Thursday, October 29, 2009

KUPOTEA KWA SIKU CHACHE + JIBU KWA DA MIJA KUHUSU PICHA HII HAPA CHINI!!!!

Kwanza kabisa napenda kuwataka wote radhi kwa kupotea kwa siku hizi chache. Ila sasa nimerudi tena na TUPO PAMOJA.
Pili napenda kumjibu Da Mija swali lake "Yasinta ile picha yako pale juu kabisa katikati uliipiga lini? naizimia sana." Jibu ni hili Da mija nilipiga mwaka 1992 nikiwa Wilima Sec. huko Madaba-Matetereka. Natumaini nimejibu kama ulivyotegemea dadangu.

10 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ungeanza ku-blogu wakati wa kupiga picha hii sijui ingekuwaje binti. pozi limetulia hilo.

ulikuwa na boifurendi?

Simon Kitururu said...

Karibu tena Dada!Tulikumisi!

Christian Bwaya said...

Picha safi sana hiyo!

Fadhy Mtanga said...

Ulinitia hofu kwa kupotea kwako. Twashukuru kama u salama.
Picha pouwa sana. Ulitoka chicha. Bonge la pozi la kisichana. Bila shaka ulikuwa bado.

John Mwaipopo said...

mie sisemi. ila 'kalibu' tena

ERNEST B. MAKULILO said...

Old is Gold ndio oni langu dada Yasinta. Kipindi hicho cha 1992 upo Sekondari, hapo mimi darasa la pili shule ya msingi Kigoma, huko Kigoma kwa Bwana Zitto - Nyepesi bin Kabwe.

MAKULILO, Jr.
www.makulilo.blogspot.com
San Diego, CA

Mija Shija Sayi said...

Yasinta, Madaba Matetereka ndio wapi? samahani kwa maswali. Jamani una mapozi.

Yasinta Ngonyani said...

Wote ahsanteni kwa maoni. Tupo pamoja na upendo daima. Da mija Madaba-Matetereka ni vijiji vilivyopo Songea vijijini Tanzania. Natumanini sasa umenielewa.

Anonymous said...

Uliona wapi msichana kama huyo akakosa boifurendi, ni wazi alikuwa nae, na kama alikuwa shule basi huenda kuna ticha alikuwa anapata, maana maticha nao ni balaa tupu, tena msichana anavaa skuna nyeusi.ahh, sio ajabu ndio kipindi ambacho na mwalimu wa watu akamuona na kuopoa jumla

Yasinta Ngonyani said...

We usiye na jina una yako ambbayo hata mimi siyajui kabisaaaa! Ni hayo tu Ahsante!!!