Monday, March 26, 2012

UJUMBE WA JUMATATU YA LEO!! MATATIZO KATIKA MAISHA!!

Ulijua kwamba:- Matatizo ni mazuri kwa vile hukufanya uwe mbunifu. Pili huwezi kukwepa matatizo kama unaishi hapa duniani. Matatizo ni sehemu ya maisha, tatizo kubwa linakuja jinsi unavyoliona tatizo, ukiliangalia tatizo tofauti basi tatizo huwa kubwa zaidi na ukiliangalia tatizo kama sehemu ya ufumbuzi au ubunifu au hamasa ya kufanikiwa na kupiga hatua basi ukipata tatizo badala ya kulalamika na kuona unaonewa utachangamka na kuanza kushughulikia. Nahisi matatizo yangu ninayokutana nayo ni makubwa kuliko yako ila naamini yangu ni yangu na nikiyashinda tu nitakuwa mbali zaidi na nitakuwa mtu wa mafanikio.Mara nyingi matatizo nayo huwa yanazalisha stress sana kwa hiyo inabidi daima uwe imara kuyatatua lakini siyo matatizo ambayo yanakufanya uumie huku wanaokuumiza hawana chembe ya haki ya kukuumiza angalia usianguke.
Tumalizie na wimbo huu usemao MATATIZO NIMEYAZOEA

JUMATATU NJEMA !!!!!!!

5 comments:

sam mbogo said...

Napenda niseme,kwamba ujumbe wa leo nimuhimu sana kwa sisi binaadam. neno tatizo au matatizo ni pana sana.mwanamuziki kaimba kuwa matatizo kayazoea yuko sahihi kwa upande wake.Ila kwa mtazamo wangu mimi nipatapo au nipatwapo na tatizo au matatizo,kitu cha kwanza hulikubari hilo tatizo(kulipokea),pili huliangalia kwa jicho la ndani je ninani aliye sababisha tatizo hilo/hili? je nimimi? au nimtumwingine. Tatu nikishajuwa chanzo chake hapo huwa sipotezi muda, kama chanzo ni mimi basi nitatafuta njia za kulitatua kimazungumuzo,na hapa kama nikati yangu namtu mwingine awe rafiki,mke ndugu au hata jamaa.kama tatizo hili lime sababishwa namtu mwingine,hapa niwajibu wangu kujuwa huyu mtu,jamaa nini kimemsukuma mpaka kunitumbukiza mimi katika tatizo? maranyingi hujiambia au kujiuliza je ningekuwa mimi katika nafasi yake ningefanyaje kuhusu tatizo hili.kiukweli unaweza kugundua mengi tu kuhusu huyo mtu au jamaa yako hasa kuhusu tatizo lenyewe,mfano waweza gundua kumbe anakilema,nakilema hicho ndo kina mfanya marakwamara mkwaruzane,nawewe kama binaadamu unaona unafanyiwa siyo vizuri. kwahiyo ukisha muelewa mtu nirahisi kujiepusha na matatizo ambayo kabla ulijuwa labda nimakusudi nakujijali wewebinafsi ,kumbe tatizo siwewe.nahapo utajipunguzia msongo wa mawazo .ndomaana wengi husema matatizo nikupambana nayo, ila sikujitesa nayao. kaka s.

Ester Ulaya said...

Ujumbe mzuri sana, matatizo yapo kwa kila mtu, na ni wajibu wetu kuyakabili na si kulalamika kuwa mimi ndo nina matatizo mengi zaidi ya wengine, angalia matatizo yako bila kuyalinganisha

Rachel siwa Isaac said...

Ahsante sana Binti Ngonyani kwa Ujumbe Mzuri!!!Bwana weee chebisikuti yangu kaka Sam baa Umenena!!!

ray njau said...

Biblia Inafundisha Nini Hasa?
Je, Hivi Ndivyo Mungu Alivyokusudia?
----------------------------
KATIKA magazeti, televisheni, na redio, kuna habari nyingi kuhusu visa vya ugaidi, vita, na uhalifu. Hebu fikiria pia mahangaiko yako mwenyewe. Labda unasumbuliwa na ugonjwa fulani au umefiwa na mtu unayempenda. Huenda ukahisi kama alivyohisi Ayubu, aliyesema kwamba maisha yake yalikuwa ‘yamejaa masumbuko.’—Ayubu 10:15, Verbum Bible.
Hebu jiulize:
• Je, hivi ndivyo Mungu alivyokusudia maisha yangu na ya wanadamu wengine yawe?
• Ninaweza kupata wapi msaada wa kukabiliana na matatizo yangu?
• Je, dunia itapata kuwa na amani?
Biblia inajibu maswali hayo kwa njia ya kuridhisha.
BIBLIA INAFUNDISHA KWAMBA MUNGU ATATIMIZA MAMBO HAYA DUNIANI.

