Tuesday, October 20, 2009

KWA NINI TUNAWAPA WATOTO WETU MAJINA KAMA HAYA????

Ni juzi tu nilikuwa naongea na rafiki mmoja kuhusu majina. Nimeona niandike machache na tujadili kwa pamoja:-

Majina yenyewe ni kama haya:- Matokeo, Maneno, Sikujua, Zawadi, Mashaka, Matatizo, Asante, Baraka, Wasiwasi, Sikudhani, Shida, Huzuni, Halimoja, Majuto, Bahati, Mapambano, Tuombe, Maombi, Tumaini, Masikitiko, Maua nk.
Na huku kwetu kusini yaani Songea (wangoni) wanawaita watoto majina kama haya wa kike Kachiki na wa kiume Kadoda. Maana ya majina haya angalia kwenye kamusi ya kingoni:-)

20 comments:

chib said...

Afadhali kidogo majina ya kwetu, ukienda kwenye baadhi ya nchi za Asia ya kati, maana ya majina yao kama ukiweza kutafsiri, du yanatisha. Sababu kubwa ya kuwapa majina mabaya , ati mashetani watayachukia hayo majina kwa hiyo hawawezi kuwaingilia watu hao. Kule mtu kuitwa Bichwa, Mbwakoko, Mauti, Kikojozi nk ni kawaida. We utasikia mtu anaitwa Maung..., uliza tafsiri yake, he heeeeee

Mzee wa Changamoto said...

Wacha nirejee maoni ya mtu kwenye post yangu moja iliyofanana na hii.

Yasinta Ngonyani said...
inawezakana kwani ninakotoka mimi mtoto akilia sana hasa usiku eti analilia jina kwa hiyo wanamshikia kuku na kutaja majina yote ya mababu na mabibi waliokufa. Akinyamaza katika jina lile walilotaja basi ataitwa hivyo. Na pia hii mtoto kuitwa matatizo, huzuni, shida hutokea mara nyingi kama wazazi/familia wamepatwa na jambo la kusikitisha kabla ya mtoto kuzaliwa.

hizi ni fikra zangu

Maoni haya yalitolewa kwenye post iliyobandikwa tarehe 24 Nov 2008. Ikumbuke kwa kuisoma hapa
http://changamotoyetu.blogspot.com/2008/11/ni-kweli-majina-yetu-huathiri.html

viva afrika said...

hakika jibu kwa nini tunawapa watoto majina kama haya sina, ila naamini wakati mwingi majina yanaathiri mwenendo mzima wa mtoto husika.

Fadhy Mtanga said...

Majina kama hayo nadhani hayafai. Mi siyapendi na kila kitu.
Nimerudi wajameni.

Anonymous said...

Unachakuandika..funga blog

Simon Kitururu said...

Chochote awezacho kuitika mtu ni JINA!

Na kwa kuwa chochote chaweza kumkasirisha mtu , ni TUSI!

Na jamii zote zina majina ya ajabu kwa kuwa kitu chaa ajabu hutofautiana kutoka mtu na mtu , jamii na jamii!

Kuna waliokuwa wanamshangaa jina Rais Bush na hawajiulizi KIKWETE maana yake nini!:-(

Mwanasosholojia said...

Dada Yasinta, nafikiri kupeana majina kunaenda na utamaduni unaomithilisha mantiki kulingana na mazingira/maana/tukio n.k. Kusema jina fulani ni baya/ lina mkosi n.k nako kunaendana na tasfiri inayojengwa na utamaduni vile vile. majina haya si mabaya kwa vile yanaonesha tamaduni..ubaya unakuja pale tunapotafsiri kwa upande hasi tu.

Chacha Wambura said...

jina upewalo hata kama halina maana kwa mwenzio laweza kuwa na maana halisi katika maisha yako ya kila siku...lol!


Ukiitwa shida yawekana ukawa na shida ama ukwa shida hata kwa mkeo/mumeo...lol

John Mwaipopo said...

F. Mtanga majina mengine mboni mazuri tu hapo juu.

nadhani ni vema kuwapa watoto majina mazuri ama yenye kuashiria mambo mema. sidhani kama ni vema kumpa mtoto majina kama ya kizaramo ya havintishi, chuki, siwema n. eti kwa kuweka kumbukumbu ya tukio fulani. afanaleki! hivi mtoto wako ndio awe kumbukumbu ya mambo mabaya!

pamoja na yote majina nisiyoyapenda sana ni haya yafuatayo kwa kuwa hayaonyeshi utamaduni wa kiafrika:

John
simon
yasinta
yakobo
emmanuel
james
julius

nk

ninayoyapenda ni kama
alinanuswe
kadoda
muberwa
chacha
ghati
tulijako
nisajile
ndimbuni
babeiya
nk

Chacha Wambura said...

Mwaipopo mbona nawe unalo usolipenda na unalolipenda?...lol

kwa hiyo wewe ni vuguvugu?...lol

PASSION4FASHION.TZ said...

Hahahaha,umenikumbusha kadoda! kuna kaka mmoja mngoni tulikuwa tunamtania sana na hilo jina lake.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

eti twambie nini maana ya yasinta!!!!!!!!

naitwa Lutatinabigambobyabantukyomakyamukulanyondoetelaamabelelusindurankonge

na ninajua maana yake hilo

bora kuitwa mkosi na ukajua maanayake kuliko kuitwa majina ya wanaoaminika kuwa ni watakatifu ulimwenguni eti kwa kuwa walikubaka kiroho

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahaaaaaaaaa
Nimependa jina la Kamala. Yaani jina linaandikwa kwenye passport kisha unaambiwa "p.t.o" ili kumalizia ukurasa wa pili.
Hahahahaaaaaaaaaa

Chacha Wambura said...

Yasinta, kwa nini usitafute jina lingine je tukubatize?...lol

Yasinta Ngonyani said...

Ni furaha kuona maoni yanye mitazamo tofauti. Lakini ngoja niseme hivi mimi sijapanga kubadili jina na wala kubatizwa tena kwa mara ya pili. Kwanza nalipenda sana jina langu Kaka John wewe kama hulipenda sio mbaya lakini muhusika nalipenda sana tena sana tu. Na pia ni jina TAKATIFU sana nadhani wote mnakumbuka wale watoto watatu wa FATIMA. Jina langu halina maana mahimu zaidi ya Yasinta ni jina.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Na hapa je?

Masangu Matondo Nzuzullima Balya Malugu

Yasinta Ngonyani said...

Kaka! "Masangu Matondo Nzuzullima Balya Malugu" Je na jina lako hili ndefu lina maana gani?

John Mwaipopo said...

natamani ningekuwa na jina lenye mahadhi ya matondo nzuzulima

John Mwaipopo said...

natamani ningekuwa na jina lenye mahadhi ya matondo nzuzulima

Anonymous said...

Mimi naunga mkono kwamba sio lazima kubatizwa kwa mara ya pili.Binafsi naona muhimu kuwa na jina lenye maana fulani,tusijali lugha mama. Kwetu sisi tuna majina ya utoto/kifamilia typical kwa Wangoni (wakina Nakomba hao): Kadebedebe; Kadoda (mdogo wangu) na Kadala...sister wetu mpendwa wamwisho.