Thursday, March 8, 2012

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI :- UJUMBE!!!

Mwanamke ni kama jua ambalo bila wao sayari ingekuwa bila watu.
Unapotoa, ni kama kutoa pumzi ya uhai.
Na kuzaliwa kwa mtoto, aliye tumboni mwake.
Wanawake ni watu wa kipee, kama watu wangejkuwa wema wangewapa wanawake thamani zaidi.
Wanaume/watu hawajui vipi kujivunia wanawake na ndio sababu wanawake hawasikilizwi hata kama wana la kusema.
Ba watu wanajifanya vipofu ili kuweza kurahisisha ushahidi wao katika neema ya kutambua uzuri wa wanawake.
HONGERA WANAWAKE WOTE KATIKA DUNIA HII. PIA TUSIWASAHAU WANAUME KWANI BILA WAO UWEPO WETU HAUNGEKUWEPO.

8 comments:

Ester Ulaya said...

Upendo kati yetu ndo nguzo kuu, asante sana kwa ujumbe na Mungu aendelee kutubariki wanawake, Amen

Baraka Chibiriti said...

HONGERA SANA DADA YASINTA NA WANAWAKE WOTE WATAKAO SOMA UJUMBE HUU....HONGERENI SANA BILA NYINYI TUSINGEKUWEPO DUNIANI.

Anonymous said...

pamoja na yote bila kuwepo mwanaume hakuna mwanamke sote tunashirikiana,hatahivyo ninawapongeza sana wanawake halafu ninawapenda sana

SIMON KITURURU said...

Wanawake OYEEE!

Rachel siwa Isaac said...

Oyeeee kaka wa mimi Kitururu mwana,Ahsante da'Yasinta kwa Ujumbe.

sam mbogo said...

bado mnasafari ndefu wanawake wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.ila kuwapongeza haikataliwi hongereni sana.
kaka s.

Festo Tarimo said...

Maendeleo ya Mwanamke ni Maendeleo ya Taifa zima, Pokeeni Pongezi Zenu Wanawake wote akiwemo Mama yangu Mzazi.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hongereni wanawake wote. Bila nyinyi kusingekuwa na jamii. Mungu Aendelee kuwabariki !!!