Tuesday, March 13, 2012

UMEWAHI KUJIULIZA HIVI.....

Kwanini Nguruwe Hana Pembe?

11 comments:

ray njau said...

1 Na Yehova akasema na Musa na Haruni, akiwaambia: 2 “Semeni na wana wa Israeli, na kuwaambia, ‘Hiki ndicho kiumbe hai ambacho mnaweza kula kati ya wanyama wote walio kwenye uso wa dunia: 3 Kila kiumbe kati ya wanyama chenye ukwato uliopasuka na chenye mwanya kwenye ukwato na kinachocheua, hicho ndicho mnachoweza kula.
4 “‘Ila hiki ndicho ambacho hamtakula kati ya wacheuaji na wenye ukwato uliopasuka: ngamia, kwa sababu ni mcheuaji lakini hana ukwato uliopasuka. Huyo si safi kwenu. 5 Pia wibari, kwa sababu ni mcheuaji lakini hana ukwato uliopasuka. Huyo si safi kwenu. 6 Pia sungura, kwa sababu ni mcheuaji lakini hana ukwato uliopasuka. Huyo si safi kwenu. 7 Pia nguruwe, kwa sababu ana ukwato uliopasuka naye ana mwanya kwenye ukwato, lakini yeye mwenyewe hacheui. Huyo si safi kwenu. 8 Msile yoyote kati ya nyama zao, wala msiguse mizoga yao. Hao si safi kwenu. _ Mambo ya Walawi 7:17-23
---------------------------------
17 Basi alipokuwa ameingia katika nyumba akiwa mbali na umati, wanafunzi wake wakaanza kumuuliza habari ya mfano huo. 18 Kwa hiyo akawaambia: “Ninyi pia hamna ufahamu kama wao? Je, hamjui kwamba hakuna chochote kutoka nje kinachoingia ndani ya mtu ambacho kinaweza kumtia unajisi, 19 kwa kuwa hicho hupita na kuingia, si ndani ya moyo wake, bali ndani ya matumbo yake, nacho hutoka nje na kuingia ndani ya shimo la choo?” Kwa njia hiyo akatangaza vyakula vyote kuwa safi. 20 Tena akasema: “Kile ambacho hutoka ndani ya mtu ndicho humtia mtu unajisi; 21 kwa maana kutoka ndani, kutoka katika moyo wa watu, hutoka mawazo mabaya: uasherati, wizi, mauaji, 22 uzinzi, kutamani, matendo ya uovu, udanganyifu, mwenendo mpotovu, jicho lenye wivu, makufuru, majivuno, ukosefu wa akili. 23 Mambo hayo yote maovu hutoka ndani nayo humtia mtu unajisi.”_Marko 7:17-23

Rachel siwa Isaac said...

Kwanini hana Pembe kulikuwa na sababu maalum?haya tujuze dada yangu.Ahsante kaka Ray kwa NENO!

Simon Kitururu said...

Kwanini Watu hawana MKIA?

Nami nimewaza tu!

Yasinta Ngonyani said...

Ray! ahsante kwa NENO...

Dada Rachel usiwe na haraka tusubiri kwanza inawezekana kuna wengi wanajua sababu:-)
Mtakatifu Simon! WATU WANA MKIA ila tu hauonekani...si unakumbuka historia ya binadamu?

Rachel siwa Isaac said...

Haya dada yangu tusubiri, hahahhaahah ooohhiii nimecheka Jibu ulilojibu kwa kaka wa mimi Kitururu mwanakwetu,nanukuu;''WATU WANA MKIA LAKINI HAUONEKANI''mAMA Erik!!!!!

Mija Shija Sayi said...

Sijawahi kujiuliza kwa kweli..ila nadhani ni zilezile sababu za vidole havilingani..

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni wote kwa michango yenu:-)
Hii ni hadithi ambayo nilisimuliwa na bibi yangu hapo zamani ni kwamba. Hapa kale mfalme wa wanyama aliwaita wanyama wote na kuwapa pembe na nguruwa akiwa moja wapo. Lakini nguruwe akawa anajidai kwa wanyama wale wadogo na kuwatisha kuwa ana pembe nzuri na wasipomtumikia watakiona cha mtema kuni. Wale wanyama wadogo wakaenda kwa mfalme wa wanyama kutoa taarifa...Mfalme wa wanyama akakasirika na kuzitoa zile pembe kwa nguruwe na hii ndiyo sababu nguruwe hana pembe...Je tupo pamoja hapa?

Penina Simon said...

Ha ha ha wewe Yahsinta, Kila mnyama aliumbwa kwa makusudi yake, sio kwamba kwa vile wote ni wanyama basi lazima wawe na maumbile sawa, naona sku nyingine utauliza tena kwnn paka hakuwa mbwa?

ray njau said...

Asante dada Yasinta kwa hadithi yako.Lakini hii inatufundisha nini sisi binadamu kama kwa ubabe wake nguruwe aliondolewa mapembe.Lakini mimi nami napata swali iwapo nguruwe kwa ukali wake angebakia na pembe hali ingekuwa tete!!

Simon Kitururu said...

@Dada Yasinta:Nahisi kuna historia ya BINADAMU siijui kwa kuwa siamini Binadamu alikuwa ana Mkia au hata sasa ana Mkia !

Na nimeona mpaka maiti zilizoanza kuoza na sehemu ambayo kungekuwa na mkia huwa hakuna MKIA!

Ila asante kwa hadithi na changamoto!

Matha Malima said...

ni nadhani ndio maumbile mungu alomjalia kuwa nayo