Kwanini watoto wa kiume hupewa mali nyingi na vitu muhimu kama vile ardhi na nyumba wakati watoto wa kike hunyimwa?
Nimewahi kuwasikia watu wengi wanadai kwamba sababu ya kutoa urithi kwa watoto wa kiume ni sababu wao hushika nafasi ya baba(marehemu) na kwamba ni HASARA ikiwa watoto wa kike wakirithi kwa vile wao huolewa na kuambatana na ukoo mwingine. Wanaona ya kwamba kuna hatari urithi wake kwenda kwa mumewe. Je huu ni uungwana kweli? NAOMBA TUJADILI KWA PAMOJA.....
8 comments:
Sio ugwana kabisa Dada Yasinta, ila ndio hivyo tulivyo utamaduni wetu toka enzi za mababu huamini hivi kuwa urithi hutolewa kwa watoto wa kiume kwasababu mali hubaki katika ukoo huo huo...tena kwa watoto wakike hata kile kidogo huwa ni shida sana kukipata. Utafikiri watoto wa kike hawajazaliwa na baba aliyefariki....(kuwa hawana haki na Baba yao) huwa sielewi kabisa kwanini swala hili, na bado lipo sana tena sana tu Tanzania yetu, wakati watoto wote wanahaki sawa hata kama ataolewa na kwenda kwenye ukoo mwingine, haki yake anatakiwa apewe halafu yeye atajua la kufanya na mali zake. Umenikumbusha mbali sana, mimi nilishawahi kugombana sana na ndugu zangu fulani kuhusu swala hili, maana nililisimamia kidedea sana....wananichukia mpaka leo, mimi huwa nasema potelea mbali ili mladi mdada alipata haki yake na anaendelea kusoma kwa haki yake aliyemwachia Baba yake marehemu. Hebu fikiria Dada Yasinta, hawa jamaa waliokuwa wakiombea mali hizi ni Kaka wa marehemu, walikuwa wakisema; huyu mtoto wakike sio ukoo wetu maana ataolewa na kwenda ukoo mwingine, hivyo mali zote zigawe kwa wanandugu halisi....mimi nilisimama na kusema ndugu halisi wa marehemu ni huyu mtoto wake, ndugu zaidi ya huyu hakuna....yani hili swala huwa linaniumiza sana tena sana,( watu unakuta hawana aibu hata kidogo kwenye mali za watoto). Utamaduni mwingine kama huu, mimi husema ni wa kishenzi sana tu! Na watu inabidi wabadilike kabisa kuhusu swala hili.
Hii ni changamoto ya kijamii na swali hapa ni:MTOTO WA KIKE ANA SEHEMU GANI MUHIMU KATIKA MIRATHI YA FAMILIA?
Kwa hili jambo la urithi Dini ndiyo msemaji, Mwenyezi mungu ameshagawa katika vitabu vyake sisi ni wafuataji.Hakuna tena kujadiliana ni kutekeleza mafuataji ya dini.
Kwenye Quran inasema ikiwa mzee amewacha mtoto wa kiume mmoja na wa kike wawili.
Nusu ya mali anapewa mwamume na nusu iliyobakia wanagawana mabinti.
wa kike watatu.
basi nusu ya mwanamume iliyobaki wanagawana wanawake watatu
pia tunasema mume ndio anamwongoza mke.
egual but not uniformity
man are the protector and maintainer of women,because go has given the one more (strengh)than te other'
Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili. Na ikiwa wanawake zaidi ya wawili, basi watapata thuluthi mbili za alicho kiacha maiti. Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja, basi fungu lake ni nusu. Na wazazi wake wawili, kila mmoja wao apate sudusi ya alicho kiacha, ikiwa anaye mtoto. Akiwa hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndio warithi wake, basi mama yake atapata thuluthi moja. Na akiwa anao ndugu, basi mama yake atapata sudusi. Haya ni baada ya kutolewa alicho usia au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu, nyinyi hamjui ni nani baina yao aliye karibia zaidi kwenu kwa manufaa. Hiyo ni Sharia iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima. (11)
Hii kitu inabadilika lakini siku hizi. na tukumbuke pia si kila kabila ni wanaume wenye neno. Nafikiri Morogoro kwa Waluguru kwa mfano ni mwanamke mwenye nguvu zaidi na maswala muhimu hupelekwa kwa Mjomba. Kwa hilo najaribu kutonya kuwa kuna makabila warithi ni wanawake. Na kama Mmasi kuwa na mabinti bonge la mradi!
Mimi binafsi nimeshaona mambo hayo yakitokea kwenye jamii inayo nizunguka lakini nichangie kwakusema tu kwamba kwa sasa hiyo hali imepungua sana kulingana na wanawake wengi wameamka na wanajua haki zao kingine ni mila nadesturi potofu nyingi zimeachwa kingine mimi napinga sana ubaguzi wa kijinsia sababu watoto wote ni sawa unaweza ukazaa wakiume asikusaidie na badala yake akutie hasara tu.Na unaweza ukazaa mtoto akawa ndio msaada mkubwa kwa familia.TUKOMESHE UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO WOTE NI SAWA,TUSIWABAGUE .MBONA DADA YETU WEWE UNAWEZA.
Post a Comment