Saturday, October 10, 2009

URAIA WA NCHI MBILI

Kwa Pro. Mbele nimesoma kuhusu watu kuwa na uraia wa nchi mbili. Kwa hapa Sweden sheria ni kwamba ukisha ishi mika 5 unaruhusiwa kuwa raia wa nchi. Kwa mimi sioni umuhimu wa kuwa raia wa nchi nyingine kwa hiyo mimi bado ni raia wa nchi moja na nina passport ile ya kijani.

Watoto wetu ni raia wa Sweden tu. Huwa tunapata shida sana kuomba ruhusa (VIZA) kwenda TZ kwani kwa wao na baba yao wanaruhusiwa kuwa ndani ya nchi miezi mitatu tu. Lakini mimi sihitaji ruhusa.

Ila ningefurahi sana kama kungekuwa na hii sheria ya uraia wa nchi mbili hapo ndiyo ningechukua nafasi na kuwa raia wa nchi mbili. Ila sasa hapana, mimi ni mTanzania tu. Kwa undani zaidi soma blog ya Pro. Mbele URAIA WA NCHI MBILI

8 comments:

ERNEST B. MAKULILO said...

Nashukuru kwa mada hii dada. Nimekwenda pia kusoma kwa Prof Mbele, na maoni ya mdau mmoja aliyeweka comment yake pale.

Kwanza kabisa, suala la uraia wa nchi mbili mimi nadhani ziwekwe sababu za ukweli na si kuzungushana. Maana kuna hoja ambayo inatawala isemayo kuwa uraia wa nchi mbili utaleta uwekezaji Tanzania. Nataka kujua kivipi uwekezaji huo utafanyika kupitia uraia wa nchi mbili?

Mtazamo wangu, hili libaki suala la maamuzi ya mtu binafsi, kama unapenda kuwa mtanzania kuwa, na kama unataka kuwa mmarekani, mwingereza au mfaransa nk kuwa. Maana hili mimi naliona ni faida binafsi, hivyo mtu unabidi uangalie cost-benefit analysis ya wapi unapapenda na unafaidika zaidi, na si kudanganyana hapa kuwa kutaongeza uwekezaje.

Vile vile, suala la serikali la Tanzania kuwanyanyasa na kuwatesa watanzania hasa watoto na vijana wakuao hili nalo linaongexza wimbi la watu kuichukia nchi yao. Mfano, mtu kasoma elimu ya sasa ya mkopo vyuoni, na si ile ya zamani mambo shwari, pia kupata kazi unasaka zaidi ya mwaka, na ukiipata kama wewe ni mwalimu au nesi unaambia ni kazi ya wito, hivyo unasubiria miezi 3 na kuendelea kupata mshahara wako. Fikiria mtu huyu afike ughaibuni na mambo yaende vizuri, hamu ya kuwekeza huko bongo itatoka wapi?Anajua kabisa ili uwekeze lazima utoe rushwa, ujipange na wanasiasa vyema nk.

MAKULILO, Jr.
www.makulilo.blogspot.com
San Diego, CA

ERNEST B. MAKULILO said...

Napenda kuweka maelezo yafuatayo yakifuatiwa na nukuu moja muhimu ambayo nayo inahusu mambo ya uraia.

When Adolf Hitler came into power as Germany's new chancellor, Eistein (Albert) then promtly resigned from academic positions in Berlin, renounced his German citizenship, and went into exile. A statement at this time said, in part: "AS LONG AS I HAVE ANY CHOICE, I WILL ONLY STAY IN A COUNTRY WHERE POLITICAL LIBERTY, TOLERATION, AND EQUALITY OF ALL CITIZENS BEFORE THE LAW ARE THE RULE".

Maelezo hayo na nukuu hiyo najifunza mambo makuu yafuatayo. Uraia wa nchi fulani si kitu lazima uishi nacho mpaka ufe nacho. Ni kwamba unaweza kuwa nacho, ukakipenda au ukakikataa kama unayo choice, na choice hiyo ni bora kuliko uliyonayo.

Pili, kuna sababu zinazoletwa na tawala kufanya watu wachukie nchi zao hivyo kuamua kuchukua uraia wa nchi nyingine. Hapo Eistein amekumbana na ubabe wa Hitler ambao unaonekana. Na Tanzania kuna ubabe kama wa Hitler inategemeana unatumia lenzi ipi kuangalia na upo angle gani kuona.

