Saturday, August 30, 2014

PICHA YA WIKI...SEHEMU FULANI TANZANIA..JE? UNAJUA WAPI?

Nimeipenda hii picha na nimeiona iwe picha ya wiki hii haya sema kama unajua hapa ni wapi?:-) ni mimi Kapulya wenu:-)

Friday, August 29, 2014

NAPENDA KUWATAKIENI MWISHO MWEMA NA KIPANDE HIKI CHA MZIKI ........ASILI YA MZIKI


Hakuna mwanamziki ambaye alikuwa akimba na wengi wakimwelewa anasema nini. Katika nyumba hii Remmy anapendwa sana...kwa hiyo nimeona leo tumkumbuke/tumuenzi. MWISHO WA JUMA UWE MWEMA KWENU!!

Wednesday, August 27, 2014

MSIMU WA MAVUNO UMEFIKA /YAANI MWISHO WA BUSTANI KWA MWAKA HUU NA HAYA NDIYO BAADHI YA MATOKEO....!!!!

 viazi mviringo (sisi wangongo twasema matosani)
 Vitunguu saumu/swaumu
Na hapa ni vitunguu maji / au ni vitunguu vya kawaida
NAWATAKIENI SIKU NA KAZI NJEMA

Monday, August 25, 2014

HUU NDIO MLO WANGU WA LEO MCHANA SUPU YA BROCCOLI....

 Broccoli kabla haijachemchwa
Na hapa tayari  supu...nimechemsha dakika kama tano halafu nimemix na hapa tayari kuliwa na kiteremshio ni maji . KARIBUNI MJUMUIKE NAMI!!

Saturday, August 23, 2014

Thursday, August 21, 2014

KISWAHILI:- METHALI ZETU!!

1. Usimwamshe aliyelala, utalala wewe.
2. Usipoziba ufa utajenga ukuta.
3. Usitukane mkunga na uzazi bado.
4. Uso mzuri hauhitaji urembo.
5. Vikombe vikaka pamoja havina budi kugombana.
6. Waraka ni nusu ya kuonana.
7. Wagombanao ndio wapatanao.
8. Usiache mbachao kwa msala upitao.
9. Mchumia juani, hula kivulini.
10. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
Ni hizi tu kwa leo ila nawe kama una mojo, mbili tatu usisite kuweka hapa eilimu ni kugawana. Haya siku na kazi njema . Wenu Kapulya:-)

Tuesday, August 19, 2014

BUSTANI YETU INAVYOENDELEA SIJALIMA MBOGA MBOGA TU NIMALIMA NA.......

 Mahindi na sasa yamechanua ila nina wasiwasi kama nitakula maana bado hayajabeba :-)
 Kule kwetu Litumbandyosi tunalima sana Karanga kwa hiyo nikaona niendeleze kilimo..
 Na kulima mboga bila kiungo/pilipili si safi sana na hapa nilijaribu na matokeo yake ni kama muonavyo.
..na bila kusahau nyanya  nazo sasa ndo zinaanza kuiva na tumeshaanza kula...kazi ya mikono yangu/yetu mwenyewe/wenyewe.

Sunday, August 17, 2014

KUMBUKUMBU YA MAMA ALANA NGONYANI NI MIKA KUMI IMETIMIA TANGU ATOTEKE!!!


MAREHEMU MAMA ALANA NGONYANI 1952-2004
Imetimia miaka 10 tangu ututoke ghafla usiku wa tarehe 17 Agosti 2004 wakati bado tulikuwa tunakuhitaji. Ingawaje kimwili umetutoka, kiroho bado tunakukumbuka. Tunakukumbuka siku zote kwa upendo wako, mawazo yako yaliyojaa busara , ukarimu/ucheshi na malezi bora. Tulikupenda lakini Mungu alikupenda zaidi.
Tunamwomba Mwenyezi Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi. AMINA
Na tumkumbuke mama yetu kwa wimbo huu
TUTAKUKUMBUKA DAIMA MAMA

Saturday, August 16, 2014

JUMAMOSI YA LEO NA USEMI /UJUMBE HUU!!!

Mimi ni mmoja, lakini mimi ni mmoja tu. Mimi siwezi kufanya kila kitu, lakini hata hivyo naweza kufanya kitu fulani.
JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE!!

Thursday, August 14, 2014

NI CHAGUA LA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA HII IWE PICHA YA WIKI ..UREMBO!!!

Kama watu wasemavyo ukitaka kupendeza basi  inabidi uvumilie....na urembo hauna utoto wala uzee. Nimependa hii picha maana ipo kiasili kabisa. Ila sijui anavua anapolala?

Wednesday, August 13, 2014

SWALI /TAFAKARI LANGU/YANGU LA/YA LEO ....NAOMBA TUTAFAKATI PAMOJA

Swali langu la leo:- Hivi tusemapo  NI MTU NA MJOMBA WAKE au Ni MTU NA SHANGAZI YAKE.
 JE? kati ya hao  MTU NI NANI NA MJOMBA/SHANGAZI  NI YUPI?
HAYA KILA LA KHERI  TUPO PAMOJA.....Kapulya wenu.

Tuesday, August 12, 2014

BAADA YA KUWA LIKIZO .....BUSTANINI/ MBOGA YA MABOGA IMEFUNGA/STAWI MNO:-)

 Nikaona niichuma kama muunavyo hapa na kuifanyia kazi ...nikapata kiasi hiki. Basi nikaichambua .....
 ....nikaikatatakata  kama muonavyo katika picha , wakati huo nishaweka maji katika sufuria ...
 ...ipo ndani ya sufuria ili ishemshwe kwa muda wa dadika 2-5
 na hapa baada ya dakika 2-5 inaonekana hivi, baada ya hapa nasubiri ipoe na halafu
...naiweka katika mifuko kwa ajili ya akiba  na pia naandika tarehe na ni mboga aina gani, baada ya hapo ni kuweka kwenye friza(freeze) ...mjanja  eehhh:-)

Sunday, August 10, 2014

MSIONE KIMYA NIPO...NIPO KAMA NILIVYOSEMA LIKIZO AMBAO MUDA MZURI KUWA NA FAMILIA....NIPO!

Kwanza nisema habari za siku mbili -tatu au niseme za wiki nzima bila kuwa nanyi.. nilikuwa nikisafisha macho na kujifunza kidogo historia. Ila sasa nimerudi na nipo nanyi....naweka picha kidogo kuonyesha wapi nilikuwa. Nimewamiss ndugu zanguni.

 Hapa ni mitaani ndani ya Nchi ya Estonia. Kwa kweli nimesafisha macho sana na pia kupumzisha akili.
Haikuwa muda mrefu nilikuwa kule na hapa sasa narudi tena ila duh!....na sasa Likizo imekwisha wiki ijayo ni mtindo mmoja kubeba maboxi:-) JUMAPILI/DOMINIKA NJEMA  KWA WOTE...!!!