Friday, October 30, 2009

WIKI ILIYOPITA TULIONA MAJINA TUWAITAYO WATOTO WETU:- NGOJA LEO TUANGALIA MAJINA YA UBINI(VIB0NGO) TULIYONAYO!!

Hivi haya majina ya ukoo/ubini(vibongo) alianza kupata nani wanadamu, wanyama au ndege?

Ninekuwa nikijiuliza hili swali na nimewauliza watu wengi hivi haya majina tuliyonayo nani alianza kupata/kuitwa? Yaani kwa mfano:-Ngonyani, Nguruwe, Nyati, Tembo, Komba, Mwaipopo, Sungura, Soko, Mapunda, nyoka, kunguru, Mbawala, Kifaru. Tujadili pamoja......

10 comments:

John Mwaipopo said...

tehe! tehe! tehe! mpaka machozi. hivi umefikiria nini? tehe!

la kwangu ngoja nikamuulize baba.
ila hayo mengine yamekaakaa ki-nyumb-ii bomb-ii. tuwasikie wanaotoka huko.

nasikia siku za nyuma kiongozi mkuu wa nchi alitakiwa ale chakula cha mchana sehemu inaitwa Nakapanya.

ngoja tumsikilizi mtakatifu simon na profesa mbele.

you made my day today.

Chacha Wambura said...

hayo yote ni ya huko kwenyu wakishapata ugimbi a.k.a ze ulabu ama pingu-baha wanaita watoto wao majina hayo...lol

mbona wengine wanaita kutokana na matukio?

kwetu hapa utasikia majina kama:
magesa: alizaliwa wakati wa mavuno
marwa: wakati kuna ugimbi kwa hausi
magena: sijui kama walikuwa wanabeba mawe ama la...lol
chacha: jina la heshima kubwa apewalo mwana mzaliwa wa kwanza wa kiume ktk familia
matiku: wakati wa usiku
n.k.

je wewe lako lina maana gani? isijekuwa ikawa ni kulewa na kuwa chakari kama mkuu...lol

Unknown said...

wambura: wakati wa mvua
gati,robi nk

Simon Kitururu said...

Walianza watu kwa kuwa bado sijastukia Kuku , bata au chura tukiachilia mbali Mbwa wenye Ubini.

Kwa MTAZAMO WANGU:

Naamini ukiliangalia hili swala kwa kuwachukulia waaminio duniani familia ya kwanza ilikuwa ni ya Adam na Eva baada ya kuumbwa na MUNGU halafu kutolewa baruti bustani ya EDENI , basi jina la ukoo la kwanza lilikuwa ni Adam au Eva kutokana na kama walifuata mfumo wa patriarchal family au Matriarchal family .


Na walioanza kutumia ubini itakuwa ni Wajukuu wa Adamu na Eva ambao walitokana na watoto wa Adam na Eva kuingiliana KIMWILI wenyewe kwa wenyewe kutokana na kuwa hawakuwa na majirani ambao wangezini nao.

Kwa hiyo kwa waaminio stori za Biblia , nahisi ni akina Kaini, Abel ....nk ambayo ni majina ya watoto wa Adamu yaliyoanzisha umaarufu wa ubini ili Adamu na Eva wakati wamezeeka watambue hili jukuu lenye chogo ni toto la Kaini au Abeli nk.

Halafu nawasiwasi na hii familia ya kwanza kuhusu swala la mapenzi yao /Ngono , hasa ukizingatia inaonyesha kama hili swala la kaka na dada kuzaa ilikuwa ruksa,sasa huhisi labda Baba na Binti nayo ilikuwa poa tu?

Na bado sijui kwanini Mungu hakuwaumbia hawa jamaa wachumba wengine wakufanya nao uasherati ili wajaze dunia kama Biblia isemavyo kuwa ndio hasa sababu hiyo binadamu wanazalishana kwa uroda na walizaa kwa uchungu mpaka sikuhizi walipogundua kama Michael Jackson unaweza ukatotolesha toto maabara.:-(

DUH naacha fafanuzi nisijepigwa konzi bure kijiweni kwa mtu hapa!

Fadhy Mtanga said...

Duh ya leo kali. Mi jina langu limetoka mbali hata sijui wapi? Ninachokifahamu ni kuwa Mtanga lina maana inayokaribiana na Fadhili. Yote yanahusisha tabia ya kusaidia na kuwa na ukarimu.
Lakini hivi karibuni katika Facebook na Google nimegundua jina hili linatumika sana Malawi kusini na Zimbabwe. Sifahamu huko lina maana gani!
Lakini majina ya ubini mara nyingi asili na maana yake si wazi sana. Huo ni mtazamo wangu.
Ni hayo tu!

chib said...

Hayo ni majina ya wangoni. Nasikia asili yake ilikuwa mtoto akizaliwa basi mnyama wa kwanza atakayeonwa basi ndio jina la mtu hivyo kapewa. Tunashukuru walikuwa na busara, maana ingekuwa ni kitu cha kwanza kinachoonekana ndio jina la mtoto, basi mengine yangekuwa haya andikiki achana mbali na kutamkika :-(

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yep majina yetu yanatokana na mazingira na matukio. hata wazungu kwa mfano smith ni wale waunzi. kuna shumeka (shoemaker) nk

sasa langu kwa mfano ni kamala (stabiliser, finisher, slover) Lutatinisibwa (nonfreightenable, hero, gwiji, mshindi)

naambiwa niliitwa Lutatinisibwa kama ujumbe wa baba kwa babu kuwa hatishiwi Nyau. babu angekuwa hai ningelifuta jina hili.

baba aliitwa Lutabasibwa yaani hawezekaniki. kuna kiburi, ubabe na majigambo katika majina ya wahaya zaidi

Anonymous said...

Kuna Kibwengo, naomba pia kaka Kitururu ulitafakari na hili maana watu wanakuwa kma Vibwengwo haswa kuna mdada tulisoma nae UD enzi hizo kiukweli yule Cjui yu wapi?Maana ni Kibwengo wa tabia maaana mmmhhhhh

Mzee wa Changamoto said...

Niliposoma hapa jana nikaenda kutafakari kiasi. Kisha nikaingia mazoezini. Nikikutana na mbwa namuita "mbwa" na hageuki. Nikikutana na paka nakuita PAKA na hageuki. Ila mtu ukisema "mtu" atageuka tu japo kujua kama aitwaye ni yeye.
Kwa hiyo kwa akili yangu (ya matope) nimegundua kuwa sisi ndio tujuao kuwa Komba ni Komba japo yeye hajijui na hajihesabu kama Komba. Yaani Nyani hajijui kuwa nyani wala nyoka
Kwa hiyo sio tu majina haya yameanza kwa binadamu, bali bado ni UTAMBULISHO KWA BINADAMU kwani wanyama waitwao majina haya hawayajui wala hawayatumii
Kwa hiyo si majina ya wanyama, ni "namna (sisi binadamu) tujikaririshavyo kuwakumbuka na kuwatenganisha wanyama ilhali wao wanajuana kwa namna na (pengine) majina mengine."
Blessings

Yasinta Ngonyani said...

Asanteni wote. Nadhani hata mie nifanye kama Mwaipopo naenda Ruhuwiko kumuuliza baba Ngonyani maana yake nini. Ngo - Nyani labda inawezekana nina ukoo na Nyani...lol, kaazii kwelikweli