Monday, October 12, 2009

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA DA SUBI!!


Ni furaha kuwa na rafiki kama Da Subi na leo ni siku tukufu kwako. Ni siku ambayo ulitokea hapa duniani . Napenda kukutakia yote mema, uishi miaka mingi uwe bibi kizee na wajukuu wengi uwe nao. Subi ni mtu mtukutu sana kwa hilo nakuheshimu na pia nakupenda sana .HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA RAFIKI YANGU!!!!!!

17 comments:

viva afrika said...

hongera sana da subi, hakika ni kheri na fanaka nikutakiazo kwa siku hii muhimu maishani mwako. epi besdei da subi.

Markus Mpangala. said...

HERI TITI ULILONYONYA, HERI TUMBO LILILOKUZAA, HERI WAZAZI WALIOKULEA......AMANI KWAO WATU HAO.....

Fadhy Mtanga said...

Hongera sana da Subi. Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu uwe na maisha marefu yaliyojaa afya njema, amani, furaha na mafanikio.
Ubarikiwe sana.

Anonymous said...

Du, nimekutangulia siku moja tu, mimi nimesherekea jana. Hongera sana kwa siku ya kuzaliwa, hakika leo ni siku muhimu sana kwako, du, hizi sherehe zinatukumbusha majukumu yanayoendana na umri! waswahili wanasema "cheza ngoma angalia jua" giza lisijekukuta bado unacheza!

chib said...

Kumbe tupo wengi kwenye tarehe ya leo. Pongezi nyingi Subi, mie nimesheherekea na kusherehesha

Subi Nukta said...

Loh, jamani, ni furaha ya ajabu kupata baraka ya marafiki na watu wanaokukumbuka hasa katika sikukuu yako ya kuzaliwa, siku inayosababisha wewe kuwepo duniani.
Basi natoa shukrani za dhani.
Namwomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema akupeni baraka na mafanikio tele kadiri ya kipimo kile kile cha heri mlichonitakia.
Mfanikiwe katika mengi mnayoyatenda!

Da Yasinta, ninakushukuru kwa namna ya kipekee kwa kunikumbuka hivi na kwa kunipa nafasi kwenye blogu yako. Shukrani sana jirani na rafiki yangu mpendwa!

Unknown said...

Jamani naamini sijachelewa, nami dada subi nakutakia kila la kheri katika kusherehekea sikukuu yako ya kuzaliwa.... mungu akujalie afya njema na maisha mema yenye furaha

Simon Kitururu said...

Hongera Da SUBI!

Bila kukusahau Mkuu CHIB, honera na wewe kwa siku ya kuzaliwa!

chib said...

Nitakuwa mchoyo wa fadhili kama sitakushukuru Simon kwa kunipa hongera katika blogu hii.

mumyhery said...

happy birthday Subi

Subi Nukta said...

Ninawiwa wingi wa shukrani kwa Shabani, Simon na MumyHery.
Shukran. Mwenyezi Mungu akupeni heri katika ulimwengu huu na ule ujao!

Faustine said...

Hongera Mdau! Nakutakia kila la kheri katika kusherehekea sikukuu yako ya kuzaliwa.... Mwenyezi Mungu akujalie afya njema na furaha tele.

Subi Nukta said...

Shukran Dr. Fau kwa salam za heri kwa sikukuu yangu. Inshaallah, Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na akubariki kadiri ya kipimo kile ulichonibariki kwacho na ziada!

Mzee wa Changamoto said...

Kama kuna kauli kali basi ni ya Anon October 12, 5:29PM ambaye namnukuu hapa akisema ""cheza ngoma angalia jua" giza lisijekukuta bado unacheza!"

Ni kauli yenye nguvu na naamini Da Subi unacheza ukiangalia jua. Kama nawe ni mvivu wa kugeuza kichwa juu kuangalia, weka bseni la maji utaona tu jua likizama.
Lol
Heri kwako Dada

Yasinta Ngonyani said...

Ni furaha kuona jindi tunavyoishi, Napenda kusema namshukuru mmtu aliyeanzisha hizi blog. Leo wanablog wote tumekuwa familia moja maana tumeshikamana na tunapendana tukiwa na shida pia furaha. Heri sana kwa siku ya kuzaliwa Da Subi na kama nilivyosema nakutakia maisha marefu mpaka uwe bibi kizee. UBARIKIWE SANA.

malkiory said...

Pamoja na kuchelewa kuweka wino hapa,kwa moyo mkunjufu napenda kuwapongeza wote mliomtakia mema siku yake ya kuzaliwa dada Subi.

Subi, mungu akujalie afya njema. Kama siyo wewe Subi nadhani blog yangu isingeweza kuwa kwenye sura iliyonayo sasa.

Subi Nukta said...

Mzee, nimekusoma, ushauri kuzingatiwa.
Asante sana Da Yasinta!
Malkiory? kisa hata upotee hivyo ni kipi? loh, umekuwa adimu kama shilingi ya Mdachi bwana? ha ha hah, afadhali umerejea ukumbini. Shukrani kwa salam, natumai tutaendelea kupata posti kwenye blogu yakko.
Shukrani nyote!