Friday, October 16, 2009

KUMUITA MKEO MAMA…AU MUMEO BABA KWELI….NI HAKI?


Ni kawaida sana kumsikia mke akimuita mume baba, au mume kumuita mke mama...jamani mbona yapo majina mengi ya kuitana kama vile mpenzi, kipenzi, habib, na mengine mengi. Na kama mna mtoto ndio rahisi zaidi yaani kumuita mama fulani au baba fulani. Ila si mama au baba. Mama anaheshima yake mambo yote unayoyafanya na mkeo kweli anastahili kuitwa mama??!...au unayoyafanya na mumeo unaweza muita mumeo baba???

Au hata majina ya ubatizo (ya kwanza) tuitane. Au kama kule kwetu kusini wanaitana vibongo yaani majina ya ukoo kama Na-Ngonyani, Na-Nyoni, Na-Komba nk. Na waBena/waHehe wao wanasema Sa au Se badala ya Na kwa hiyo itakuwa kwa wao. Sa-Mgaya, Sa-Mwageni, Sa-Mbilinyi kama kuna wabena na wahehe mnisaidie kama nimekosea. Na hiyo ya kuita Na na Sa ni kwa akina mama tu isije ukamwita mwanaume pia.

Pia sasa kuna mtindo wa kuwaita wazazi wetu babu na bibi yaani tunawita kama watoto wetu wanavyoita. Mara nyingi nimekuwa nawasikia watu wakisema ni bibi alipiga simu ukimuuliza bibi yako bado anaishi anasema hapana ni mama yangu lakini kwa vile watoto wanasema bibi /babu basi nami nasema hivyo. Na babu yako utamwitaje?
Naomba mnisaidie kufafanua hapo!!!!!!

15 comments:

chib said...

Mimi nafikiri ni heshima tu kati ya wana ndo kuitana hivyo na ni kwa watanzania.
Yaani ni kifupi cha baba nanihii na mama nanihii.
Usiwe na shaka Da Yasinta mumeo akikuita hivyo, hana maana ya kuwa sasa umekuwa kijeba. lol!

viva afrika said...

ondoa hofu da yasinta, kwangu mie naona fahari kumwita mke wangu mama kwa kuwa sasa yeye ndo anilea, anajua navaa nini, nakula nini naumwa ama mzima. nami kwake kadhalika.

Simon Kitururu said...

Mimi naamini kwa kawaida haya mambo hutokea tu ndani ya nyumba na wahusika huelewa unamaanisha nini. Naamini kabisa mtoto akimsikia baba naye anamuita mama yao mama huelewa kabisa anamaanisha nini.

Mambo mengine ni maneno tu na hakuna cha zaidi .

Kwani unafikiri kuna uhusiano gani kati ya mtu na jina aitwalo? Mi sidhani Simon na mimi tunauhusiano ingawa jina langu ni Simon a.k.a Mtakatifu Simon.:-)

Mambo mengine ukiyafikiria tu sana utastukia ni manjonjo tu ya binadamu kujua kutoa sauti ndio maana wanayatungia neno gumu wakati jina la kujamba kirahisi lingeeleweka tu kwa kuiga sauti yake PUUUUUH au chuiiiii na sio mpaka kutunga bomba la neno ambalo ukifikiria halina uhusiano na kitendo. [Samahani kwa mfano wa kitakatifu!:-(]


Nachojaribu kusema ni kuwa kama tu mtu azoeavyo kuwa jina lake ni Maimuna na kujihusishanisha nalo mpaka ukiliita anajua niyeye unamuitaji chobisi, ni staili hiyohiyo mtu hutambua kuwa ukimuita mama wakati sio mama yako hageuki.

Simon said...

ni heshima tu kati ya wana ndoa.
ni vizuri kuitana hizo..hiyo inaonesha ni jinsi gani wana ndoa hao wanapendana na kuheshimiana.

Chacha Wambura said...

Mtakavyombo Simon,nakubaliana nawe kabsaa. Inategemeana na muktadha wa kitu ama hicho unakitaja kina maana gani kwa wakati huo.


Viva Afrika, una maanisha mamsapu sivo, ha!

cheers

Chacha Wambura said...

YN, kwani wewe mumeo wamuitaje? honey ama baba?

just being curious!!!

Yasinta Ngonyani said...

Nimefurahi kusoma maoni yenu yenye karibu mtazamo sawa. Safi sana kila siku tunajifunza kitu. Asanteni sana wote kwa majibu yenu.

Kaka Chacha Wambura! labda nijibu swali lako mimi namwita mume wangu jina lake alilobatizwa au baba fulani:-)

Simon Kitururu said...

Swali la Kadinali Chacha Wambura lilinitisha kwa kuogopa jibu ambalo kirahisi lingeweza kujibiwa bila kubaniwa pua!

Yani Dada Yasinta unaheshima wewe!

malkiory said...

Mimi nadhani ni heshima zaidi kukamilisha kwa kusema baba fulani au mama fulani kuliko kuachia hewani.

Watoto wadogo ambao wako katika hatua ya kujifunza lugha wanaweza wasiwaelewe mnamaanisha nini kwa kitendo cha kuitana baba au mama kwa mke na mume.

Yasinta Ngonyani said...

Simon mtakatifu! Kubania pua:-) Na ni kweli mimi nia heshima sana si unajua mie nusu sister:-)

Malkiory! kwanza karibu sana hapa kibarazani kwangu. Na halafu nakubaliana nawe kabisa kwa nini nimwita mume wangu baba na watoto wangu wamwite baba. Hii hata kwa mimi inanichanganya sana

John Mwaipopo said...

mtu atamuacha baba yake na mama yake na kuenda kuanzisha nyumba yake katika ndoa na hao wawili watakuwa kitu kimoja.

kama wewe ni mwanamke unamwita mumeo 'baba' kureplace yule uliemwacha kule ulikozaliwa. vivo hivyo kama wew ni mwamaume unamwita mkeo mama kureplace yule aliyekuzaa kule ulikozaliwa. baba na mama ndio watu wako wa karibu.

kuhusu watoto kujifunza nini, potelea mbali hao wanapita tu. watajifunza mbele ya safari. kama tulivyopita kule tulikozaliwa. hapo sio kwao. ni wapita njia hao.

Yasinta Ngonyani said...

Mwaipopo umeifanya jumapili hii iwe ya kucheka kweli . "Watoto kujifunza potelea mbali"

Anonymous said...

hhahahah

Anonymous said...

kiislam uezi replace mama na mkeo na hapo kama ni ndoa mnaivunja

Anonymous said...

Usione ufahari kumuita mama haifai kabisa kumuita hilo jina