“Atafuta kila chozi kutoka katika macho yao, na kifo hakitakuwapo tena, wala maombolezo wala kilio wala maumivu hayatakuwapo tena.”—Ufunuo 21:4


“Kilema atapanda juu kama vile paa anavyofanya.”—Isaya 35:6


“Macho ya vipofu yatafunguliwa.”—Isaya 35:5


‘Wale wote waliomo ndani ya makaburi ya ukumbusho watatoka.’ —Yohana 5:28, 29


“Hakuna mkaaji atakayesema: ‘Mimi ni mgonjwa.’”—Isaya 33:24


“Kutakuwa na wingi wa nafaka duniani.”—Zaburi 72:16

FAIDIKA NA MAFUNDISHO YA BIBLIA

Usidhani kwamba mambo hayo ni ndoto tu. Mungu ameahidi kwamba atatimiza mambo hayo, na Biblia inaeleza jinsi atakavyofanya hivyo.
Hata hivyo, Biblia ina faida nyingine nyingi. Inaweza kukusaidia kuwa na maisha yenye kuridhisha hata sasa. Hebu tua kidogo, ufikirie mahangaiko na matatizo yako mwenyewe. Huenda yanatia ndani ukosefu wa pesa, matatizo ya familia, matatizo ya afya, au kifo cha mpendwa. Biblia inaweza kukusaidia kushughulika na matatizo leo na inaweza kukufariji kwa kujibu maswali kama haya:
• Kwa nini tunateseka?
• Tunawezaje kushughulika na mahangaiko ya maisha?
• Tunawezaje kufanya maisha ya familia yetu yawe yenye furaha zaidi?
• Inakuwaje tunapokufa?
• Je, tutapata kuwaona wapendwa wetu waliokufa?
• Tunawezaje kuwa na hakika kwamba Mungu atatimiza ahadi zake kuhusu wakati ujao?
Kusoma kitabu hiki kunaonyesha kwamba ungependa kujua yale ambayo Biblia inafundisha. Kitabu hiki kitakusaidia. Sehemu ya chini ya kurasa kuna maswali yanayoambatana na mafungu. Mamilioni ya watu wamefurahia kuwa na mazungumzo ya Biblia pamoja na Mashahidi wa Yehova kwa njia ya maswali na majibu. Tunatumaini kwamba wewe pia utafurahia kufanya hivyo. Mungu na akubariki unapochukua hatua hiyo yenye kusisimua na kuridhisha ya kujifunza mambo ambayo Biblia inafundisha hasa!
IJUE BIBLIA YAKO

KUNA vitabu 66 katika Biblia. Kila kitabu kina sura na mistari, ili kurahisisha usomaji. Maandiko yanapotajwa katika kitabu hiki, nambari inayofuata jina ndiyo sura ya kitabu au barua katika Biblia, nayo nambari inayofuata ni mstari. Kwa mfano, “2 Timotheo 3:16” ni barua ya pili kwa Timotheo, sura ya 3, mstari wa 16.
Ukifungua na kusoma maandiko yaliyo katika kitabu hiki, utazoea kuitumia Biblia. Pia, mbona usianze kuisoma Biblia kila siku? Ukisoma sura tatu hadi tano hivi kila siku, unaweza kuisoma Biblia nzima kwa mwaka mmoja.

seleman Awadh said...

Ni kweli Dada matatizo ni sehemu ya darasa zuri sana ila yanatofautiana makali na pia kuna haki hazipatikana hapa duniani ila tu mpaka mbinguni nadhani kwa wale wanaoamini siku ya mwisho watakuwa wanaamini ninavyoamini mimi.Sitaongea mengi ila umenigusa sana ni kwakuwa tu mwanamme machozi hudondokea ndani yasionekane na hata ukilia utamlilia nani?Haliyakuwa wewe ndio mwenye dhamana ya kutatua matatizo yanayokuandama.Ni kweli matatizo hayawezi kutokeasehemu nyingine isipokuwa duniani na humtokea mara nyimgi binadamu ila kama ulivyosema inawezekana ukapambana ukashinda na mengine ukashinwa ila mwisho wa yote usishindwe ukanyong'onyea nafsi (MKABIDHI MUNGU MATATIZO YAKO YOTE UNAYOYAONA KWAMBA NI MAZITO KWAKO KWANI YEYE HUJIBU KWA NAMNA YA PEKEE KABISA.