Showing posts with label utajiri. Show all posts
Showing posts with label utajiri. Show all posts
Wednesday, July 26, 2017
MAKABILA TANZANIA: UTAJIRI WA KUJIVUMNIA
Je? wewe kabila lako ni lipi hapo? Tujenge Taifa letu. Tutumie utajiri wa makabila yetu kuwa na Taifa imara na lenye mshikamano wa hali ya juu. PAMOJA DAIMA!
Monday, July 23, 2012
Tuendelee na ile yetu …….HADITHI HADITHI…..HAPA NI HADITHI YA MVUVI NA SAMAKI WA DHAHABU!!!
Ilipoishia ”Usiwe na hofu, baba kizee enenda kwa amani sasa.” Baba Kizee alirejea kwa mkewe mzuri. Lo! Akaona nini?
Jumba zuri na barazani mkewe amesimama , amevaa vazi la maridadi la nyoya jema.
Na kichwani kavaa kilemba kilichotariziwa vilivyo na vito vyema vikimning´nia
shingoni. Na pete za dhahabu zilipamba vidole vyake na viatu vyororo vyekundu
vikimkubali miguuni….NA SASA INAENDELEA…………
Na mbele yake watumishi wakimhangaikia,
huku akiwavuta nywele zao na kuwacharaza bakora. Baba kizee akamsaili mkewe
mzuri “Je, waonaje sasa mke wangu sasa roho imeridhia kibibi? Mkewe akamjibu
kwa jeuri , na kumpeleka mazizini kufanya kazi za suluba huko.
Wiki moja ilipita iklifuatwa na
nyingine. Na mkewe mzuri akiwa haridhiki kupita siku zote. Akamwamuru baba
kizee aende tena baharini. “Enenda tena baharini ukamkabili samaki mkuu mwambie
sitaki kuwa mwanamke wa basaba bora bali malkia mwenye enzi!”
Baba kizee akaona vi mno akadahili kwa
nguvu. ”Nini tena, ew mwanamke! La hasha umechanganyikiwa! Kumbuka ya kuwa wanena na kutenda. Kama
mke wa mvuvi utaifanya milki nzima ilemewe na kicheko!”
Mke wa mvuvi akazidi kisirani akamvuta masikio mumewe na kusema ”unathubutuje
kubishana . Ewe kisonoko na mimi mwanamke wa nasaba bora? Elekea hivi sasa baharini nakuamuru!
Kama hutaki, nitakuburura hadi huko!” Baba kizee alijizoazoa na kwenda tena
baharini. Bahari ile ya maji ya mbingu ikawa nyeusi tii, tena inatisha.
Akapaza sauti yake, akaita na samaki wa dhahabu akaja akiogolea.
”Ni nini tena kinachokukera. Ewe baba kizee, hebu niambie!” Kwa mwinamo wa
hadhi baba kizee alijibu sawia ”ujaliwe neema Ewe Bwana wa Samaki! Mke wangu
mzuri amecharuka tena safari hii ajipa wazo hatakuwa tena mwana wa nasaba bora.
Yu ataka kuwa Malkia mwenye enzi.” Naye samaki wa dhahabu akajibu ”Usijali, ewe
baba kizee rejea nyumbani kwa amani nawe utamkuta mkeo mzuri yu malkia!”
Baba kizee alirejea kwa mkewe mzuri na nini alikiona? Jumba lla
kifalme, likimilikiwa na mwanamke wa hila akiwa ametamakani mezani. Wakuu na
mabwana wakimngojelea, wakimnywesha mvinyo kwenye chombo cha dhahabu huku
akividonadona vipande vinono vya nyama. Huku walinzi wenye macho makali
wakimlinda pande zote wakiwa wamejihami kwa vishoka mikononi. Baba kizee
akatupa jicho huku na huko. Jicho likamfeli, akagwaya! Alijiinamia hadhi
ardhini mbele yake na kuweza kutoa maneno haya ”Heshima kwako na kicho Ewe
malkia habe niambie sasa ikiwa moyo wako umeridhika?” Mkewe hakumthamini hata
kwa mtupo wa jicho bali aliamuru watu wake kumuondolea mbali. Ndipo waungwana
na wa nasaba bora wakamwelemea mbiombio wakamkwida shingoni. Na kumbeba
hangahanga na mabawabu wa mlangoni wakamsindikiza nje kwa vishoka vyao.
Na halaiki yote kwa jumla yao wakajisheheni kwa kicheko. ”Hiyo
ndiyo tosha yako ewe kizee mtovu wa busara! Na hilo liwe funzo lako kujijua
wewe u nani siku za hapo baadaye! Na hivyo wiki ikayoyoma na nyingine ikafuata.
Mama kizee akazidi utakavu, akatuma wajumbe wake kumkamata baba kizee.
Walimpata, wakamleta mbele ya Malkia. Naye mke mzuri akanena kwa mumewe ”Enenda
tena ukasujudu kwa samaki mkuu. Sitaki tena kuwa Malkia mwenye enzi, bali
nataka kutamalaki maziwa yote na bahari na katika vina vya bahari. Nitaweka
ngome yangu na huyo samaki wa dhabu atanitumikia mimi. Huku nikimtuma kotekote!”
Baba kizee hakuthubutu kupinga kauli ya mkewe hivyo akaenda tena baharini na
tazama! Tufani kuu ilitokea mawimbi makuu yaliinuka kumlaki, tetemeko tupu,
muondoko wa ghasia, muungurumo mkuu hata hivyo baba alipaza sauti na kuita. Na
samaki wa dhahabu akaja akiogelea ”kulikonit ena baba kizee njoo unieleze!” Kwa
mwinamo wa hadhi baba kizee akajibu sawia ”Na ujaliwe neema Ewe Mkuu wa Samaki!
Nimfanyeje huyu mwanamke? Huyu ajuza mjinga, hataki tena kuwa Malkia pia
anataka kutawala maziwa na bahari. Anataka kuweka ngome zake katika vilindi vya
bahari, na kukufanya wewe mwenyewe umtumikie. Na kukutuma wewe huk ona huko.”
Samaki wa dhahabu alitulia tuli pasi na jibu na badala yake alipiga mkia wake
majini akajerea kwenye maji makuu. Baba kizee alisimama ukingoni, akisubiri .
Alisubiri kwa muda mrefu, lakini halikuja jibu. Hatimaye akarejea kwa mkewe
mzuri, na tazama! Akamkuta amekaa mekoni kwenye kibanda kikongwe cha udongo na
miti na mble yake kukiwa na kibeseni kilichoraruka hadi katikati. HADITHI
IMEKWISHA..
Je Hadithi hii inatufunza nini?
Thursday, August 14, 2008
2008,8,14 UTAJIRI WA LUGHA
Watanzania kwa kweli tuna haki ya kujivunia nchi yetu nzuri yenye amani na utulivu. Halafu sasa kitu kinachonifurahisha ni kwamba Tanzania haina utajiri wa mbuga za wanyama tu na mlima wetu mrefu Kilimanjaro ambavyo watalii huja kuangalia. Hapana, Tanzania ni tajiri wa lugha mnajua hakuna nchi yenye makabila mengi kama TZ. Makabila 129(130) ambayo ni machache tu huwa wanaelewana wanapoongea, kama vile Wangoni na Wamanda, Wabena na wahehe nk. Hii ndiyo maana Hayati baba wa Taifa Mwl. J.K Nyerere aliona ni vema kuwe na lugha moja ambayo watu wote tutaweza kuongea na kuelewana ni lugha ya Taifa KISWAHILI.
Subscribe to:
Posts (Atom)