Friday, October 16, 2009

TUSISAHAU UTAMADUNI WETU TINGATINGA (BATTIK) NI KAZI YA MIKONO YETU/NI UBUNIFU WETU

Hapa naona kazi zimezidi kidogo lakini tutafika tu.

Sisi ni wamoja tunatwanga

Na sisi pia tunatoka kuchota maji
Ni mapambo lakini pia yana maelezo yake kwa hiyo inakuwa raha katika nyumba kuwa na mapambo kama haya. NAPENDA KUWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA KWA PICHA/TINGATINGA/BATIKI HIZI.
UKITAKA KUJUA MENGI USISITE KUULIZA.


3 comments:

Chacha Wambura said...

ni nzuri lakini duh!!

ubunifu wa hali ya juu. Laiti tungeweza kupenda vya kwetu mambo yangekuwa saaafi sana.

lakini ndo hivyo tena...vyathaminiwa na wageni nasi twathamini vya wasungu...lol

Bennet said...

Hizi picha wananunua zaidi wageni, sisi wenyewe kama vilivyo vivutio vya utalii na hata picha zetu pia huwa hatuna muda nao
picha nzuri sana kwa kweli

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kabisa Chacha Wambura usemavyo. Na nasikitika kwa hili kwasababu kila mara tunaona kitokacho nje ndo kizuri kuliko tulichonacho wenyewe.

Kaka Bennet, nwe umenena na kweli ni picha nzuri sana. Ila mimi nitauendeleza utamaduni wangu hizo ninazo hapa na najivunia sana maana nautangaza utamaduni wangu.