa ya wajulikanao kama wachawi, waganga wa kienyeji au hata uchawi wenyewe haukuthibitika ingawa una uhalisi. Halafu si kweli zote ni zakufundisha maana nyingine ni zakutishana kwa madhumuni yakutishana tu.Na nyingi za mila na desturi hizi hatakama zilikuwa zinafundisha zamani hazina mchango mkubwa sasa hivi katika kuifundisha jamii ya leo.Na kama kuna sababu zakuzikubali hizi dini za kuletwa moja ni kwamba kwa sasa ndio zimeshikilia ukanda katika kuipa jamii muelekeo, ingawa hata kwa hili sina uhakika zitaweza jukumu hili mpaka lini kama jamii haifumbui macho nakuelewa mchango wake bila ya kukariri na kufuata kiulimbukeni. Lakini hizi mila za kutishana kwa dhumuni la kufundisha kitu haziko afrika pekee. Na rafiki yangu Myahudi alikuwa anatishwa na wazazi wake asiweke Tattoo kwa sababu hata weza kuzikwa kiyahudi akiwa na tattoo, kitu ambacho baadaye akagundua hakina ukweli. Nakumbuka pia nilipotembelea Russia mitaa ya Viborg nishawahi kuwatisha wenyeji wangu kwa kuwa nilipiga mluzi ndani ya nyumba na wao waliamini kabisa kwa kupiga mluzi ndani ya nyumba unaleta bomba la balaa. Kitu ambacho mimi siamini, kwani mimi nilifundishwa usipige miluzi porini. Hivyo hizi mila na desturi ambazo zina mambo haya ya kutishana haziko Afrika tu. Duh !Unakumbuka kitabu kiuzacho kuliko vyote siku hizi cha Harry Potter kinastori gani za kichawi?Sasa ngojea nikupe stori fupi kuhusu uoga wangu wa makaburi.Nakumbuka tokea utotoni nilizoea kusikia habari za kutisha kuhusu maeneo ya makaburini. Nakumbuka kunakipindi nilikuwa nang'ang'ania kutokwenda kulala mapema ilikuendelea kusikiliza stori za wakubwa, basi ilikutaka kunifanya niondoke wanaanza kusimulia stori za kutishatisha. Sehemu kubwa za stori hizi zilikuwa zinalenga maswala ya majini mashetanishetani na maeneo ya stori yanakuwa makaburini. Basi nisitake kukuongopea mara nyingi ilivyokuwa inaingia giza nilikuwa natishika kukatizia njia yoyote inayokatizia makaburini.Kilichokuja kunishinda ni pale nilipokuwa natembelea Upareni kwani kule ni kawaida kabisa marehemu kuzikwa katika eneo la nyumba. Sasa kutokana na kukulia mikoani ambako kunatamaduni za kuogopa maeneo ya makaruri ilinichukua muda kidogo kuzoe mpaka kuona ni kawaida.Kama nakumbuka vizuri Wachaga nao hawana uoga sana na makaburi hivyo nadhani kwa waogopa makaburi wanaweza kupata taabu sana uchagani na Upareni pia. Lakini akipata tabu Uchagani atatokwa na jasho akikatiza katika anga kama za Ufini ambako kuna mpaka siku katika mitaa ya krismasi ambapo makaburini ndio pakwenda sio kikilio bali kimatembezi. Mila na desturi zetu nyingi ni nzuri lakini hatuzisomi na kuzielewa sasa hivi tunapo ingia katika tamaduni za bongo fleva. Tatizo linalojitokeza ni kwamba mila nyingi nzuri zitapotea, halafu na zipo mila na desturi nyingi zisizo na manufaa sana kwetu tutaendelea kuzitunza. Bahati mbaya mila ambazo zitatunzika ni zile tuziogopazo! Je ukimchungulia mtu mzima utapofuka macho?Je , utakwenda pikiniki makaburini?

PANAPO MAJALIWA TUTAONANA JUMATANO NYINGINE TENA. KILA LA KHERI!!!!

10 comments:

Simon Kitururu said...

DUH!

