Showing posts with label matetereka. Show all posts
Showing posts with label matetereka. Show all posts
Monday, June 26, 2017
KUMBUKUMBU:- KARIBU TUNYWE PAMOJA MTANI
Leo nimekumbuka ubenani au niseme MATETEREKA KWETU kwa babu MBOZA...ULAZI. ILA huyu dada duh! kazi kwelikweli...nawatakieni JUMATATU NJEMA WOTE MTAKAOPITA HAPA!
Tuesday, October 30, 2012
SIKU YA MAHAFALI KATIKA SEKONDARI YA WILIMA/MADABA/MATETEREKA=SONGEA!!!!
Kutoka kushoto ni Meneja wa shule ya sekondari Wilima mzee Lucas Mayemba, katikari ni Mwl.Paul Mgaya wakati sisi tunaishi hapa alikuwa mkuu msaidizi. Hapa wapo katika jengo la utawala katika shule hiyo na mwisho hapo ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Songea Bw. Rajabu Mtiula
Thursday, November 3, 2011
Kijiji cha Lilondo wilayani Songea mkoani Ruvuma kinaoongoza kwa kuwa na ndizi nyingi
Leo mwenzenu nimekumbuka kweli enzi zili wakati naishi Matetereka. Kijiji hiki na kijiji jirani cha Lilondo kuna ndizi za aina mbalimbali. Wakati ule bei yake ilikuwa ndizi tatu shilingi tano. Halafu watu wa Matetereka pia Lilondo ni wakarimu sana. Licha ya ndizi, kuna magimbi si mchezo, karanga, mahindi, maharagwe, kahawa bila kusahau kinywaji cha ulanzi pia. Halafu kulikuwa na watu walikuwa wakipisha nyama pori...nimeyatamani sana maisha haya... Mtani Fadhy upoooo maana najua hapa vyakula hivi umekua nanyo:-)
Thursday, October 29, 2009
KUPOTEA KWA SIKU CHACHE + JIBU KWA DA MIJA KUHUSU PICHA HII HAPA CHINI!!!!

Pili napenda kumjibu Da Mija swali lake "Yasinta ile picha yako pale juu kabisa katikati uliipiga lini? naizimia sana." Jibu ni hili Da mija nilipiga mwaka 1992 nikiwa Wilima Sec. huko Madaba-Matetereka. Natumaini nimejibu kama ulivyotegemea dadangu.
Subscribe to:
Posts (Atom)