Monday, March 5, 2012

JE? HAPA BORA ELIMU AU ELIMU BORA?

Picha hii imenirudisha mpaka enzi nipo shule ya msingi. Naweza kusema mie nilikuwa na bahati kwa vile baba yangu alikuwa mwalimu, tulikuwa tukiishi nyumba za shule ambazo zilikuwa karibu sana na shule. Lakini kulikuwa na wanafunzi walikuwa wakiishi mbali sana, na mwanzo wengi walikuwa wakishinda na njaa. Ila baadaye ndo wakagundua mtindo huu ya kwamba walikuwa wakichukua mboga na unga na shule ilijenga jiko wakawa wanapika pale shuleni. Ila ilikuwa kazi yao kuangalia kuna kuni maji na kadhalika.
Ama kweli maisha ni kujitegemea nikawa najisemea mwenyewe!!! Halafu nikawa najiuliza kweli hawa wanafunzi watasoma kweli au watakuwa wanafikiria jinsi ya kuanza kupika? halafu pia kusoma bila kula nako si vizuri.....maswali mengiiiiiiii....tujadili pamoja...

1 comment:

Rachel Siwa said...

Duuhh maisha ni safari ndefu sana!!!mmmhh watu wanapitia magumu mpaka kufikia walipo,Mungu yu mwema!