Yasinta Ngonyani said...

nami nimekumbuka nilipokuwa mdogo nilikuwa nasikia wakisema usipige mluzi jioni/usiku ukiwa ndani ya nyumba kwani ukifanya hivyo nyoka watakuja yaani ilikuwa ni kama kuwaita. Pia hiyo ya kupita maburini ilikuwa ni mwiko kabisa. Halfu umewahi kusikia ya kwamba mtoto mdogo kuanzia mwezi hadi miezi sita huwa wanalia sana hasa masaa ya jioni basi kule kwetu WANGONI tuna mila ni kwamba mtoto huyo analilia jina la mababu/marehemu basi hapa watawataja wafu wote na mtoto akinyamaza basi amelikubali hilo jina lilitaja. Kwa maana hiyo itabidi ashikwe kuku na kukabidhiwa yaani kama shukrani. ngoja na wengine wapate nafasi....

sam mbogo said...

Kazi kwelikweli. ila naweza kusema hivi, shikilia kile nafsi yako inakutuma kukiamini. uchawi upo namamboyake yote yahusi uchawi. mila nadesturi za makabila mbalimbali zipo,na kuna wanao ziendeleza mila hizo kutokana na mahitaji yake. dini zipo na zitaendelea kuwapo kwa wale wanaoziamini.,kumchunguli mtu mzima hupofuki ila ni adabu tu inayo sisitizwa hapo, ,ndomaana zamani ,mtu mzima akijamba,kama kuna mtoto pale karibu lazima amsitiri mtu mzima huyo kwa kujitaja kuwa yeye ndo kachia kitu(kajamba).kaka s.

batamwa said...

mhh kaka s sawa kabisa kamaulivyo sema yasinta kwetu huko bukoba mtoto akizaliwa akilia sana miezi hiyo nahana tatizo lolote la kiafya basi wanasema anataka aitwe jina la mababu hivyo anapelekwa kwa babu akishapewa jina hilo basi mambo shwari ndio mila na utamaduni huo tuyaenzi mazuli ya kimila na mabaya tuyatunze kama alivyosema mtakatifu kitururu

batamwa said...

mhh kaka s sawa kabisa kamaulivyo sema yasinta kwetu huko bukoba mtoto akizaliwa akilia sana miezi hiyo nahana tatizo lolote la kiafya basi wanasema anataka aitwe jina la mababu hivyo anapelekwa kwa babu akishapewa jina hilo basi mambo shwari ndio mila na utamaduni huo tuyaenzi mazuli ya kimila na mabaya tuyatunze kama alivyosema mtakatifu kitururu

emu-three said...

Yah, wazee wetu walikuwa na hekima, wanasema kuwa ukimchungulia mtu mzima, utaota kile kipele cha jichoni...ni imani, kama zile ukiruka mdudu utapotea njia, na ukikutana na nyoka mwenye vichwa viwili, kuna balaa...pia kuna bundi akili akwenye bati,...na vitu kama hivyo, ni imani na wazee wetu walikuwa na sababu....na hekima pia.
Shukurani dada Yasinta na mkuu ndugu yangu Simon

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Dah.... mwanaume ukiruka kanga ya mwanamke ama ukipigwa na upande wa kanga ya demu unageuka kuwa demu!!!

ni vijimambo vya kale tu hivo!

Rachel siwa Isaac said...

Duuh kazi kwelikweli, Chumvi haiombwi usiku,duh Makaburini Msimbazi kulikuwa na Maembe tuliosoma hapo tumepopoa sana tuu,lakini peke yangu nilikuwa naogopa kupita hata mchana tuu!

simba deo said...

Rachel Siwa Isaac, kumbe na wewe ulipopoa maembe ya pale Msimbazi makaburini? Ilikuwa enzi zipi hizo? Ila Simon, UCHAWI ule wa kulogana ni fix. Haupo. Uliopo ni huu wa majungu, fitina, kijicho, kusingiziana, kubambikiziana, kuiba, kufisadi ... huo ndiyo uliopo na una madhara ya hakika na bayana kabisa. Tunaona kila siku 'uchawi' huo unavyoliumiza taifa na mtu mmojammoja. Tupo pamoja sana. Asante Yasinta.

Rachel siwa Isaac said...

Simba deo duhh hayo uliyosema ni Uchawi mkubwa sana, kusingiziana,Majungu na.........

Sasa turudi kwenye MAEMBE YA MSIMBAZI MAKABURINI!!Hahahahh nimepopoa sana tuu,Tena tulikuwa tunatumia Misalaba,duuhh SIMBA DEO niliacha kupopoa pale mwaka 1988.je ulisoma Mseto au Boys,au ulikuwa unakaa mitaa ile? hahahhaahhh duuh kwa BURUDA!!!!!!