Uraia wa nchi fulani, kuipenda au kuichukia nchi hiyo ni suala binafsi. Mapenzi sio lazima umpende mtu au kitu mwanzo mwisho bila kuhoji au kuchukiana.Mfano, kwa wale ambao walisoma kipindi cha kina Nyerere wakala matunda ya uhuru, elimu bure, shuleni/vyuoni chumba mtu mmoja au wawili, hakuna kubebana, wanakunywa maziwa mpaka kusaza...wakafanya migomo ya kukosa blue-bank (kama Samweli Sitta) nk, watu hao watakuwa wanaipenda sana nchi ya Tanzania kwani kuna mema mengi iliafanyia mpaka kufikia hapo walipo.Watu hao kila wakati watahubiri suala la uzalendo na watu kuipenda nchi yao na kuwa watanzania daima mpaka kufa kwao. Lakini kwa kizazi hiki cha sasa, mtu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu anajilipia mwenyewe, hana deni na serikali, hana cha kuona ana deni la kufanya kwa watu wengi wa Tanzania kwani akifanya tafakuri kwani njia aliyopita hakupata msaada wa serikali au jamii yote, alitumia nguvu zake na wazazi na ndugu, basi mtu mtu huyo mapenzi yake kwa nchi ya Tanzania ni madogo, na akiamua kuchukua uraia wa nchi nyingine asilaumiwe kwani mfumo umemlazimu ili awe furahani na kutimiza mahitaji yake.

MAKULILO, Jr.
www.makulilo.blogspot.com
San Diego, CA

chib said...

Makulilo, kwa kweli nimekuelewa kabisa. Mawazo yako yangekuwa yanasomwa na hao walioshika mpini, nafikiri tungekuwa mbali.

Anonymous said...

Mjadala wa uraia wa nchi mbili umejaa sana faida binafsi na sio manufaa kwa nchi kama hao wanaojidai kuupigia debe wanavyodai. eti uwekezeji na kadhalika, nani kasema hayo. watu huwa wanaelezea kwamba Tz itafaidika sana na hiyo kitu, lakini hawajui kwamba sio watanzania wote wana uwezo wa kuwa na huo uraia wa nchi mbili. sana sana watakao faidika ni hao hao wajanja, mafisadi watakuwa na jeuri ya kuiba kwetu na kukimbilia nchi nyingine. nakumbuka kuna kiongozi mmoja tuliwahi kuambiwa alikuwa na uraia wa nchi nyingine ndio alienda huko kutibiwa, akafia huko na kuzikwa huko huku akiacha skandali kubwa tu Tanzania, nadhani hao wabalozi wa huu mpango wanataka kufanya hivyo pia.

Simon Kitururu said...

Na nyege kweli ya kuwa raia wa nchi tatu kama hata maana ya nchi moja imenisaidia FAFANUZI Zanzibar ni Tanzania:-(

Mbele said...

Dada Yasinta, nafurahi kwa uamuzi wako wa kuiweka makala yangu hapo kwako, tuwasikie wadau wanavyotema cheche :-)

sanga said...

Haya niliandika kwenye page ya Prof. Mbele.

Prof. Mbele asante sana kwa huu mjadala wa uraia wa nchi mbili. Kwa kweli umeandika vizuri na umeeleza wazi msimamo wako na mtanzamo wako.

Najua umeongea kipengere cha waTanzania wanadai kwamba wakiwa raia wa nchi mbili watawekeza Tanzania umesema hudhani kwamba hii ni kweli lakini umeacha kwamba utafiti zaidi inabidi ufanyike. Hapa mimi nitakuwa wazi kwamba kwa uchunguzi wa kina ambao mimi mwenyewe nimefanya ni kwamba watanzania hata wawe na uraia wa nchi mbili HII HAIWEZI kuongeza uwekezaji Tanzania au kuwafanya wawekeze Tanzania. Hii ni kisingizio tuu cha sisi watanzania katafuta visababu ambavyo wala havina msingi na havina logic yeyote. Hivi leo hii nini kinanizuia mimi nisiwekeze Tanzania? Na hivyo hivyo nini kinamsumbua bwana Kyando wa kanada kuwekeza Tanzania? Mbona kuna watu wengi tuu wanawekeza Tz ambao siyo raia watanzania? Nilibahatika kwenda Zanzibar mwaka 1990 na kukaa pwani ya mashariki ya visiwa hivi hakukuwa na ujenzi wowote ule. Leo hii nimekwenda pale tena kuna hoteli nyingi mpya zimejengwa na eneo lote limechukuliwa sasa na wamarekani, wasomali, wa-Ulaya (European), wahindi na wengine. Hawa wote siyo watanzania na sisi watanzania tunabaki na visingizio tuu kwamba tuwe na uraia wa nchi mbili.

