Friday, March 30, 2012

SWALI LA WIKI HII!!!!

Umewahi kufanya maamuzi magumu sana kwenye maisha yako? ilikuwa ni kuhusu nini?haya funguka sasa!
NAWATAKIENI WOTE KILA LA KHERI NA MUWE NA MUDA MZURI NDANI YA MWISHO WA JUMA HILI LA MWISHO WA MWEZI HUU WA TATU.UPENDO DAIMA.

6 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

kukaa kimya!!!

Anonymous said...

Nilikunywa uji wa mtoto wangu mwenyewe baada ya kubanwana njaa ya kufa mtu1

Anonymous said...

nilishawahi kufanya maamuzi magumu kumwacha mkewangu..........baada ya kugundua anatembea na mdogo wangu

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Chacha! kwa nini kukua kimya?
Usiye na jina wa 1.48 njaa haina mkubwa ndugu yangu...
Na usiye na jina wa 2:09..Hayo kwali ni maamuzi magumu...pole sana na ukizingatia kuwa alimchagua mdogo wako....

Simon Kitururu said...

Niliamua kuacha kudanganyika na RAFIKI nimpendaye baada ya kugundua yeye ni watu WAWILI au ELFU na inategemea tu na mazingira! Ila sina kinyongo kwa kuwa nimegundua anafurahisha kila watu wakati kwangu miye nimestukia HAKUNA BINADAMU afurahishaye kila mtu kama kweli kangangamala kikweli kwa UKWELI hata wa nani ni RAFIKI wa KWELI!

Yasinta Ngonyani said...

Mtakatifu Simon! Una uhakika huyu RAFIKI umpendaye kweli ni watu WAWILI? inawezekana labda alikuwa na hofu tu...Na unaposema ya kwamba umegundua kuwa anafurahisha watu wote unamaanisha nini?...Hii inasikitisha kidogo ningekushauri uongee na RAFIKI yako ili muongea. Maana RAFIKI ni kitu bora sana....Ni ushauri tu!!