Sababu kubwa watu wengi hawasemi ni kwamba hawapo tayari na usumbufu wa kutafuta visa wakati wa kurudi Tanzania na wengine kama waliopo hapa Marekani pengine ingekuwa wa-save $100 ya visa. Najua hapa nifanya uchokozi lakini huu ndiyo ukweli wenyewe.

Pengine kuna sababu zingine ambazo watu wanataka kuwa raia wa nchi mbili lakini sababu ya kwamba kutokuwa raia wa nchi mbili kunazuia uwezekaji ni sababu tuu ya kisiasa at best kuliko kwamba ni sababu ya msingi. Nani asiyejua kwamba wale wahindi wote wa Iringa au Dar siyo raia wa Tanzania ki-ukweli isipokuwa tuu kuwa na passport kwa jina tuu? Sasa kweli wewe mtanzania mwenye bibi yako na babu yako mnyalukolo mtu akuzuie kuwekeza Tanzania? Pia ukweli niTanzania wangapi kweli watawekeza kama wakipewa uraia sehemu zote mbili? Je wamewekeza huko waliko? Enterprenuship ipo kwenye damu za watu na mazingira. Kizazi cha sisi tuliotoka kwenye ujamaa kwa kweli ni vigumu sana kuwa wawekezaji pengine tuombe mungu kwamba kizazi cha sasa hivi mungu akijalie kweli wawe wawekezaji kama walivyowasomali na wakenya. Kizazi cha ujamaa tunajua sana kuongea lakini vitendo almost hakuna. Kila siku vikao lakini hakuna utekelezaji.

Pengine nirudi kwenye kwenye kipengere cha kiapo cha uraia wa marekani. Ni kweli mtu unakula kiapo cha kuwa ni raia wa nchi ya marekani na kwamba utapigia nchi ya marekani. Sasa hapa ni swala la mtu kuangalia tuu uwezekani wa nchi yako kweli kupigana na marekani. Mimi binafsi sidhani kwamba kuna siku moja at least in my life time kwamba Tanzania itapigana na Marekani kwa hiyo mtu inatakiwa uchague nchi gani utapigania. Ila nchi zingine kama wakati wa vita baridi ukitoka urusi pengine kweli you have to consider hii possibility very serious. Au kwa miaka ya nyuma au mbele kama mtu umetoka china bado kuna possibility kwamba siku moja unaweza ukaambiwa kwamba China na marekani zipo vitani na wewe lazima upiganie upande wa marekani (hii kwa sasa inaendelea kuwa remote possibility) lakini inaweza kutokea. Ukiwa raia umetoka Iran or North korea kweli inaweza kutokea. Chukulia baadhi ya askari wa jeshi la marekani ambao asiri yao ni Iraq waliweza kwenda kupigana kule chini ya jeshi la marekani.

Ukiacha hilo la vita kuwa raia wa marekani na nchi nyingine siyo gumu kama ambavyo wengine wanasema. Chukulia wayahudi wengi nchi hii ni raia wa marekani na Israeli lakini huoni matatizo yeyote ya msingi ambayo yanawakumba. Vivyo hivyo raia wengi wa wenye asili ya India ni raia wa India pia raia wa marekani na sidhani kama unasikia matatizo mengi.

Mwisho napenda kusema asante kwa kuandika kwa uwazi juu ya swala hili ambalo mara nyingi linaongelewa katika muundo wa ushabiki bila kuwa na analysis yakutosha. Samahani kwamba nimechanganya kiswahili na kingereza that in part is my laziness.

Yasinta Ngonyani said...

Asanten sana kwa kutoa michango yenu. kwa kweli ni changamoto nzuri sana. Na naona mmesema yote ila nami nisime tu ya kwamba,mimi kama nilivyosema sijatarajia kuchukua uraia wa nchi nyingine zaidi ya huu nilionao na najivunia sana. Nitabaki kuwa mTanzania mpaka nakufa.